Makutano Show: Exclusive Interview na Mhe. John Mnyika - Oct 06, 2012

M4C itaendelea muda si mrefu baada ya ratiba mpya kutolewa.

Mnyika pia anasema inawezekana uchaguzi mkuu ujao katiba mpya ikawa bado. Analalamikua sheria ya mabadiliko ya Katiba kwamba haina dhamira ya kupatikana katiba ya wananchi.
 
Anasema matumaini ya kutumia katiba mpya kwenye uchaguzi ujao ni madogo sana..
 
Anatoa historia ya M4C, mafanikio yake mpaka sasa. Ni sehemu ya mpango mkakati wa chama tangu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2005, ambapo mojawapo ya maagizo ilikuwa ni kufanya operesheni maalum nchi nzima. Ilianza kwa mkakati wa kupata VIJANA kwa kutumia Y4C, Youth for Change.
 
Mnyika anamwaga pointi tupu.

Nimeamini CDM noma na Mnyika ni kichwa. Kila anachozungumza reference yake ni CDM na kamwe si sifa binafsi. Anaelezea historia ya katiba mpya kwamba ni pale wabunge wa CDM walipotoka nje ya bunge Rais alipohutubia kuzindua bunge.
 
Anazungumzia suala la Zitto kutangaza kugombea urais..anasema vikao bado avijakaa kuteua mtu..chama akijaanza mchakato na ni mapema sana..
 
Mgombea Urais CDM-Mnyika anasema wazi muda wa kugombea urais bado.Hamungunyi maneno anasema katiba inaweka wazi kwamba masuala ya kupitisha mgombea yanaanza kwenye Kamati Kuu na kuendelea baada ya hapo.Anasema kutamka kugombea kwa mtu yeyote si tatizo lakini alimradi utamaduni na maadili ya chama yalindwe.
Mnyika ni Jembeeeeeeeeeeeeeeeeee...!
 
Naona Fina amejaribu kumbana kuhusu Zitto na urais,amekuwa mjanja kukwepa kuleta labsha.
 
Anasema CDM haijawahi kusababisha mauaji na wala CDM haisababishi nchi isitawalike.Anawataka watawala waheshimu sheria na haki za binadamu.
 
CDM haijawahi kupokea fedha kutoka mashirika ya kidini.Mnyika anatiririka pointi tupu.Amesema kamwe propaganda nyepesi haiwatishi CDM.
 
Swali la kwanza kwa mh Mnyika,

Karibuni zimetokea tetesi kuwa chama chako kinapata misaada ya moja kwa moja toka mashirika na vyama vya kidini kama Jesuit na CDU, Je uko tayari kutuelezea ni misaada ipi na ina dhamira gani?

Swali la pili,

Siku za nyuma kwa nyakati tofauti viongozi wa CHADEMA waliwahi kutoa kauli kuwa nchi haitatawalika na sasa hivi tunashuhudia vurugu na mauaji sambamba na maandamano. Je, hii ni njia mojawapo ya kuhidhoofisha serikali iliyopo madarakani na nini hatima yake? Toa ufafanuzi...

Ni hayo tu

swali lako analijibu sasa ivi,tena kwa ufasaha mkubwa...anasema kushindwa kwa dola kufikia matalajio watanzania ndio kunachofanya nchi isitawalike.

Anakanusha Chadema kupokea fedha kutoka Cdu..ata Cuf inapokea fedha kutoka FNF chama kinachounga mkono ushoga,anasema kama kupokea msaada ndio kuunga mkono mlengo wa chama,je CUF inaunga mkono ushoga!?
 
Ruzuku ya CDM kwa mwezi ni milioni 203 lakini mahitaji yake kwa mwezi ni zaidi ya milioni 500,hapa inabidi wananchi wachangie wenyewe chama chao.
 
Anasema anayedhani kuna mgogoro utakaoua CDM anaota ndoto za mchana.Amesema CDM inazo kamati maalum za kutatua migogoro.
 
