Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
hapo kwenye red kama uliandika wewe basi utakuwa na matatizo makubwa ya kifikra.Hilo kundi la kilimanjaro unalosema umeweka wajumbe wa nchi nzima kama supporters.Kuthibitisha jinsi mlivyo wagumu kuelewa.Wewe mpaka uahdithiwe kuhusu CDM wakati kila siku wansemwa na wao wanajieleza.Hizi habari za kuambiwa na akina Mukama ni ishara kuwa wewe ni mbea siku siku zote.chadema kina makundi makubwa matatu huku la kwanza likiundwa na idadi ya viongozi wanaotoka mkoani kilimanjaro na kuongozwa na mbowe, la pili lina watu kutoka manyara na arusha kiongozi wake ni dr. slaa, halafu la tatu linamuunga mkono zitto.
tofauti ya mawili ya kwanza, kundi hili la mwisho lina watu wanaotoka nje ya mikoa hiyo ya kilimanjaro, arusha na manyara, lakini jitihada zake huenda zisifanikiwe kwa kiwango kikubwa kutokana na sababu za maslahi zaidi.
zitto binafsi anafahamu kuwa yeye, mbowe na slaa kila mmoja anapambana kikamilifu ili kuhangaikia uteuzi wa kugombea uraisi katika uchaguzi mkuu ujao, lakini anaelewa ni jinsi gani inabidi apambane na ubanguzi mkubwa wa ukabila na ukanda.
anajua kuwa viongozi wenzake wanaotoka kilimanjaro wanafanya kila wanavyoweza ili mbowe ndiye aje kugombea urais mwaka 2015, kazi inayofanywa kwa kutumia ushawishi wa kisiasa na kifedha. anafahamu kuwa kamati kuu ya chadema imerudikwa na watu wanaotoka kilimanjaro ili wawe na nguvu, wale ambao kuna wengine ni wafanyabiashara wakubwa wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hichi katika mkoa huo, philemon ndesasamburo. viongozi wengine wanaotoka kilimanjaro ni pamoja mbowe, mkurugenzi wa habari na uenezi john mnyika, mbunge wa kawe halima mdee, mbunge wa ilemela hayness kiwia, mkurungenzi wa fedha na utawala anthony komu na mkurugenzi wa bunge na halmashauri john mrema
Kundi hilo pia linasaidiwa na wabunge kama akina peter msingwa [iringa mjini] ezekieli wenje [nyamagana] joseph mbilinyi [mbeya mjini] joshua nasari [ arumeru mashariki] vincent nyerere [ musoma mijini] saidi arfi [mpanda mjini] mbunge wa zamani wa arusha mijini godbless lema.
Tofauti na hilo, kundi la dr. slaa linaudwa na kikundi cha wabunge wachache wa majimbo na baadhi wa viti maalum hususani wanaotokea mikoa miwili ya arusha na manyara, lakini kutokanana mzozo wa ndoa yao mkewe ambaye ni mbunge wa viti maalum, rose kamili hajihusishi nalo. aidha kundi hili pia halina nguvu za kifedha na hata ushawishi wowote mahali popote kwasababu ukimwondoa dr. slaa hakuna mtu mwingine yeyote mwenye nguvu kwa namna moja ama nyingine kisiasa.
Kundi la zitto ndilo halina idadi kubwa ya wabunge isipokuwa wachache tu ambao ukimwondoa yeye mwenyewe baadhi ya waliomo ni mkurungezi wa uchaguzi, msafiri mtemelwa pamoja na wabunge wa viti maalum wanatoka naye mkoa wa kigoma, muhonga saidi na philipa mturano. pamoja na juhudi anazofanya za kutaka augwe mkono na vijana mikoa yote nchini, tatizo kubwa linalokuja ni ukweli kwamba hata iweje hatateuliwa kuwa mgombea urais wa chadema katika uchanguzi huo mkuu wa mwaka 2015. hawawezi kuipata nafasi hiyo ya kwasababu hana wafuasi wengi ndani ya kamati kuu ambacho ndicho kikao kizito kuliko vyote na pia hatakiwi kwa namna zote na mwasisi wa chadema, mzee mtei. ni yeye aliyemzuia zitto kugombea nafasi ya mwenyekiti wa taifa mwaka 2009 akisema hawezi kuruhusu chama chake kichukuliwe na mtu asiyemfahamu "wapi anakotoka"
katika hali hiyo, nafasi ya kugombea uraisi mwaka 2015 ipo wazi zaidi kwa mbowe na siyo dr. slaa, zitto wala mwingine yeyote yeyote kutokana na uwepo wa makundi hayo matatu ingawa huenda yakaongezeka hapo baadaye. katika uchaguzi wa 2010 dr. slaa alishinikizwa kugombea uraisi kwa sababu tu kundi hilo lilijua kamwe hawezi kupata ushindi, na pili lilitazama mazingira ya matatizo yaliyokuwepo ndani ya ccm na kugundua kuwa angesaidia kupata wabunge, jambo ambalo lingemwekea mazingira mazuri mbowe ya kugombea urais mwaka 2015
SOURCE: gazeti la sauti huru
Kinaniuma san akuona CCM inapenda ishi na ujinga kiasi hiki, wananchi wa kawaida tuu wanaijua CDM vizuri kuliko uongozi mzima wa CCM.Wao kila siku huja na habari ambzo hata raia wa kawaida naweza sema ni uongo.CCM wapo so dettached with the society kiasi cha kufanya raia ndio wawaletee ccm maendeleo.