Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
- Thread starter
- #61
unachokiongea ni kweli kbs ila nina waiswasi na muafaka huo, je tuko tayari kuwaachia hilo ziwa? wako tayari kutuachia kipande tuchukue ili hali wanaamini kuwa ziwa lote ni la kwao?, je wananchi wao watalubali kipande cha ziwa kiwe mali ya tz? je watz watakubali ziwa lote liwe la malawi?...hapo bado kazi ipo..ikishindikana njia ya kawaida inabidi mafahali wawili waiingie ulingoni na atakaye shindwa ndio akubali kumwachia mwenzie...
Wamalawi wako makini sana katika kuamua hatima yao. Nimesoma magazeti na blogs zao nyingi za kwao nimegundua wamalawi wengi wako against vita baina yao na sisi, na wengi wanatutambua kama majirani zao wa karibu na wa siku nyingi. Wapo walevi wachache kama i(ilivyo huku) pia wanaoshabikia vita. Nionavyo serikali yao imepima upepo na kuligundua hilo, kwamba vita kamwe haitakuwa kwa maslahi ya wamalawi wala watanzania; ndiyo maana wameamua kulipeleka suala hili mbele ya vyombo vya kisheria vya kimataifa ili kupata suluhu. Binafsi nazipongeza hatua za hivi karibuni za serikali ya Malawi kuongeza mahusiano yake na sisi na nashauri sisi pia tufanye hivyo ili kuepusha uhasama usio wa lazima uliozalishwa na historia yetu ya kutawaliwa. Wote, wamalawi na watanzania wana madai ya haki kabisa kudai kama wanavyodai; Mkoloni alikabidhi Nyasaland ramani inayoonyesha nchi hiyo kumiliki ziwa lote, kwetu alikabidhi ramani ambapo Tanzania ilionekana kumiliki nusu ya eneo la maji ya ziwa na UN baadae walithibitisha nadharia ya umilikaji wa nusu ya eneo la maji pale ambapo mipaka ya nchi inakutana na ziwa au maji. Ni kwa mantiki hayo inapaswa pande zote kuketi na kuzungumza nini kifanyike ili udugu na ushirikiano uliodumu karne nyingi uendelee. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.