MAKUBALIANO YA SIRI: JK aahidi kumrudisha Lowassa madarakani

itachukua muda mrefu sana kama siyo karne, kwa watanzania kujua haki zao na kuzisimamia. Watanzania asili yetu ni watu wa kujipendekeza kwa wakubwa hata katika mambo ya kipuuzi.
ni njaa tu na uzembe wa kutafuta kula na kutaka vya dezo ndugu yangu inayowafanya watu wajipenpekeze kwa wakubwa......ila njaa hiyohiyo itakapozidi ndio italeta mageuzi...
Amini amini nakwambia mageuzi hayako mbali.....kwa utawala huu wa jk na njaa kali mageuzi yako njiani...ingekuwa enzi ya mwinyi usemi wako hapo juu ungekua kweli
kunahotuba mwaalimu alitoaka akasema mnapowabana na kuwanyonya wananchi...............
 
Great thinker wanajadili tetezi???? Upuuzi mtupu!Sikutegemea kuona majina makubwa kwenye hii mada kwa sababu ni tetezi.
 
Tatizo na sisi tukiamua kumchukia mtu hatutaki hata kusikiliza mema yake...kwa maoni yangu Lowassa ataendelea kuwa mfano wa kuigwa katika utendaji wa waziri mkuu ndani ya Tanzania (ukiachilia suala la ulafi wa kupindukia).

Lowassa ni mtendaji anayependa kuona matokeo na si longolongo za kisiasa na kwa uhakika kabisa mtakubaliana nami kuwa alifanya mambo mengi ktk kipindi kifupi alichokaa madarakani. Sisi wa mikoani ndio tunajua utendaji wa Lowassa kwani tulikuwa tunaona kwa macho yetu jinsi wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wa mikoa na wilaya walivyokuwa wanahaha wakisikia ziara ya waziri mkuu kwani alikuwa hapendi siasa bali vitendo.

Kwa hiyo tukiachana na suala la kupenda pesa ambalo nadhani mpaka sasa atakuwa ameshajifunza, Lowassa should be given another chance...we all make mistakes, and we shouldnt be defined by our mistakes but our achievements!!!
 
except Lowassa.. hivi umemsikiliza? yeye hajafanya kosa lolote na kwa maneno yake anasema yeye yuko "clean".
 
Mukulu hatuna vyeo vya Wakurugenzi wa Mikoa,badala yake katika mkoa tuna watu wenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa (Regional Administration Secretary kwa kifupi RAS)
 
kwa JK na CCM kila kitu kinawezekana... kidumu chama cha mapinduzi...

nawahi kuchukua fomu, nitarejea tena kuwapa maendeleo ya huko jimboni.....
 
Mukulu hatuna vyeo vya Wakurugenzi wa Mikoa,badala yake katika mkoa tuna watu wenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa (Regional Administration Secretary kwa kifupi RAS)

Baba wa Taifa alitoa mfano ambapo mke wa mfalme kwa kuhisiwa tu kafanya uzinzi , ingawa ikaja thibitika kuwa hakutenda, bali yule mke aliachwa kwa kigezo cha kukosa uadilifu.

Kwa EL haihitajiki , kama alitenda au la, kwa kile kitendo cha kuhusishwa na kashfa zote hizo Richmond nk, nk, basi yatosha kwamba apishe wengine katika uongozi.

Watu wengine wanasema, yeye ni mtendaji mzuri, ingawa ana tatizo la tuhuma za ufisadi basi akubalike kwani anajenga nchi!!!!!

Hivi ukiajili askari wa kulinda nyumbani kwako, kwa vile anapendwa na watoto, familia na wengine, lakini unasikia ana tuhuma za kula njama za wizi, basi utaendelea kuwa naye kwa vile anaonekana ana bidii ya kazi, bidii ya kazi au uchapakazi atautumia siku kukuliza wewe mwenyewe!!!

Nyerere alisema kiongozi ambaye hana sifa ya uadilifu kwa kumpima au kwa kudhihirika hana sifa, hafai hata kidogo!

