KOMBAJR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 5,827
- 1,271
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi-CDM John Mnyika amesema hana mpango wa kugombea urais hivi karibuni wala katika kipindi cha miaka kumi ijayo na zaidi.Amesema Urais kamwe si kipaumbele chake.
Akihojiwa wiki iliyopita Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo alisema kwa sasa anayo majukumu makubwa mawili ambayo ameyaweka kama kipaumbele chake.
Mnyika amesema kipaumbele cha kwanza ni kukitumikia chama chake cha CDM kwa moyo mmoja na kuwaunganisha wanachama wote ili kujiandaa kuchukua dola 2015.
Mnyika amesema kipaumbele cha pili ni kuwatumikia wananchi wa ubungo kwa uwezo wake wote.Alisema wananchi wa Ubungo walimuamini yeye na chama chake na kamwe hatawaangusha.
Nina wasiwasi na hawa waandishi ambao kila kukicha maswali yao Je utagombea urais?mnaidhalilisha tasnia yenu.
Pamoja sana kamanda mnyika