uzuri wa intelijensia, kila kitu kinakusanywa na kufanyiwa analysis na baada ya hapo ndio wenyewe wanaita classified info...sasa hapa wanakusanya kila wakionacho na mwisho wa siku wanaunganisha dts kupata habari kamili...tusiwa-undermine. leo madame wao katangaza kuwa hatapenda nchi hizi zinaingia vitani kwa sababu ya ziwa malawi, anasema atatumia diplomatic ways kumaliza tatizo,je, iwapo tutang'ang'ania kumiliki kipande kimojawapo atakuwa tayari kukitoa ilihali alishasema ziwa lote ni mali ya malawi?
ukitakujua huyu mama ni anatumia akili za ajabu, kila siku anatoa kauli tofauti na wana jf wanaziwekaga humu, mara yuko tayari kufa kwa ajili ya malawi hapa na maana gani, mara hotosimamisha uchunguzi kwa kuwa ziwa lote lake, mara leo atatumia diplomasia! kweli inakuingia akilini? ujue lazima kuna kutofautiana hapa, membe was simple, njia za kidiplomasia zinaendelea ivyo wenzetu wasitishe uchunguzi,sisi tukamsema membe ooh anawaita wale wenzetu, leo yule mama kasema sisi ni wenzao kama dada na kaka, ati tumenyamza hatujasema kitu! watu wa maswala ya usalama na ulinzi na walikuwa simple, tukotayari kwa vita kama njia ya diplomacia hatufikiwa, hawakuwa na kubadilisha adilisha maneno! kama hawatakubaliana kidiplomasia kwa mtazamo wangu kutakuwa janga hapo.