Mwisho chukua mfano huu, umeoa mke , ni mchapa kazi , anasafisha nyumba, anahudumia wageni vizuri, na hata miradi ya maendeleo ya familia anasimamia vizuri, lakini unagundua ana mahusiano ya nje ya ndoa, yaani ametengua kiapo cha uaminifu wa ndoa, je utaendelea kuishi naye kwa kigezo cha uchapakazi???

Mbona viongozi wenye ueledi, sifa, uadilifu wa kuongoza nchi wapo wengi. Hii nongwa ya kutaka uraisi kwa udi na uvumba ni kwa nini?

Watanzania tukumbuke la kuvunda halina...........
 
Jamani, Lowasa kwani si mtanzania kama walivyo watanzania wengine?. Ina maana hana haki ya msingi ya kugombea uongozi ndani ya Tanzania?.

Tusiwe kama wayahudi waliokuwa wanashangalia na kushabikia kwamba YESU asulubiwe bila kujua hali halisi ya mambo.

Hivi hapa jamvini kuna mtu anaweza kuja na facts kuonesha na kudhibitisha mabaya na machafu ya Lowasa?.

Bila shaka ni wachache sana hapa jamvini wanaojua ukweli kwanini Lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu na pia kwanini hakupewa nafasi ya kujieleza mbele ya kamati ya Mwakyembe.

Jamani shilingi ina pande mbili, hivyo kuweza kujua urembo wa shilingi ni hekima kuangalia pande zote.

Wengi mlifurahi sana kuona Lowasa amejiuzulu uwaziri mkuu, lakini mliweza kujiuliza kujiuzulu kwake katika nafasi hiyo kuliwapa faida gani hapa jamvini ama ndani ya Tanzania?. Mnaimba kwamba Lowasa alikuwa ni fisadi, sasa amejiuzulu uwaziri mkuu je ufisadi umekoma ama umeisha ndani ya Tanzania?.

Hapana Lowasa si kama watanzania wengine, yeye tayari ameshapoteza sifa za kuwa kiongozi, watu watasema mengi lakini ukweli kwamba yeye na RA ndio walimuweka JK madarakani basi moja kwa moja hawezi kukwepa kashfa ya Kagoda kama vile RA asivyoweza. EL ni mjanja sana, sasa sisi wdanganyika hatutakubali watuletee ujanja wa sungura. EL ni fisadi na fisadi tu, sasa arudi madarakani ndipo wadanganyika tutakapoamka.
 
Mukulu hatuna vyeo vya Wakurugenzi wa Mikoa,badala yake katika mkoa tuna watu wenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa (Regional Administration Secretary kwa kifupi RAS)
Ni kupitiwa kidogo tu mkuu...i meant wakurugenzi wa halmashauri na manispaa
 
except Lowassa.. hivi umemsikiliza? yeye hajafanya kosa lolote na kwa maneno yake anasema yeye yuko "clean".

Seriously speaking hivi Lowassa amefanya kosa gani??hata hiyo ripoti ya kina Mwakyembe yenyewe haikutaja makosa aliyofanya...Kosa pekee alilofanya ni kutengeneza maadui wengi kuliko marafiki ktk mchakato mzima wa tokea Mtandao mpaka walipochukua madaraka. Kama alihusika ktk kutenda kosa lolote (hapa namaanisha kuvunja sheria zozozte za nchi) angekuwa amefikishwa mahakamani au anachunguzwa kama walivyo akina Karamagi na Msabaha. Tuacheni chuki binafsi!
 
Lowassa is NOT a clean man. Ana utajiri mkubwa sana usioleweka chanzo chake (unexplained wealth). Pia he is motivated by personal financial wealth, hivyo daima anafikiria jinsi kujilimbikizia mali.

Fisadi huyu anastahili KUSHITAKIWA kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma (abuse of public office) na kuisababishia serikali hasara kwa kuingiza kwenye mkataba wa rushwa wa Richmond. Si sahihi yeye kusema kuwa hajafanya kosa kwani siye aliye saini mkataba wa Richmond. Ukweli ni kuwa yeye ndiye aliyeunda kamati kushuhulikia tenda ya umeme na kuipokonya Tanesco kazi hiyo. Yeye alifanya ufuatiliaji wa karibu wa tenda hiyo na kuiagiza kamati yake itoe tenda kwan Richmond na kukiuka sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) na ku-ignore ushauri wa Tanesco.

