Makundi CCM yamzonga Kikwete

Am still in disbelief about this kauli

JKMJM.jpg


IMG_2525.JPG


h1.jpg

Hapa picha ya chini ni kama anamwambia " kwisha habari yako wewe". Jamaa ana kisasi kama nyoka.
 
Kama Mwenyekiti wa chama tawala ametambua kuwa chama chake kinaendesha chaguzi zake kwa njia ya Rushwa nini hatima yake?
Je ni ujumbe gani anautoa kwa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa Takukuru??Je Mkurugenzi wake ananini chakuwambia wananchi ambao Rais wao alimwamini nakumkabidhi madaraka lakini ameshindwa kuchukua hatua kwenye chama mpaka mkuu wa chama anagundua kuwa rushwa inatumika hadharani bila ya kificho huku watanzania tukiendelea kuwalipa mishahara watumishi wa Taasisi hiyo??
Je hapo CCM ina lakujitetea?
 
Takukuru, kama wana chembe ya nia ya kupambana na rushwa, wamwite raisi wamhoji, awape ushahidi wake juu ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwenye chaguzi za CCM...
 
Ni kweli jk amechemsha lakini hilo hilinishangazi hata kidogo kwani hakuna wisdom ndani take. Ndio maana sikubaliani na sentensi yako ya mwisho. Sio raisi wangu.

Asante mkuu,

Tatizo ni mfumo wetu, mimi ni mtanzania, nikiulizwa Rais wa nchi yako ni nami utajibu ni nani?
Mioyo mwetu tunaweza kuwa na majibu tofauti.
 
Jamani huyo ni dhaifu tu,yaani mi hadi ninaona aibu akiongea eti prezida ninatamani angejikalia tu kimya km ambavyo huwa hasemi kitu kwenye mambo ya msingi ya taifa letu,hata huko kwenye pumba zao angekuwa anajikalia kimya tu!..
 
Usanii mtupu na ni propaganda za kisiasa. Rusha ndani ya CCM ni ya siku nyingi Kumbuka ilivyo halalisha kwa kuita takrima.
 
Magazeti yameongeza chumvi hata katika nukuu ya direct speech iliyowekewa alama za kunukuu "" ?

Kama Kikwete hajasema hayo maneno Ikulu inangoja nini kufanya kazi yake ya kila siku ya kukanusha?
 
“Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu,” alisisitiza.

Kweli CCM inaye mwenyekiti kauli hii ya kumtaja mtu na tukichukulia Matatizo aliyopata Mwandosya na tukiangalia visasi ndani ya CCM napata ufahamu sasa kwa nini Mwandosya aliugua.

Kauli ya Mheshimiwa JK inashangaza sana. Aliyoanzisha makundi na rushwa ni yeye na bado makundi yake yanaendelea hata bada ya miaka nane ya utawala. Mwandosya alimfanyia kitu gani kibaya?? Baada ya 2005 Mwandosya hakua na makundi wala kinyongo, aliendelea kutumikia nchi yake na kumpigia debe Mheshimiwa Rais.Hata asingepewa uwaziri angetafuta njia nyingine yakutumikia nchi yake anayoipenda. Kama ni kweli alitamka hivyo arekebishe kauli hiyo.
 
Kwa mwenye video clip yake atuwekee, manake mapozi ya Rais wetu ni mengi, isijekuwa kuna commas, full stops na pauses zimepotea au kutowekwa pahali pake.

Manake kwa hali ya kawaida, hii nukuu imhusuyo Prof. Mwandosya haionekani kutolewa na Rais anaetafuta kuvunja makundi wala kuheshimu wenziwe
 
“Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu,” alisisitiza.

kauli hii ina maana MWANDOSYA alimfanyia vitu visivyovumilika ndio maana prof. iko gonjwa dots connected
 
"Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu," alisisitiza.

Kama kweli Rais wa Nchi ametamka maneno haya ni hatari sana. Hivi haya maneno yaliandaliwa yatamkwe na Rais au ameropoka tu. Kitendo cha kumsingizia Prof. Mark Mwandosya vitu ambavyo hakuvitenda ni aibu kubwa kwa rais wa nchi.

Niliwahi sema hapo nyuma kuwa Kikwete na Serikali yake inamuhitaji Prof. Mark Mwandosya kuliko yeye anavyomuhitaji Kikwete.Prof. Mwandosya ni mtu makini sana, najua hatajibu lolote kuhusu kauli hii mbaya yenye aina ya mipasho ya taarabu.

Kikwete pamoja na Urais wake hawezi kusimama na kujinasibu mbele ya Prof. Mwandosya.Kwa kauli kama hizi ukimwambia mtu ana degree ya Chupi utakuwa umemtukana?

Prof. Mwandosya naomba usijibu lolote, Watanzania wanakufahamu ulivyo na ndio maana wengi wanashangaa humu JF.


Prof. Mark Mwandosya for President - 2015
 
MAKUNDI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), yanaonekana kumwelemea Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na sasa ameamua kutumia mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), kukemea vitendo vya kudhalilishana na makundi wakati na baada ya uchaguzi.

