Makubwa - Mbunge ashiriki chakula cha Krismasi na wafungwa

Huyu jamaa ni noma. bungeni alishawahi kumwambia spika kuwa wahujumu uchumi kwa ufisadi wanyongwe
kabla ya hapo alitaka kutumbukia ziwani akiwa kwenye mtumbwi anatoka kuwaona wapiga kura wake. Huyu jamaa anawaokoa sana magamba kwa mambo yake.
Hili alilolifanya ni jema sana kwa kweli.

Wewe ndiye unayefuatilia na kuona yote hayo, wengine hapa ni kuangalia upande mmoja, kwani wengine fikra zao ni kwamba hawa magamba hata angejitahidi namna gani wanaendelea kumwacha ndani ya kapu la samaki wanaonuka uozo licha ya ukweli kwamba kuoza kwa samaki mmoja si kuhalalisha tenga zima kutupwa.
 
umenena kweli mkuu angekuwa ni mbunge wa CHADEMA hapa misifa ingezidi maelezo tuwe wakweli pale linapofanywa jema na mbunge wa Magamba
 
Nashikiria mbavu zangu!:biggrin::lol:

Hapa JF tupo watu tofauti tofauti usishangae wengine wapo kupotezea muda wakati wengine wanajadili mambo mazito, ndio majukwaa huru yanavyokusanya ngano na magugu.
 
Kwani Candid scope ni mwandishi wa habari wa Deo Filikunjombe? maana kila upupu ukifanywa na Deo lazima utalipotiwa na Candid, au niyeye mwenyewe Deo anajiita Candid?

Unajua mambo ya JF lazima atakuwa Deo mwenyewe. Anatafuta publicity cheap.
 
Ni kweli kabisa Deo ni mwandishi by professional na anajaribu kuwahadaa watu wa Ludewa kwa kutumia taaluma yake!!
Ludewa wana matatizo lukuki kama ya barabara mbovu, Uhaba wa vituo vya afya na watumishi, mashule mabovu yenye waalimu wachache, Uhaba wa visima vya maji tarafa ya Masasi, Mwambao , Njaa karibu nusu ya jimbo lake nk. Badala ya kushughulikia mambo hayo na kutoa progress yake anatuma taarifa ya kula na wafungwa ambayo siyo ishu ya msingi huko Ludewa. By the way Mh DEO kuna ahadi ile ya meli ya tani 400 ya JK kule ziwa Nyasa, je imefikia wapi?
Deo Tunakujua vizuri sana Tekeleza wajibu wako Sifa zitajileta zenyewe!!!!!!
 
Majukumu aliyo nayo Filikunjombe lini atakuwa na muda wa kuchambua mambo hapa JF kila siku? Wengine wanaropoka bila hata kutathmini , maana hata kufanya upembuzi na ziada badala ya kufanya tadhmini ya kutosha. Bora tuache, maana wengine wakikosa cha kuchangia basi ili mradi aandike kitu hapa, niulize mie mwandishi niliyeandika haya badala ya kuanza kumsuta mtu na pengine hajui hata kama kuna mada hii hapa JF.

Isitoshe huyu mwandishi ungeweza kumsoma vizuri kama ni Filikunjombe au la kutokana na uchambuzi wake unavyotalii hapa duniani iwe ya Ujeruamani, Italia, Marekani, Kulyamba lya Mfipa, Sekenke, Kwamtoro kule njia panda ya Singida na Kondoa, Kule Babati, Kula Ntwara (Mikindani nk.), Makongorosi kule njia panda ya Itingi na Tabora kuelekea Sikonge, Moshi, Kule miamba ya Kwimba kabla hujaingia rock city, Kule Serengeti na seronera kabla hujatua kijijini Butiama, Biharamulo na Karagwe anakopenda kwenda badala ya Bukoba kwa vile Bukoba hakuna barabara ya lami, Kirando mwambao wa ziwa Tanganyika, Tunduru vijiji vya Nakapanya - Nanguruwe mpakani na Masasi, bora niishie hapa maana wengine ninavyoorodhesha ni sawa na kumwambai habari za mwezini ambako ni habari za kufikirika kadiri zinavyofahamika ingawa maastronati wametuhakikishia uwepo huo.
 