Uhalifu uliofanywa na Lowassa kwenye Richmond ni sawa na makosa ambayo Liyumba alihukumiwa kwenye kesi ya Twin Towers na ni sawa pia na makosa yanayo wakabili mawaziri wa zamani Daniel Yona na Basil Mramba kwenye kesi ya Alex Stewart Assayors.

Lowassa ameonyesha dharau kwa wananchi wa Tanzania na kejeli kwa Bunge la Tanzania kwa kusema kuwa hajajutia makosa yake kwenye Richmond.

NI AIBU KUBWA SANA KUWA SWAHIBA MKUBWA WA LOWASSA, RAIS JAKAYA KIKWETE, AMEAMUA SASA KUJITOKEZA HADHARANI KUMTETEA MHALIFU HUYU IKIWA NI MAANDALIZI YA KUMRUDISHA TENA MADARAKANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA ILI AMRITHISHE UTAWALA WA NCHI KIHUNI KAMA WALIVYOKUBALIANA KWENYE MTANDAO WAO TANGU MWAKA 2005.

Huu ni uhaini wa demokrasia na mustakabali wa nchi na ni sawa na kunyea kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Nimemuota Lowassa leo akiwa amezungumza kwa undani sana. Ilikuwa ni siku ya mwisho ya Kikao cha Bunge ambapo hatimaye aliamua kuzungumza kwa "vipengele". Hotuba yake Bungeni (katika njozi yangu, na huwa nina sababu za kumuota huyu jamaa) ilichukua muda kuanza kuzama kwa wasikilizaji na matokeo yake ni aliweza kuonekana akishangaliwa na wabunge mbalimbali ambao walitambua nguvu yake na kuswitch allegiances zao. Watu wawili wakawa casualties wa move hiyo ya kisayansi ya Lowassa... It was just a dream but it is more than a dream.

Hahaaaa, kaka we unajiandaa kumrithi Sheikh Yahya?
 
Hii inanirejesha pale nilimuona lowassa akizungumza na Tido Mhando kwa kujiamini huku akijua hakuna atakae thubutu kumponda. Daah hii nchi inatia hasira kweli kweli.
 
Bado ni tetesi na zitabaki ni tetesi. Lakini JF huwa inapata siri nzito . Yaweza kuwa kweli. Mzee wa datas yuko ndani ya shughuli nzito za uchaguzi kiasi haonekani hapa kuleta this sort of datas. Labda naye anasubiri uchaguzi ukiisha ndipo atuletee datas zake.

Nafikiri mpaka sasa umeishapata jibu
 
Mimi pia nimesikia maneno haya yakizungumzwa na watu wakubwa serikalini. Wanasema kuwa Lowassa na Rostam Aziz walimweka madarakani Kikwete mwaka 2005 kupitia Mtandao kwa makubaliano kuwa Rais Kikwete atamteuwa

Lowassa kuwa PM na kumrithisha Urais 2015. Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa habari iliyoandikwa na MwanaHalisi hivi karibuni kuwa "Kikwete amtosa Lowassa" si sahihi hata kidogo.

Yanazungumzwa pia kuwa wamiliki na wahariri wa vyombo vikuu vya habari hapa Tanzania sasa hivi wameshaingia upande wa Lowassa na kuanzia sasa hakuna habari yoyote mbaya itakayoandikwa kuhusu Lowassa ili kumwekea mazingira ya kurudi kwenye uongozi wa kitaifa.

Magazeti ya New Habari Corp. yanayo milikiwa na Rostam Aziz - Mtanzania, Rai, The African, Dimba, etc yamepewa amri ya kuhakikisha kuwa kuna habari na picha za kumpamba Lowassa kila siku ili asisahaulike na wananchi.

Ukweli au uongo wa tetesi hizi tutazijua Novemba mwaka huu Rais Kikwete atakapofanya uteuzi wa Baraza lake jipya la Mawaziri!

Ni mimi nimechanganyikiwa au HUYU bwana amechanganyikiwa??? maana sijamuelewa hapa.... kuwa november kuna baraza jipya tena la mawaziri??? Nani kasema hivyo??? Ushahidi gani?? ni sababu ipi mpaka unataja na actual mwenzi kuwa kuna mabadiliko?? Sijakuelewa kabisa ndugu.
 
