"Makuwadi wa Soko Huria" Hakikuzingatia Hali Halisi ya Ulimwengu wa sasa

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Napenda kutoa rai kwamba uandishi wa kitabu makuwadi wa soko huria cha marehemu professa Chachage hakikuzingatia uhalisia wa mambo yafuatayo:

1.Kwamba mfumo wa uchumi unaitawala dunia leo hii ni ubepari.
2.Kwamba utandawazi huja na out-build chances na si in-build (mara nyingi).
(You fit urself to the world instead of the world fitting itself to you).
3.Historia ya ubepari duniani,kutawanyika kwake na malengo yake pamoja na nguvu ya sura tofauti zitumikazo kuuendeleza.
4.Nguvu halisi ya nchi kama Tanzania na nafasi yake katika ushiriki wa uchumi wa dunia.(vipi hasa ni sahihi kufanya katika muda husika).

Kwa mliokisoma naomba mnipe mtazamo wenu katika hili na mustakabali wetu kama taifa.
 
Kuna tofauti kati ya riwaya na insha. Riwaya ni kazi ya sanaa zaidi. Huwa inasadifu ama kuakisi jamii - pia inaweza kutumika kama kebehi kuhusu mfumo fulani. Na mwandishi mzuri sio lazima aoneshe kitu waziwazi kama kwenye insha.

Hivyo nakushauri usome mahojiano haya ya mwandishi wa riwaya hiyo utapata majibu ya maswali yako kuhusu ubepari/ubeberu duniani: http://www.ifeas.uni-mainz.de/SwaFo/SF11Diegner_MahojianoChachage.pdf
 
Haya ungeyaongea alipo kuwa hai.
Angekupa majibu maridhawa ya kukuridhisha
napenda kutoa rai kwamba uandishi wa kitabu makuwadi wa soko huria cha marehemu professa chachage hakikuzingatia uhalisia wa mambo yafuatayo:

1.kwamba mfumo wa uchumi unaitawala dunia leo hii ni ubepari.
2.kwamba utandawazi huja na out-build chances na si in-build (mara nyingi).
(you fit urself to the world instead of the world fitting itself to you).
3.historia ya ubepari duniani,kutawanyika kwake na malengo yake pamoja na nguvu ya sura tofauti zitumikazo kuuendeleza.
4.nguvu halisi ya nchi kama tanzania na nafasi yake katika ushiriki wa uchumi wa dunia.(vipi hasa ni sahihi kufanya katika muda husika).

kwa mliokisoma naomba mnipe mtazamo wenu katika hili na mustakabali wetu kama taifa.
 
[QUOTE=Kiranja Mkuu;1067773]Haya ungeyaongea alipo kuwa hai. Angekupa majibu maridhawa ya kukuridhisha[/QUOTE]

Ni kweli ila kuna majibu mengi tu kwenye huo mtandao niliowekea hapo juu - kwa mfano, humo kuna dondoo hii:

Riwaya yako inaweza kusomwa kama handbook ya ukosoaji wa utandawazi unaotawaliwa na siasa ya soko huria. Hivi juzi [mwanzoni mwa mwaka 2004] Rais Mkapa kama mwenyekiti wa Tume ya Utandawazi alitoa ripoti – kwa Kiingereza – inayowataka Watanzania wazingatie upya manufaa ya utandawazi. Unaonaje hoja hii ya Rais?

Mimi nimekuwa natofautiana sana na watu wengi katika suala hili la utandawazi kwa ujumla. Mimi kwa maoni yangu, huu unaoitwa utandawazi ni kitu ambacho kilikuwepo siku zote. Globalization ni kitu ambacho kilikuwepo siku zote isipokuwa ni kitu ambacho wanataka kukigeuza kitu ambacho ni kibaya kiwe kizuri. Ubeberu na ukoloni mamboleo ndio utandawazi. Hakuna tofauti yoyote ile. Kwa hiyo sijaona kwamba utandawazi una manufaa.

Mimi kama naamini kwamba kuna kitu kama utandawazi, ni kitu ambacho kinaitwa globalization from below. For example, human rights ni global movement, women's rights ni global movement – that's the real globalization. Environmental protection – that's the real globalization. Lakini other globalization ambayo ni movement ya capital, na communication or whatever – these things zimekuwepo siku zote, you know?

Lakini
we can talk about human rights kwamba ni phenomenon ambayo imeanza miaka ya 1945, au peace movement ni ya miaka sitini na sabini. Lakini hiyo ya capital kutoka wakati wa ukoloni, na hiyo ya watu kutoka wakati walipochukua slaves mwaka 1441, akina Goncalves – ni kitu hicho hicho. Kwa hiyo utandawazi ni unyonyaji. Ni ubeberu.

Kitu kimoja cha kujiangalia zaidi ni impact, kwamba kuna madhara. [Rais] Alikubali kwamba kuna madhara, ingawa anasema tunaweza ku-accomodate, na tunaweza kuishi nao kwa kukaribisha vitu fulani. Kwa hiyo miye ninachopinga ni madhara ya utandawazi.
 
Nashukuru kaka.Good way of thinking.
 
ndugu yangu unanisikitisha kwa kusema hakikuzingatia hali halisi ya sasa, unachomaanisha ni kwamba hata kama tuko pabaya inabidi tuvumilie tu kwani hatuna jinsi, ur very wrong, extent ya kubanwa na soko huria inaonekana bado kwa waafrica sio kubwa, angalia wenzetu wa amerika ya kusini waliouanza mfumo uu toka 30's.
Leo ndio wamethibitihsa kua sio lazima tufiwe wote uko kama venezuela, bolivia nk zinageuka, kuna mifano wanaiona ya failed state kama haiti ambazo kwa sasa no way out kwani haman resources wala chanzo cha uchumi hadi wendawazim kama kina wyclef jean wanataka kua ma rais! baada ya amerika kusini zitafuatia za south east asia kwani sasa umasikini unatisha kama bangladesh, nepal, sri lanka etc then na sisi africa tutafuatia.

Angalia jirani zetu wa kenya walianza baada ya uhuru lakini sasa wanatafuta breathing space walivyodesperate na east africa federation! zimbabwe nao waliona hali halisi ni chungu wakabidilika na sasa ukiacha negative publicity zote walizopata wameanza kustabilize na wanaerekea ktk right direction!
 
For the 1st time here is a man hailing Hugo Chavez na kusema he's right!!So u agree now to live the South American's style democracy has to stay aside for a while?
 
Napenda kutoa rai kwamba uandishi wa kitabu makuwadi wa soko huria cha marehemu professa Chachage hakikuzingatia uhalisia wa mambo yafuatayo:

1.Kwamba mfumo wa uchumi unaitawala dunia leo hii ni ubepari.
2.Kwamba utandawazi huja na out-build chances na si in-build (mara nyingi).
(You fit urself to the world instead of the world fitting itself to you).
3.Historia ya ubepari duniani,kutawanyika kwake na malengo yake pamoja na nguvu ya sura tofauti zitumikazo kuuendeleza.
4.Nguvu halisi ya nchi kama Tanzania na nafasi yake katika ushiriki wa uchumi wa dunia.(vipi hasa ni sahihi kufanya katika muda husika).

Kwa mliokisoma naomba mnipe mtazamo wenu katika hili na mustakabali wetu kama taifa.

Ukishaita riwaya huna haja ya kuhoji uhalisia. Maswali yako yanakaa kama unafanya utafiti vile, kila la kheri
 
Back
Top Bottom