Ni kweli kabisa Deo ni mwandishi by professional na anajaribu kuwahadaa watu wa Ludewa kwa kutumia taaluma yake!!
Ludewa wana matatizo lukuki kama ya barabara mbovu, Uhaba wa vituo vya afya na watumishi, mashule mabovu yenye waalimu wachache, Uhaba wa visima vya maji tarafa ya Masasi, Mwambao , Njaa karibu nusu ya jimbo lake nk. Badala ya kushughulikia mambo hayo na kutoa progress yake anatuma taarifa ya kula na wafungwa ambayo siyo ishu ya msingi huko Ludewa. By the way Mh DEO kuna ahadi ile ya meli ya tani 400 ya JK kule ziwa Nyasa, je imefikia wapi?
Deo Tunakujua vizuri sana Tekeleza wajibu wako Sifa zitajileta zenyewe!!!!!!

Ahadi za Kikwete ni jukumu la serikali kutekeleza ambalo halimhusu Filikunjombe moja ka moja. Yeye binafsi baada ya kuona ahadi hizo hazitekelezeka, ameamua kwa hiari na moyo alio nao kwa wapiga kura wake kuchangia kila alicho nacho sawa na baba asiyekubali kumwacha mtoto wake afe kwa njaa, bora ampe kidogo kinachowezekana kadiri ya nafasi na uwezo unavyomruhusu.
 
Majukumu aliyo nayo Filikunjombe lini atakuwa na muda wa kuchambua mambo hapa JF kila siku? Wengine wanaropoka bila hata kutathmini , maana hata kufanya upembuzi na ziada badala ya kufanya tadhmini ya kutosha. Bora tuache, maana wengine wakikosa cha kuchangia basi ili mradi aandike kitu hapa, niulize mie mwandishi niliyeandika haya badala ya kuanza kumsuta mtu na pengine hajui hata kama kuna mada hii hapa JF.

Isitoshe huyu mwandishi ungeweza kumsoma vizuri kama ni Filikunjombe au la kutokana na uchambuzi wake unavyotalii hapa duniani iwe ya Ujeruamani, Italia, Marekani, Kulyamba lya Mfipa, Sekenke, Majimoto kule njia panda ya Singida na Kondoa, Kule Babati, Kula Ntwara (Mikindani nk.), Makongorosi kule njia panda ya Itingi na Tabora kuelekea Sikonge, Moshi, Kule miamba ya Kwimba kabla hujaingia rock city, Kule Serengeti na seronera kabla hujatua kijijini Butiama, Biharamulo na Karagwe anakopenda kwenda badala ya Bukoba kwa vile Bukoba hakuna barabara ya lami, Kirando mwambao wa ziwa Tanganyika, Tunduru vijiji vya Nakapanya - Nanguruwe mpakani na Masasi, bora niishie hapa maana wengine ninavyoorodhesha ni sawa na kumwambai habari za mwezini a,balp ni habari za kufikirika kadiri zinavyofahamika ingawa maastronati wametuhakikishia uwepo huo.
Wewe kiazi unajiita MWANDISHI na upupu wako huu!! Labda ni mwandishi wa gazeti lenu huko Ludewa linalotoka mara moja kila baada ya miaka mitano. Eti filikunjombe yupo busy, hao wenzie kama akina Mnyika wanaoandika articles ambazo ni ANALYITICAL hawapo busy!! Narudia, nadhani jina lako zuri ni KIAZI tena kilichochemshwa tayari kwa kuliwa.
 
Ukitaka kumjua anayeishiwa hoja ni kuanza kuvurumisha matusi, wenye kutumia akili na utashi hujibu hoja na kujadili mada. Mimi kwa taarifa yako si wa kiwango chako, najadili na wanaopenda kujadili isues badala ya hulka kama hiyo. Simtusi mtu hapa, na kama sina cha kuchangia mada bora ninyamaze badala ya kuanza kumshambulia mtu binafsi nje ya hoja inayojadioliwa.

