Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
WATANZANIA zaidi ya 800,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Malaria. Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesema katika takwimu rasmi kutoka katika vituo vya afya imebainisha kuwa malaria ni tishio kwa watanzania kutokana na wanaofika katika vituo hivyo wanasumbuliwa na ugonjwa huo.
Amesema katika tafiti nyingine imegundua kuwa asilimia 60 hadi 80 ya vifo hutokea nyumbani kabla ya wagonjwa kufikishwa katika vituo vya afya.
Amesema ugonjwa wa Malaria unaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudhuria katika vituo vyote vya afya na unaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa katika vituo hivyo.
Prof. Mwakyusa amesema katika vifo hivyo pia idadi kubwa zaidi vinatokana na watoto chini ya umri wa miaka mitano na wakina mama wajawazito.
Hivyo amesema Wizara ina mikakati ya kudhibiti yenye ufanisi mkubwa katika kudhibiti ugonjwa huo endapo itatumika kama ipasavyo.
Amesema mikakati hiyo ikiwemo ya kuangamiza mazalio kwa kusafisha mazingira kote nchini, vilevile na kutumika kwa vyandarua vyenye dawa maalumu ambavyo vinagaiwa katika zahanati kote nchini kwa akina mama wajawazito.