Malaria 150: wataalam hebu tuelewesheni hii kitu.

Kawaida vijidudu vya malaria (malaria parasite) huesabiwa ukilinganisha na idadi chembe nyeupe za damu(white blood cells),majibu tuliozoea idadi ya chembe nyeupe za damu huwa ni 200 kwa mfano mtu mwenye malaria 4 kawaida inamaanisha huyu mtu vijidudu vinne vilionekana katika chembe nyeupe za damu 200,sasa kama vijidudu 150 vimepatikana katika chembe nyeupe za damu 200 ni malaria kali sana lakini kama vijidudu hivyo 150 vimeonekana katika chembe nyeupe za damu nyingi zaidi kwa mfano katika chembe nyeupe za damu 50000 hiyo nikawaida si ya kushangaza,so inategemea hao malaria parasites walihesabiwa per how many white blood cells, thats ol i know

Thanks for sharing. I love JF
 
no D hujanielewa.niliandika kuwa usually malaria parasite (mp)huhesabiwa per 200 white blood cells (wbc's) so kama walihesabu wakapata 150mp/200wbc's ikimaanisha katika wbc's 200 wameona malaria parasite 150 that means ni malaria kali,kwa uelewa wangu mdogo najua hvo, cjui umenielewa mkuu!

Shukurani mkuu, lakini naona kama najilazimisha kuelewa, kidogo lakini.
 
..Dhana ya kuitazama malaria na idadi ya wadudu(parasite) ni potofu, na hii lugha ya malaria moja, mbili nk imepanda sana chati na ongezeko la utitiri wa maabara za binadamu ambazo (nyingi) uwezo/weledi wa wafanyakazi wake na vitendea kazi vyao ni questionable! Sambamba na hili pia ni ongezeko la hospitali binafsi (za kibiashara). Kifupi ni matokea ya biashara huria. Severity ya malaria haipimwi kwa idadi ya vidudu/parasites (kuna mchangiaji kaeleza) kinachoangaliwa ni parasites wameshambulia mwili kwa kiasi gani (mf. je ubongo , figo nk vimehusika? na hii huangaliwa kwa kum examine mgonjwa na kuangalia dalili zake. Kwa mfano mtoto mwenye malaria inayoambatana na degedege (Convulsion) husemwa kuwa na malaria kali (severe) na suala la parasite wangapi per WBcs halina umuhimu hapa. Pia Vipimo kama renal function test, Liver function test nk huweza kusaidia. Mfano mtu mwenye malaria na dalili za kuchanganyikiwa (altered mental state) huyu ana malaria kali hata kama ana malaria moja! (I hate this language, malaria moja!?$#**). Mwisho, severity ya malaria pamoja na mabo mengine inategeme sana previous exposure ya mtu kwa ugonjwa wa malaria; yaani, je ulishawahi kuugua kabla? Ndio maana, watoto wachanga chini ya miaka 5 ndio wanaokufa na malaria zaidi kwa malaria na pia watu wanaotoka nje ya malaria endemic areas(maeneo yenye ugonjwa) e.g. Europe, nk wakiugua malaria huwa severe zaidi. wanaojua zaidi wanaweza kuongezea......Nitarudi on this thread ueleza pia mama mjazito na malaria

Shukurani sana, rudi pesi.
 
Kwa hiyo wewe unatumia vipimo gani ku assess level of severity ya Malaria?
Easy....soma vizuri post yangu. Diagnosis ya malaria inafanywa kwa kwa Blodd smear Microscopy (BS) hapo unachofanya ni kutambua kuwa mtu ana vijidudu vya malaria. Hiyo ni kazi ya mtu wa maabara; daktari akipata majibu analinganisha na history aliyochukua kwa mgonjwa na examination aliyomfanyia. Fahamu kwamba, daktari mzuri anakuwa amefashafanikiwa kujua tatizo kwa 75% au zaidi kutokana na maelezo uliyompa hivyo lab results inacomplement 25% iliyobaki. Hivyo akipewa majibu ya malaria 1 huku yeye ame examine mgonjwa na history ameona mgonjwa ana upungufu wa damu(anemia), degedege (convulsion), nk diagnosis ni severe malaria sio malaria moja! Ndio maana nasema kumpa mtu majibu kwa kumueleza idadi ya parasite haina maana. Pia fahamu kwamba kwenye maeneo ambayo ni malaria endemic (ugonjwa wa malaria ni common sana-hii tafsiri sina uhakika nayo) kumkuta mtu na malaria 1,2 3 ni kawaida na haimaanishi huyu ni mgonjwa. I can assure you nenda sehemu kama bagamoyo pima watoto wa shule 100 malaria utashangaa kuwa wengi utawakuta na hiyo malaria 1,2,3 nk na wote wako fiti waacheza mpira
 
Jamani hapa ni swala la hesabu za ujazonene (density).....kwa comparison vijidudu 6 katika chembechembe say 2 (6/2=3) ni tatizo kubwa kuliko vijidudu 150 katika chembechembe za damu say 75 (150/75=2)....... Hapa ni mfano tu kwa sisi ambao sio Madr ila Engineers.
 