Mnyika mbona uongelei mradi wa mabasi yaendayo kasi wakati unafika mpaka jimboni kwako au hakuhusu.
 
Kipindi kinashika kasi, John is really driving the show with a good control of Fina. Sasa anafafanua swali kutoka kwa mpiga kura wake juu ya matatizo ya usafiri.
 
SWALI LANGU NI MOJA LAKINI LINA VIPENGELE A na B

A: Tumekuwa tukiingia milango ya ubungo terminal kwa sh 200 mbaya zaidi unaingia kwa mguu wako yani hakuna chombo cha kukubeba uingie ndani...lakini tulikusikia mh mnyika ukipaza sauti wewe na wabunge wenzako baadhi wa Dar kuhoji swala la kupanda kwa nauli ya kivuko cha kwenda kigamboni kutoka tshs 100 mpaka 200, swali langu je hao wanaoishi huko kivukoni wana tofauti gani na sie wapiga kura wako ambao umekaa kimya tangu uingie bungeni? Ina maana kero zawana kigamboni zinakugusa kuliko zetu wapiga kura wako? Kama jibu ni hapana, sasa je, utatusaidiaje wana ubungo tuingie na sisi pale terminal ubungo kwa sh 100? Tena sisi wala hatutaki kubebwa tutaingia kwa miguu yetu wenyewe acha wa kigamboni wabebwe

B: Swali la nyongeza, ni kwanini Kwa mfano, wakazi wa Kiluvya walioko katika Jimbo la Ubungo wanalipa nauli Sh. 900 kutoka Kiluvya hadi Ubungo wakati wakazi wa Mbagala wanalipa Sh 450 kutoka Mbagala hadi Mwenge. Je, wewe Mh. Mnyika kama mbunge wetu wa jimbo letu hili la Ubungo, ulipata wapi ujasiri wa kwenda kuwatetea wakazi wa Kigamboni wanaolipa Sh. 200 badala ya sisi wapiga kura wako tuliokutuma ukatuwakilishe bungeni ambao hulipa Sh 1,200 kutoka Kiluvya hadi Posta. Je, huoni kama umetutelekeza baada ya kupata ulichotaka (ubunge)?

anajibu maswali yako sasa ivi,kwa ufasaha sana.

La kiluvya:anasema kiluvya zipo mbili so ruti zinaesabika kama zinaenda Kibaha,anasema ameshalifikisha Sumatra na wanalifanyia kazi ivi sasa ili kufanya marekebisho.

La stend ya Ubungo:kwanza nauli ameikuta lakini amefanya jitihada kubwa sana,kwa mfano ilikuwa kiingilio kiongezwe hadi sh 300 lakini alipigana hadi ikabaki ile ile sh 200..anasema ata ivyo kituo hicho akitakuwepo tena maana kitabadilishwa na kuwa ni kituo cha mabasi ya kwenda kasi na kituo cha mabasi ya mikoani kitaamishiwa Mbezi kwa yusuf.
 
John is posing a very serious question; ameuliza unaweza kutaja tatizo hata moja Tanzania ambalo halina uhusiano na ufisadi? Anasisitiza umuhimu wa kushughulikia tatizo hili kwelikweli, anasisitiza uwajibikaji aw viongozi kwa wananchi.
 
Mnyika jamani ni Jembe; Huyu ni kijana shujaa ndani ya Chama! Huyu ni Role model wa vijana kote nchini, Hili ni Jembe likilopikwa kweli kweli na Dr Slaa na Kamanda Mbowe.

Anatiririka sasa kuhusu CDM inavyopambana na ufisadi nchini; Anashangaa jinsi CCM inavyokumbatia ufisadi. Anaelezea jinsi CDM ilivyoweka ilani yake ya uchaguzi uliopita .Anamsifu Mwl Nyerere alivyopambana na maovu.
 
Back
Top Bottom