Lowassa is NOT a clean man. Ana utajiri mkubwa sana usioleweka chanzo chake (unexplained wealth). Pia he is motivated by personal financial wealth, hivyo daima anafikiria jinsi kujilimbikizia mali.

Fisadi huyu anastahili KUSHITAKIWA kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma (abuse of public office) na kuisababishia serikali hasara kwa kuingiza kwenye mkataba wa rushwa wa Richmond. Si sahihi yeye kusema kuwa hajafanya kosa kwani siye aliye saini mkataba wa Richmond. Ukweli ni kuwa yeye ndiye aliyeunda kamati kushuhulikia tenda ya umeme na kuipokonya Tanesco kazi hiyo. Yeye alifanya ufuatiliaji wa karibu wa tenda hiyo na kuiagiza kamati yake itoe tenda kwan Richmond na kukiuka sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) na ku-ignore ushauri wa Tanesco.

Uhalifu uliofanywa na Lowassa kwenye Richmond ni sawa na makosa ambayo Liyumba alihukumiwa kwenye kesi ya Twin Towers na ni sawa pia na makosa yanayo wakabili mawaziri wa zamani Daniel Yona na Basil Mramba kwenye kesi ya Alex Stewart Assayors.

Lowassa ameonyesha dharau kwa wananchi wa Tanzania na kejeli kwa Bunge la Tanzania kwa kusema kuwa hajajutia makosa yake kwenye Richmond.

NI AIBU KUBWA SANA KUWA SWAHIBA MKUBWA WA LOWASSA, RAIS JAKAYA KIKWETE, AMEAMUA SASA KUJITOKEZA HADHARANI KUMTETEA MHALIFU HUYU IKIWA NI MAANDALIZI YA KUMRUDISHA TENA MADARAKANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA ILI AMRITHISHE UTAWALA WA NCHI KIHUNI KAMA WALIVYOKUBALIANA KWENYE MTANDAO WAO TANGU MWAKA 2005.

Huu ni uhaini wa demokrasia na mustakabali wa nchi na ni sawa na kunyea kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kaka umepoteza muda mwingi kumuelewesha mtuambaye ANAJUA FIKA KILICHOTOKEA ila anajifanya hajui.
Katumwa huyo... next tyme ukiona mchangiaji kama huyo hata usisome post yake ni upotevu wa muda tu.
 
Tatizo na sisi tukiamua kumchukia mtu hatutaki hata kusikiliza mema yake...kwa maoni yangu Lowassa ataendelea kuwa mfano wa kuigwa katika utendaji wa waziri mkuu ndani ya Tanzania (ukiachilia suala la ulafi wa kupindukia).

Lowassa ni mtendaji anayependa kuona matokeo na si longolongo za kisiasa na kwa uhakika kabisa mtakubaliana nami kuwa alifanya mambo mengi ktk kipindi kifupi alichokaa madarakani. Sisi wa mikoani ndio tunajua utendaji wa Lowassa kwani tulikuwa tunaona kwa macho yetu jinsi wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wa mikoa na wilaya walivyokuwa wanahaha wakisikia ziara ya waziri mkuu kwani alikuwa hapendi siasa bali vitendo.

Kwa hiyo tukiachana na suala la kupenda pesa ambalo nadhani mpaka sasa atakuwa ameshajifunza, Lowassa should be given another chance...we all make mistakes, and we shouldnt be defined by our mistakes but our achievements!!!

Hapa siyo mahala pa kujifunzia.... kifupi hamna nafasi nyingine !!! Na mkijiroga kumuweka na kulazimisha...."""" hakyamungu utabili wangu, kuanzia trh 01/11/2015 hii nchi itakuwa haikaliki tena"""

Mbona wapo viongozi waadilifu?? Mtu kesha kosa na tanznia ina watu 40ml, then unasema tumpe mtu nafasi nyingine MUMEONA NI NYIE TU NDO MNAWEZA KUTAWALA??? Na wewe hapa umetumwa kupima watu.... unapoteza muda wako.

Kwa sasa sitaki HATA kusikia kuwa aliwahi kufanya jambo zuri. Kwangu mimi HAFAI hata kuwa diwani.
 
Back
Top Bottom