Bi. Senti 50
JF-Expert Member
- Apr 17, 2007
- 290
- 12
inaoekana kuna njia moja tu ya kufind out, liwalo na liwe.
Dr. Salim - Bila ya shaka kabla ya Dr. Migiro Dr. Salim alikuwa ni mwanadiplomasia maarufu zaidi ambayo Tanzania imewahi kumtoa. Mchango wake Katika Baraza la Umoja wa Mataifa na utumishi wake kule OAU unajulikana. Hapa nyumbani hata hivyo, Dr. Salim alikuwa ni kama mtu wa hadithi, masimulizi mengi ya jinsi alivyojiendeleza mwenyewe kielimu na kuaminiwa na serikali yake akiwa na umri mdogo ni vitu vinavyojulika. Utumishi wake katika Jamhuri akiwa Waziri wa Ulinzi na Waziri Mkuu viliwafanya watu wengi waamini kuwa alikuwa ni kipenzi cha Mwalimu na bila ya shaka alikuwa anaandaliwa kuwa Rais wa Jamhuri.
WAkati ulipofikia na mara moja alipoonesha nia ya kutaka kugombea na baadaye kugombea mchezo mchafu ulipikwa uliomhusisha Dr. Salim na mauaji ya Rais wa Zanzibar Bw. Karume na wengine kumshirikisha na chama cha Hizbu. Alipotokea kujitetea alikuwa amechelewa kwani the damage was already done. Kitendo cha Dr. Salim kushindwa kujitetea na kukemea mchezo mchafu aliochezewa kimemwacha akiwa hana interests na siasa za Tanzania na amebakia kuwa "mzungumzaji" katika medani za Kimataifa huku akiongoza taasisi ya Mwalimu. Kwa ujumla, Dr. Salim atakumbukwa kama mwanasiasa aliyefyata mkia na aliyekosa ujasiri wa kutetea hadhi na heshima yake na kuwaumbua wale wote waliofanikiwa kumwangusha kisiasa. Kwa ufupi, Dr. Salim ni failure wa kisiasa za nyumbani.
Dr. Malecela. Huyu kama Dr. Salim alikuwa ni kipenzi cha mwalimu na bila shaka alijitengenezea mtandao mkubwa wa wafuasi waaminifu. Kuchaguliwa kwake kwa kura nyingi ilidhihirisha mapenzi ya wanaCCM wengi kwake. Miaka yake ya Uwaziri na Uwaziri Mkuu haikumbukwi kwa kitu chochote muhimu au maamuzi yoyote ya kijasiri. Kosa kubwa alilolifanya na ambalo hadi leo limebakia kuwa doa ni kitendo cha kuruhusu hoja ya Tanganyika kuletwa Bungeni. Kitendo hicho na kile cha kuruhusu Tanzania kujiunga IOC kilimtibulia nafasi yoyote ya upendeleo aliyokuwa nayo kwa Mwalimu. Mwalimu alimkemea hadharani na tangu siku ile nyota yake katika uongozi wa kitaifa ilianza kuzima. Hata alipojaribu kuweka jina lake kwenye kugombea Urais alijikuta akipingwa wazi na Mwalimu na hata baadaye baada ya mwalimu kuondoka vyombo vya juu vya CCM vilimnyima kabisa nafasi. Inadaiwa mara ya mwisho baada ya jina lake kuenguliwa Dr. Malecela alitaka kukata rufaa. Dr. Malecela kama alivyofanya Dr. Salim alishindwa kufight back na kutetea rekodi yake au kusahihisha misemo yake ya kejeli aliyoitoa huko nyuma ambayo watanzania hadi hii leo hawajamsamehe. Ingawa wananchi wa jimbo lake wameendelea kuonesha imani kwake, kitaifa Malecela kama Salim ni failure wa kisiasa. Kilichobakia kwake ni kubeza na kukejeli wapinzani kwani ndani ya CCM hana ubavu wa kupata atakalo. Kwa ufupi, Dr. Malecela naye hatakumbukwa kwa makuu yoyote aliyoifanyia nchi yetu bali kwa atakumbukwa kama mwanasiasa aliyejitibulia mwenyewe na akalipa gharama kubwa ya kisiasa kwa kufanya hivyo.
so, into oblivion? jibu langu ni ndiyo mzee, ingawa wangeweza kukwepa.
Asanteni sana.