Rais Kikwete pia alionya juu ya vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri ndani ya chama hicho akisema kuwa visipochukuliwa hatua mapema, kuna hatari ya kukifikisha chama katika hatua mbaya.

Akifunga mkutano huo wa nane wa uchaguzi UWT, Rais aliwataka kufanya jitihada za kupunguza mgawanyiko uliotokea baada ya uchaguzi wao uliomalizika juzi.

Alisema imekuwa ni hulka sasa hasa baada ya kumalizika uchaguzi kwa wanachama kuendeleza na kuwekeana uhasama kama uliokuwepo wakati wa kampeni na wengine kuwaadhibu ambao hawakuwachagua hali ambayo ni mbaya sana kwa mustakabali wa chama.

“Ambaye hakukuchagua usimbague kwani hakushinda na sasa wewe ndiye kiongozi, hivyo una kila sababu ya kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuitumikia jumuiya yake kwa ukamilifu.

“Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu,” alisisitiza.

Rais Kikwete aliwaasa wagombea wa nafasi mbalimbali wa UWT walioshindwa kutoweka visasi na walioshinda kutowapiga vijembe walioshindwa kwani kazi iliyo mbele ni kubwa kutokana na CCM hivi sasa kukabiliwa na hali ngumu ya ushindani wa kisiasa.

“
Kweli tusipokemea vitendo hivi na kuviacha vikiendelea, tutakipeleka chama mahali pabaya, ninasikitika sana kusikia hata wanawake sasa wanajihusisha na utoaji rushwa ili kununua nafasi za uongozi kitu ambacho ni hatari sana,” alisema Kikwete.

Alifafanua kuwa chama kinakoelekea si kuzuri ni lazima zifanyike jitihada za mabadiliko.


Aliwapongeza wajumbe kwa kukamilisha uchaguzi wa viongozi watakaoongoza jumuia hiyo kwa muda wa miaka mitano na hata waliojitokeza kugombea kwani kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi.

Rais Kikwete aliongeza kuwa madhumuni ya CCM yaliyotamkwa katika katiba ni kushinda katika uchaguzi wa serikali kuu na mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda serikali kuu na serikali za mitaa.

Alisema ushindi wa CCM unapatikana kwa kukubaliwa na kuungwa mkono na wananchi wengi zaidi watakaojitokeza kupiga kura, hivyo kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa na jumuiya za chama zilizoundwa ni kufanikisha hilo.

Kikwete alifafanua kuwa demokrasia ya uchaguzi ina athari zake kwani baada ya hapo kuna kazi kubwa ya kujenga umoja na mshikamano ili kuziba nyufa na mipasuko iliyotokea wakati wa uchaguzi.

Alisema kuwa huwezi kumchukia mwenzako kwa vile ameomba nafasi unayoitaka wewe, kwamba nafasi hiyo ni haki ya kila mwanachama, hivyo hakuna haja ya kuchukiana.

Rais Kikwete alifafanua kuwa uchaguzi una mifarakano mingi lakini kiongozi akishapatikana ni lazima aungwe mkono na kwamba wenye kuonyesha mfano ni wale walioshinda kwa kutowabeza walioshindwa.

Awali, Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba, alisema kuwa wamefanya mengi ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na wamejipanga kuhakikisha wanaleta ushindi katika uchaguzi mkuu wa 2015.


Source: Tanzania Daima

:bowl::bowl:CHEKI VIZURI HAPO KWENYE NYEKUNDU; kwani rushwa kwa wanaume kama alivyofanya yeye 2005 ni halali na halamu kwa wanawake? JK anatakiwa kukumbuka kuwa alivyo baba ndivyo walivyo watoto. arafu eti chama kinakoelekea c kuzuri lazima zifanyike jitihada za mabaliko. je n jitihada gani hizo na nan wa kuzichukua? na si kweli kuwa chama kinaelekea pabaya ila chama(CCM) KIMESHAFIKA PABAYA TAYARI KILICHOBAKI NI KUPSHA WENGINE, TIME IS OVER!
 
Kwa wale wanaoelewa zaidi, Je, hapo kuhusu Prof. Mwandosya alikuwa na maana gani? Kwamba kambi ya Mwandosya ilihusika katika mambo ya ajabu aliyotendewa?

ndo manake...akina mwandosya walitaka kumpiga chini asigombee urais ndo maana mwandosya akafanyiziwa, inaelekea 2010 kuna watu ndani ya ccm walitaka kumpiga chini JK asigombee tena....

Which is fair..sio lazima mtu ugombee mihula miwili...muhula mmoja unatosha rais kua madarakani miaka 10 ndio inaleta uzembe serikalini
 
Kikwete ana matatizo...Sijui ni mvivu wa kufikiri? Kila akifungua mdomo wake anakuja na jipya.Maneno aliyoyasema kwenye Mkutano wa UWT - CCM yatammaliza.Hakukuwa na sababu hata kidogo ya kusema mambo haya hadharani,ni sawa na kutonesha kidonda!
 
Back
Top Bottom