Makutano Show: Exclusive Interview na Mhe. John Mnyika - Oct 06, 2012

Namuuliza swali lifuatalo:

M4C inataaza lini baada ya kusimama kutokana na mauaji ya Mwangosi?

Ushauri wangu, mkae na Waziri wa ulinzi, na Said Mwema mkubaliane nao jinsi ya kuendesha M4C ili isitokee kutokuelewana na ma RPC wanaotumiwa kuzuia mikutano, muhimu ni kuwa huu ndio muda mzuri saana wa kuvuna wanachama wengi kutokana na makovu ya uchaguzi wa CCM.

Nawasilisha Mheshimiwa Mnyika
 
Naomba kumuuliza Mh. Mnyika swali Hili:

Barabara ya Morogoro inakabiliwa na msongamano mkubwa sana ambao hautaisha hata baada ya kukamilishwa ujenzi unaofanika hivi sasa. Kinachosababisha hilo ni Malori Mengi ya mafuta na mizigo kwenda ndani na nje ya nchi yanayolazimika kupitia Ubungo wakati wa kwenda na kutoka safari.

Je kuna mikakati gani ya kuchepusha magari haya, mfano kupitia Barabara ya Malamba mawili kutokea Kinyerezi badala ya kupitia Ubungo?

Ahsante
 
Maswali kwa Mnyika,,

1. Open space za Sinza zimechukuliwa na mafisadi, yeye kama mbunge amechukua hatua gani?

2. Sinza ni eneo la makazi ya watu, lakini kuna wimbi la kujenga maghorofa bila kufuata kanuni za ujenzi, Guest house na logde, bar zinajengwa kwenye makazi watu, tusipokuwa makini sinza itakuwa kama kariakoo
 
Lakini we fina na wenzako mnatusumbuaga tunajipinda kutafuta maswali jamaa wakija hapo hamuwagongi maswali yetu,kuweni kama waandishi wa marekani,urafiki pembeni

kama ulikuwepo,nilimsikiliza akimuhoji January ni kama anachagua maswali yatakayo mfurahisha.
 
Swali kwa JJ Mnyika:

Kuna tetesi kuwa ulikuwa na nia ya dhati kuomba uondolewe au upunguziwe vyeo na majukumu ya kichama ili upate muda wa kutumikia Wananchi kwa ufanisi zaidi. Inadaiwa azma yako hii imepingwa sana na imekwamishwa na rafiki zako wa karibu; watu uliotoka nao mbali katika maisha na harakati. Hawataki upunguze vyeo ili waweze kukutumia kama ngazi katika teuzi za ndani ya chama hasa kwenye Ubunge wa 2015. Ukizingatia kuwa miongoni mwa hawa wanapanga kugombea majimbo ambayo tayari ama yana wabunge wa upinzani/CDM au qualified potential candidates from CDM, Je, umejiandaa vipi kukabiliana na changamoto ya matarajio ya rafiki zako dhidi ya michakato ndani ya chama?

Swali la Pili:
CDM ni Taasisi inayoongoza kwa kupewa ushauri makini bure toka kwa wataalamu waliobobea hasa vijana. Lakini hivi karibuni kasi ya CDM kupokea, kuthibitisha kupokea, kufanyia kazi ushauri na kisha kushukuru ni kama imezimika. Na Kurugenzi pamoja na chama kwa ujumla ni kama hakihitaji wala kuthamini tena ushauri makini. Je, wewe kama Mkurugenzi husika unatambua hali hii? Na Je, una mipango gani kuhakikisha ukaribu na jamii ya watoa maoni makini yenye nia njema na CDM unarejea?
 
Swali langu kwa JJ Mnyika yeye kama mkutugenzi wa habari wa chadema kwanini CHEDEMA imeshindwa kutimiza ahadi yake mpaka sasa ya kuanzisha chombo chake huru cha habari ?

Mfano redio, gazeti hata TV station yake? (DR slaa aliahidi kwenye mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu Iringa mwaka juzi)
 
Swali langu ni kwamba:

Mheshimiwa Mnyika mara nyingi nikisikiliza bunge linazungumzia mambo ya msingi sana hasa umaskini wa nchi yetu, punguzo la bidhaa limesemwa sana lakini serikali bado halijali.

Je, ukirudi bungeni utalizungumzia vipi suala hilo la uzembe na uropokaji wa serikali bila utekelezaji?
 
Fina naomba umuulize swali Mh mnyika kuhusu mabilioni yaliyo semekana kufichwa nje huko uswis chama kina msimamo gani kwenye hilo?
 
John anafafanua namna ambavyo Jeshi la Polisi limeamua kuanzisha 'mradi' kuua raia wasiokuwa na hatia. Walianza kwa kuua watu kwenye matukio mbalimbali, sasa wameanza kuua kwenye matukio ya siasa, ambayo hasa yanayohusisha shughuli za CHADEMA. Kwa hiyo hiki kitu si bahati mbaya. Imeanza muda mrefu.
 
John anasema: Rais Kikwete alitoa OK kwa vitendo wanavyofanya polisi kwa sasa, kuua raia wasiokuwa na hatia, hasa katika hotuba yake ya mwanzo kabisa baada ya uchaguzi mkuu 2010.
 
Jembe langu Mnyika.Anatiririka hapa nampata Live.Anaijenga CDM na kamwe hajisifu.Hawa ndiyo vichwa wa CDM....
 
Mnyika anasema CDM iliibiwa kura za urais na kura nyingi za wabunge zilichakachuliwa
 
Back
Top Bottom