Kwa taarifa tu nikiwa mwanaharakati sitachoka kutangaza mazuri yanayofanya na watanzania wenzangu kwa vile mimi si papeti wa chama fulani, bali ni mzalendo ninayeangalia zaidi utaifa, ndio maana naangalia pande zote mbili za sarafu, kwa msimamo huo niko na dhamiri safi na amani ndani ya moyo wangu ndio maana hoja ndiyo inayotawala badala ya kumshambulia mtu.

Wakomavu wanajua hili kuwa, hachukiwi mtu, yanachukiwa mabaya anayotena, hapendwi mtu, bali yanapendwa mazuri yatendwayo na mtu yule. Mtu ni nafsi isiyoonekana, na matendo yanayoonekana yanatokana na nafsi ile, miili tuliyo nayo ni udongo tu na hatuna sababu ya kuichukia kwa vile itaoza tu, ila nafsi tusiyoiona kwa macho yetu ndiyo inabaki na ndiyo inayofanya tuyaonayo kwa kuwakiliwa na mwili huu tunaouna. Hivyo ndivyo sababu ya kutochukia mtu, bali matendo yake, ndivyo tunavyomwongelea mtu si kutokana na mwili wake ila matendo yake.

Mwili kama mwili ni ule ule ambao kila binadamu anao na mwili huo kama ungekuwa unafanya kazi kama ilivyo mashine tungekuwa tunawaza namna moja, kutenda namna moja nk, lakini hali si hivyo kwa kuwa mwili si kitu ambacho unaweza kufanya programming, bali kuna kitu ambacho nimekiongelea hapo juu ndio maana tunatofautiana kimtazamo, kimatendo na kimawazo. pole naona niache kuichambua falsafa ya binadamu tuendelee na kuchangia mada.
 
Ni kweli kabisa Deo ni mwandishi by professional na anajaribu kuwahadaa watu wa Ludewa kwa kutumia taaluma yake!! Badala ya kushughulikia mambo hayo na kutoa progress yake anatuma taarifa ya kula na wafungwa ambayo siyo ishu ya msingi huko Ludewa. By the way Mh DEO kuna ahadi ile ya meli ya tani 400 ya JK kule ziwa Nyasa, je imefikia wapi? Deo Tunakujua vizuri sana Tekeleza wajibu wako Sifa zitajileta zenyewe!!!!!!

Lukuwi, fuatilieni vyombo vya habari au hansard za bunge. Kuhusu ahadi ya meli, nimemsikia Filikunjombe akilizungumzia hili. La sivyo, kama huwezi kusikiliza bunge, nenda kilondo, au lifuma, au lumbila au lupingu ukawaulize swali hili, vipi kuhusu meli mbunge anasemaje, watakupa majibu.
 
DSCF5358.JPG
DSCF5355.JPG

MBUNGE FILIKUNJOMBE AMWAGA MISAADA KWA WAGONJWA NA HOSPITALI YA LUDEWA

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (pichani anayembusu mgonjwa ) ameendelea kutenda kwa vitendo katika kuwatumikia wapiga kura wake ,baada ya safari hii kuamua kuwatembelea wagonjwa wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa na kuwapa misaada mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukabidhi misaada ya mashuka ,magodoro ,kandambili na mablanketi kwa uongozi wa Hospitali hiyo .

Mbunge huyo alikabidhi msaada huyo pamoja na fedha za matumizi kwa wagonjwa hao kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Mwaka mpya. Akikabidhi msaada huo kwa wagonjwa na mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa Happines Ndosa ,mbunge Filikunjombe alisema kuwa amelazimika kuwafariji wagonjwa hao kama njia ya kuwakumbuka na kuwapa faraja zaidi.