Huyo Dr. Riwa yupo likizo nini!!, Au hawajui Mbu!!
 
so hakuna malaria 1,2,3 etc ( hakuna malaria ya no) lol, hizo no ni wa wadudu, au mimi sielewi?
 
yaani kwa kila chembe hai nyeupe 200...kuna vijidudu wa Malaria 150. Kizimkazimkuu kaeleza vizuri sana. Watoto chini ya miaka mi5 huwa na hata vijidudu 5,000! 3,000,2,500 na hata 10,000!na wanatibiwa na kupona. Wengine huchelewa kwenda hospitali,wengine area atokayo Malaria wanasikia tu kwenye redio n.k.
 
so hakuna malaria 1,2,3 etc ( hakuna malaria ya no) lol, hizo no ni wa wadudu, au mimi sielewi?
Kitaalamu Malaria inagrediwa kama Severe Malaria ama Malaria[zamani complicated na non complicated]. Mambo ya no yamekuzwa tu na zahanati binafsi ili wawalaze watu vitanda vilipiwe biashara ifanyike!
 
.. Hivyo akipewa majibu ya malaria 1 huku yeye ame examine mgonjwa na history ... kumkuta mtu na malaria 1,2 3 ni kawaida ... hiyo malaria 1,2,3 nk na wote
Kwa hiyo kumbe hata wewe, pamoja na vipimo vingine, unatumia kipimo cha "malaria moja... malaria tatu...malaria mia hamsini" kutathmini ukali wa ugonjwa wa malaria katika majumuisho yako ya diagnosis ya ugonjwa, au?
 
tangu house girl wangu alivyokutwa na vidudu 2000 vya malaria dah, sishtuki tena nikisikia stori za nimekutwa na vidudu 2, 3 , 4 vya malaria. ila almanusra tumuage yule dada. alilazwa wiki 1 muhimbili!
 
tangu house girl wangu alivyokutwa na vidudu 2000 vya malaria dah, sishtuki tena nikisikia stori za nimekutwa na vidudu 2, 3 , 4 vya malaria. ila almanusra tumuage yule dada. alilazwa wiki 1 muhimbili!

2000!!!!!!!!!!!!!!! Acha masihara! Loh!
 
tangu house girl wangu alivyokutwa na vidudu 2000 vya malaria dah, sishtuki tena nikisikia stori za nimekutwa na vidudu 2, 3 , 4 vya malaria. ila almanusra tumuage yule dada. alilazwa wiki 1 muhimbili!

Ya kweli hayo mjomba!!.
 
Nakumbuka binamu yangu huwa ni bonge la mtu na mara kwa mara amekuwa akikutwa na vijidudu zaidi ya 30 vya malaria nikajua labda ni kutokana na kuwa mtumiaji wa vinywaji vikali hivyo kila akisikia malaria ndogo huipotezea kwa vinywaji vikali (pombe kali e.g whisky) na mmoja wa madaktari ktk hospitali flan aliwahi kuniambia kuwa kwa ukanda huu wa afrika ni nadra kumpima mtu ukakuta hana kabisa malaria kutokana na mazingira ila inatokana na historia ya huyo mgonjwa juu ya malaria hapo nilikuwa na kijidudu kimoja cha malaria na akaniambia kama huwa sisumbuliwi sana na malaria basi sio lazima kunywa dawa ila ninaweza tu kunywa maji mengi ya kutosha mara kwa mara na kujitahidi kufanya sana mazoezi na kweli ikawa imepotea kwa dizain hyo. Ila pia alinidokeza kuwa mtu aliye na malaria 2 au 3 anaweza kuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kuliko mtu aliye na wadudu 20 kupanda juu sasa hapa sikumwelewa maelezo yake na mpaka leo sijapata mtu wa kunielewesha vizuri ila thanks to KIZIMKAZIMKUU kwa maelezo yake yamekidhi majibu yangu kwa kiasi kikubwa.
 
Siku hizi kuna vipimo vya aina mbili. Cha kwanza ni kuwa angalia malaria parasites baada ya stainining kwenye microscop. Hii inatumika kujuwa kama kweli parasites wapo. Na pia kipimo hichi chaweza kutumika kujuwa ni aina gani wa parasites waliokuwepo. Wapo aina 4 tafauti. Kipimo cha pili ni serological. Yaani hupimwa damu kuangalia kama una antigens wa malaria. Hii sio conclusive kama unao wakati unapo pimwa kwani hata kama uliuguwa wiki iliyopita na ukameza dawa hizo antigens zaweza kuwepo kwenye damu. Ukiona Malaria 150 inamaanisha kuwa malaia antigens na sio parasites
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom