Makundi CCM yamzonga Kikwete

Hata mimi sijamuelewa Kikwete, awe makini na anachokiongea yeye ni rais wa nchi. Kwa hiyo uwaziri amempa kinafiki tuu?
 
Jana nimeona mama Sophia Simba na Kasheshe lake na Shyrose mama anaongea utadhani anaimba Taarabu
Kweli ndani ya hiki chama kuna mmomonyoko wa maadili na wao kwa wao ni maadui
Iko Kazi
 
Ukishafika ulipopahitaji ni kawaida kusahau njia uliyopitia kufika ulipo, nadhani mambo aliyofanyiwa Dr Salim 2005 ndio mabaya sana lkn walionufaika ndio wanalalamika, kama Kigoda, Salim na Sumaye wangekuwa inclusive kwenye serikali kidogo ningemuelewa.
 
Ina maana JK kampa Mwandosya uwaziri kwa kinyongo? Kumnyima aliogopa reaction? Je tatizo la afya yake haina mkono wa mtu?

Ktk maisha, bora adui anayekukasirikia kuliko anayekuchekea maana utampa nafasi atakusogelea na kukuzuru.

Nakumbuka ya Mwakyembe alivyokuwa mbunge alikuwa safi, alipopata uwaziri afya ikaleta matatizo tukasikia mengi mara unaweza kugusishwa tu sio lazima ulishwe bora unapokuwa tofauti kuanza mapema uking'ang'ania chamani unakuwa karubu nao wana ku do.

there you are dear, kusema kwamba yeye hakuweka kinyongo si kweli, pia tunamjudge kwa pesonality na atitude zake, kuna mtu yuko very smart, anaweza kuact kama hana shida na wewe lakini, kama ungefunuliwa moyo wake ungekimbia ufe. asiporekebisha hiyo kauli basi ajue ametoa majibu ya maswali mengi, loh
 
kwa kuwa Mark Mwandosya alivunja kundi lake baada ya kampeni na kumnadi mgombea Urais (Kikwete) kwa nguvu zote hasa katika mikoa ya kusini na Mbeya hakukuwa na sababu ya kutolea mfano huu labda kama gazeti limetia chumvi.

Kitendo cha mwandosya kuvunja kambi yake kwa matendo ndicho kilimpa fursa Rais Kikwete kumteua ndani ya serikali yake. Kama kambi hizo zingeendelea kwa lengo la kumhujumu sidhani kama Mwandosya angekuwa mmoja wa viongozi katika serikali yake.
 
Kipindi hiki ambacho Mwandosya anaumwa na kuwepo kwa hisia kwamba alilishwa sumu ingawa sio lazima iwe kweli kulikuwa na umuhimu wa kutoa mfano wa jumla kwamba serikali yake imejumuisha watu ambao hawakuwa wa kambi yake( Kikwete) na wajumbe wa mkutano mwangemwelewa.
 
"Zifanyike jitihada za mabadiliko" Only words,angechukua hatua kwa wote waliobainika. actions speaks louder!

aiseeeee umeona eee huyo ndio rais wetu anachojuwa sio kuchukuwa hatua ..kama rais kasema hivyo basi yameisha sasa unategemea takukuru wafanyeje tena zaidi ya wao nao kuwa sehemu ya rushwa ....na mamvi nae kakazana eti vijana ni bomu mbona hasemi nini kifanyike na yeye yupo jikoni

 
Am still in disbelief about this kauli

JKMJM.jpg


IMG_2525.JPG


h1.jpg
 
Kwa wale wanaoelewa zaidi, Je, hapo kuhusu Prof. Mwandosya alikuwa na maana gani? Kwamba kambi ya Mwandosya ilihusika katika mambo ya ajabu aliyotendewa?

hakuna chanzo kingine cha taarifa hii zaidi ya Tanzania daima? Vyama hivi (CCM na CHADEMA) ni mahasimu ni sawa na kuikuta taarifa ya chadema kwenye gazeti la uhuru na kuipa uzito mkubwa bila kutafuta chanzo kingine na kulinganisha. Magazeti haya ya vyama wakati mwingine yanaongeza chumvi kwa masilahi ya chama.
 
Hii inaonyesha alimpa uwaziri akijua kuna kipindi atamtumia kama reference yake kwa wengine,
kuwa alimpa uwaziri japo hakutaka kumpa maana si kundi lake na kuwa alimpinga.
 
Huyu Vasco da Gama namshangaa sana habari ya kumtaja mtu baada ya miaka nane kupita ina maana gani tena, anataka tuamini kuwa Prof Mwandosya alimfanyia mambo mabaya?
Ndugu yangu unaona ni miaka 8 wengine wataona miezi 5 soma kitabu cha Mwandosya kibba maana gani wakati Jk bado Mkiti
Miaka 8 makundi km South Corridor lilikuwa la nani km sio wasukuma (na kanda ya ziwa yote) kukataa
Kushuka ktk mabehewa
Nataka kusema kila Uchaguzi wa Chama chochote huwa na makundi uchaguzi ukiisha yanakufa yasipokufa kinachotokea aulizwe Kafulila.au Mrema
 
Makundi ya uhasama kayaasisi mwenyewe!! Asitafute mchawi. Aendelee nalo hilo jini lake asitake kumtupia Mark.
Yeye mwnyewe alishasema alikuwa na kundi la mtandao tangu 2005. Anasahau? Mtandao wa kuchafua ye yote alikuwa na nia ya kugombea urais.

Wasaidizi wake muwe mnamkumbusha aliyosema, Kauli zake zinakinzana mno. Tafadhali msaidieni
 
Kwa wale wanaoelewa zaidi, Je, hapo kuhusu Prof. Mwandosya alikuwa na maana gani? Kwamba kambi ya Mwandosya ilihusika katika mambo ya ajabu aliyotendewa?
Mkuu hata mimi nimeliona hilo, Kwa kuweka pamoja matukio, naamini Ugonjwa wa Mwandosya una mkono wa JK. Ule mfano unammaliza JK, na ni jibu la swali tunalojiuliza kila siku. JK ni mtu wa visasi, hawezi kumwacha mtu, tumeona alivyomwangamiza Salim Ahmed, Salimin Amour, Prof Mbawala nk
 
“Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu,” alisisitiza.

Kweli CCM inaye mwenyekiti kauli hii ya kumtaja mtu na tukichukulia Matatizo aliyopata Mwandosya na tukiangalia visasi ndani ya CCM napata ufahamu sasa kwa nini Mwandosya aliugua.
 
"Tunataka kiongozi akisema anachukia rushwa nasi tukitazama uso wake utuonyesha kwamba anachukia rushwa kweli, siyo maneno tu"- Mwl. JK Nyerere 1995.


“Kweli tusipokemea vitendo hivi na kuviacha vikiendelea, tutakipeleka chama mahali pabaya, ninasikitika sana kusikia
hata wanawake sasa wanajihusisha na utoaji rushwa ili kununua nafasi za uongozi kitu ambacho ni hatari sana,” alisema Kikwete.

Kwenye red: R
ushwa ni mfumo wala hauangalii jinsia wala rangi.


 
Mkuu hata mimi nimeliona hilo, Kwa kuweka pamoja matukio, naamini Ugonjwa wa Mwandosya una mkono wa JK. Ule mfano unammaliza JK, na ni jibu la swali tunalojiuliza kila siku. JK ni mtu wa visasi, hawezi kumwacha mtu, tumeona alivyomwangamiza Salim Ahmed, Salimin Amour, Prof Mbawala nk

Salmin Amour na Mbawala sijakusoma hapo mkuu...;
 
Back
Top Bottom