Alisema kuwa misaada hiyo ambayo imeikabidhi kwa wagonjwa na Hospitali hiyo inagharimu zaidi ya shilingi milioni 2 na kuwa amefanya hivyo ili kuwafanya wagonjwa hao kula sikukuu kwa faraja zaidi.​
 
Haya, hakuna kurudi nyuma hadi kieleweke, na wanaompinga ndio wanachochea aongeze speed na kazi nzito kumkuta ili kuovertake, hehehe! jamaa ameamua si mchezo, hii speed si ya kawaida.
 
Ukitaka kumjua anayeishiwa hoja ni kuanza kuvurumisha matusi, wenye kutumia akili na utashi hujibu hoja na kujadili mada. Mimi kwa taarifa yako si wa kiwango chako, najadili na wanaopenda kujadili isues badala ya hulka kama hiyo. Simtusi mtu hapa, na kama sina cha kuchangia mada bora ninyamaze badala ya kuanza kumshambulia mtu binafsi nje ya hoja inayojadioliwa.

Kwa taarifa tu nikiwa mwanaharakati sitachoka kutangaza mazuri yanayofanya na watanzania wenzangu kwa vile mimi si papeti wa chama fulani, bali ni mzalendo ninayeangalia zaidi utaifa, ndio maana naangalia pande zote mbili za sarafu, kwa msimamo huo niko na dhamiri safi na amani ndani ya moyo wangu ndio maana hoja ndiyo inayotawala badala ya kumshambulia mtu.

Wakomavu wanajua hili kuwa, hachukiwi mtu, yanachukiwa mabaya anayotena, hapendwi mtu, bali yanapendwa mazuri yatendwayo na mtu yule. Mtu ni nafsi isiyoonekana, na matendo yanayoonekana yanatokana na nafsi ile, miili tuliyo nayo ni udongo tu na hatuna sababu ya kuichukia kwa vile itaoza tu, ila nafsi tusiyoiona kwa macho yetu ndiyo inabaki na ndiyo inayofanya tuyaonayo kwa kuwakiliwa na mwili huu tunaouna. Hivyo ndivyo sababu ya kutochukia mtu, bali matendo yake, ndivyo tunavyomwongelea mtu si kutokana na mwili wake ila matendo yake.

Mwili kama mwili ni ule ule ambao kila binadamu anao na mwili huo kama ungekuwa unafanya kazi kama ilivyo mashine tungekuwa tunawaza namna moja, kutenda namna moja nk, lakini hali si hivyo kwa kuwa mwili si kitu ambacho unaweza kufanya programming, bali kuna kitu ambacho nimekiongelea hapo juu ndio maana tunatofautiana kimtazamo, kimatendo na kimawazo. pole naona niache kuichambua falsafa ya binadamu tuendelee na kuchangia mada.

Deo Filikunjombe tumekuelewa. Hata hivyo, kama alivyoshauri jamaa mmoja hapo juu, badala ya kutafuta cheap popularity kwa mwamvuli au jina bandia la MWANAHARAKATI nakushauri tumia muda wako mwingi kuwatumikia wananchi. Sifa zitakufuata tu hata uvunguni mwa kitanda. Ludewa ni wilaya tajiri sana kirasilimali lakini wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa. Kwa hiyo una kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kubwabwaja bwabwaja humu JF na story za kijinga eti za kula na wafungwa kana kwamba ni jambo la ajabu wakati watu wengi tu wakiwemo viongozi wa dini wamekuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kuwatembelea wafungwa na hatusikii publicity yoyote ya kijinga kama ya kwako.

Ushauri wa bure:
(1) WANANCHI WA LUDEWA WANAHITAJI NYAVU NA SIYO
SAMAKI

(2) Ukitaka wananchi wakukumbuke basi watumikie vema. Waletee maendeleo na SIYO KUANDIKA JINA LAKO KWENYE MISAADA UNAYOWAPATIA. After all, HUO SIYO UUNGWANA KUWAPATIA MISAADA WANANCHI KAMA HAYO MASHUKA UKIWA UMEANDIKA MAJINA YAKO. KWANI WEWE NI KAMPUNI INAYOJITANGAZA!!!! USHAMBA MWINGINE BWANA!
 
Back
Top Bottom