Makosa ya Upinzani

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kwa karibu miaka kadhaa sasa kuna mlolongo wa matukio ambayo yangetokea nchi nyingine yoyote yangetoa nafasi ya pekee kwa vyama vya upinzani. Mlolongo huo kwa Tanzania hata hivyo haujatoa nafasi hiyo kwa upinzani kiasi kwamba kama taifa badala ya kuangalia upinzani kutoa uongozi katika saa na wakati huu bado wananchi wanaangalia CCM pamoja na madudu yake kutoa uongozi kwa taifa.

Hili lawezekana ni kutokana na makosa ya upinzani na vyama vikubwa vya upinzani nchini. Makosa ambayo kimsingi kabisa yamechangia kudhoofisha demokrasia na hivyo kuufanya upinzani wa Tanzania ulivyo sasa kuwa kikwako cha mabadiliko tunayoyataka na kwamba umejenga ukuta wa kuzuia mabadiliko ya kweli kuja kwani wananchi wachache wameweka matumaini katika upinzani huo ingawa ukweli ni ulivyo sasa upinzani wa Tanzania hauwezi kuthaminiwa kuongoza taifa letu.

Kama chama chenye muundo, historia, watu na raslimali nyingi kama CCM kimeshindwa kuongoza mabadiliko ya kweli kwa Mtanzania itakuwaje kwa chama kama CUF au Chadema? Kama CCM imeshindwa kufanya hivyo ndani ya miaka 45 hivi itachukua muda gani kwa upinzani dhaifu kama wa kwetu kufanya hivyo?

Ni makosa gani ambayo upinzani usipoyarekebisha haraka (ndani ya hii miezi 12) hawatastahili kuaminiwa na uongozi wa taifa hata wakiomba kwa machozi?

Au upinzani wetu unasubiri kuombewa na kupepewa ili Mungu hatimaye awaangushie masanduku ya kura kama alivyofanya kwenye masimulizi ya safari ya wana Israeli alipowaangushia mana na kuwapeperushia kware!?

Je yawezekana upinzani wetu umekuwa hauna maana na wananchi wajitahidi kuokoa merikebu inayozama wakijua ina watu wanaoweza kuifikisha mbele kuliko kurukia mtumbwi ambao hauna uwezo wa kukabili mawimbi ya bahari!?
 
Attachments

  • EndingOnePartyDominance.pdf
    97.5 KB · Views: 118
Bado vyama vingi vya upinzani haviendeshwi kama ni vyama vya kisiasa. Vimekaa kama NGO za watu na kuthibitisha hilo ni ugumu wa wapinzani kukaa pamoja kuonyesha interest za kuwapa wananchi alternative katika chaguzi mbalimbali. Wanapigana wao kwa wao bila sababu za msingi.
Tutawaaminije kama wakichukua ofisi ya juu kama wata deliver bila shida, maana ni afadhali kudeal na shetani unayemjua kuliko yule asiyejulikana.
 
Mwanakijii upinzani imara unategemeaa na watu wenyewee katika kujiweka pamoja kwa lengo moja..

Kwa sasa kumekuwa na ushabiki mkubwa kwa wanaojiita wapiganaji wa ufisadi ndani ya CCM kuliko hata waanzilishii wa vita ya ufisadi nchinii..

Napata wasi wasi mkubwa na utekaji nyara huu wa hoja uliofanywa na wapiganaji hao na ushabiki wake kupitia vyombo vya habari...

Kwa mwelekeoo huo tuu waweza kupata picha kamili ya udhaifu wa upinzani nchini unaosababishwaa zaidi na masilahii binafsi (posho mbili nk) kuwekwa mbele zaidi.. Tutegemee nini katika hilii???

Kuwa na watu wazimaa wenye uzoefuu wa kukaa madarakani muda mrefuu wakifaidiii kwa kiasi kikubwaa masilahi ya mfumoo huu,na badoo kujifanya ni wakosoaji wa ndani ili kupata umaarufuu wa njee ni kasoroo kubwa sanaa hata kibinadamu.
 
Upinzani unaoendeshwa na wapenda pesa kuliko wote nchini hauwezi kwenda popote. Ni bora tutibu CCM labda italeta changes.
 
Kwa karibu miaka kadhaa sasa kuna mlolongo wa matukio ambayo yangetokea nchi nyingine yoyote yangetoa nafasi ya pekee kwa vyama vya upinzani. Mlolongo huo kwa Tanzania hata hivyo haujatoa nafasi hiyo kwa upinzani kiasi kwamba kama taifa badala ya kuangalia upinzani kutoa uongozi katika saa na wakati huu bado wananchi wanaangalia CCM pamoja na madudu yake kutoa uongozi kwa taifa.

Hili lawezekana ni kutokana na makosa ya upinzani na vyama vikubwa vya upinzani nchini. Makosa ambayo kimsingi kabisa yamechangia kudhoofisha demokrasia na hivyo kuufanya upinzani wa Tanzania ulivyo sasa kuwa kikwako cha mabadiliko tunayoyataka na kwamba umejenga ukuta wa kuzuia mabadiliko ya kweli kuja kwani wananchi wachache wameweka matumaini katika upinzani huo ingawa ukweli ni ulivyo sasa upinzani wa Tanzania hauwezi kuthaminiwa kuongoza taifa letu.

Kama chama chenye muundo, historia, watu na raslimali nyingi kama CCM kimeshindwa kuongoza mabadiliko ya kweli kwa Mtanzania itakuwaje kwa chama kama CUF au Chadema? Kama CCM imeshindwa kufanya hivyo ndani ya miaka 45 hivi itachukua muda gani kwa upinzani dhaifu kama wa kwetu kufanya hivyo?

Ni makosa gani ambayo upinzani usipoyarekebisha haraka (ndani ya hii miezi 12) hawatastahili kuaminiwa na uongozi wa taifa hata wakiomba kwa machozi?

Au upinzani wetu unasubiri kuombewa na kupepewa ili Mungu hatimaye awaangushie masanduku ya kura kama alivyofanya kwenye masimulizi ya safari ya wana Israeli alipowaangushia mana na kuwapeperushia kware!?

Je yawezekana upinzani wetu umekuwa hauna maana na wananchi wajitahidi kuokoa merikebu inayozama wakijua ina watu wanaoweza kuifikisha mbele kuliko kurukia mtumbwi ambao hauna uwezo wa kukabili mawimbi ya bahari!?

Duh, umetupiga sana. Hata hivyo unfairly. Unapoangalia makosa ya kambi ya upinzani ni vema uangalie 'factors' za ndani na za nje. Katika SWOT analysis hizi ni fursa na vitisho. Hapo utaweza kutoa hukumu sahihi kabisa.

Vilevile ni muhimu sana kuangalia historia ya vyama hivi katika muktadha wa historia ya Tanzania na utamaduni wa kisiasa wa Watanzania. Vyama katika nyakati tofauti - kuanzia kina Marando na Bagenda, Mtei na Makani, Fundikira na Kasanga Tumbo na Mapalala na Seif walipoamua kujitoa mhanga na kuanzisha vyama - kumekuwa na hatu kadhaa zimepigwa katika kujenga dmeokrasia ya kweli katika nchi yetu.

Watu wanaiweka Tanzania katika mizania ya nchi nyingine jambo ambalo ni kosa kubwa maana Tanzania inapaswa kupimwa kutokana na historia yake. Zoezi la ujenzi wa Taifa na kuwa na Taifa moja chini ya uongozi mahiri wa Mwalimu lilifanywa katika misingi ya udikteta mkubwa sana na chini ya amri moja ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tanzania ikajenga jamii ya watu wanaoheshimu mamlaka bila kuhoji na hata vyama vingi vilipoanzishwa vilionekana ni vya wasaliti. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa ambaye alikonga nyoyo za Watanzania na kuaminiwa - Augustino Lyatonga Mrema - lakini naye akavurugwa sana na dola, kuitwa pandikizi na kuondoa kabisa credibility yake katika jamii. Jamii imefanywa kuamini kuwa Mrema ni 'kichaa' na hana sifa ya uongozi. Hii ni kazi iliyopangwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba leo ni watanzania wachache sana ambao wanakumbuka sacrifice ya Mrema katika ujenzi wa demokrasia nchini.

Tusipojifunza na kuelewa historia hii ya vuguvugu la demokrasia Tanzania tutaishia kulaumu watu kila kukicha bila kwenda mbele. CCM itaendelea kutawala na kila baada ya miaka mitano kutakuwa kinatokea chama kina nguvu na baadae kuangushwa, wabunge wenye nguvu na baadae kuangushwa na hata wanasiasa wenye mvuto na baadae kupakwa matope na kunuka.

Demokrasia hulindwa. Viongozi hulindwa zaidi ili kubakia kama alama ya harakati. Raila Odinga aliongoza harakati za mapinduzi Kenya mwaka 1982, akaswekwa lupango kwa miaka zaidi ya tisa na kuishi uhamishoni nchini Norway kwa miaka mingi. Akajiunga na chama cha baba yake mwaka 1992 FORD, kikavunjika na kuwa na FORD-K na FORD-A. Baba yake Mzee Jaramogi alipokufa Raila akataka kunyakua uongozi wa chama, akashindwa na Michael Kijana Wamalwa na Raila akaenda kuanzisha chama chake NDP. Akaivunja NDP na kuingia KANU kuwa Katibu Mkuu na akaipasua KANU vipande 2 na kuanzisha LDP. Akaingiza LDP katika muungano wa NARC na kumpa Kibaki Urais (literally alimpa Urais maana Kibaki alikuwa armchair leader of opposition). Akatoka NARC na kuanzisha ODM-K, akagombana na Kalonzo na kuanzisha ODM na leo ni Waziri Mkuu mwenye nguvu Kenya.
Mchakato wote huu Raila alionekana msaliti, mpenda vyeo na mtu wa vita. Lakini leo huna tena KANU na Raila alipata kuniambia, demokrasia Afrika itaimarika tu iwapo vyama vilivyoleta uhuru vitapasukapasuka na kuondoa ile claim yao ya sisi tulileta uhuru - hii ni claim ya CCM na hata kumkumbatia Mwalimu kama wao.

Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.

Mwanakijiji utaandika mpaka utachoka na kutulaumu mpaka utakasirika. Demokrasia ya Tanzania itajengwa kwa sober approach ya kutazama historia yetu na kujua 'political culture' ya Watanzania. Unatutaka tuchukue fursa inapotokea. Wazo murua kabisa. Lakini capacity ipo wapi? Wapo wap wanaofikiri na kuziona fursa? Wapo wapi watu wanaojenga scenerios na kujiuliza what if?

Tulianza vizuri zoezi la kujenga imani kwa wananchi kupitia Bunge. Tulifanikiwa kupata sizable number ya wabunge wa CCM na kujenga coalition nzuri na kupashana habari. Tukamezwa. Tukajikuta tumewauzia ajenda tukijua kabisa hawatafika nayo mbali.

Ndani ya CCM hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa Rais ajaye kati ya Membe na Lowasa. Hakuna ajenda ya Taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe Mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.

Juzi nilisema hapa JF, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee Sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri - Ignore CCM
 
Mwanakijiji, moja ya mambo yanayonisikitisha sana ni kuwa hawa ndugu zetu wa upinzani ni kuwa kama wanakubali kuwa first runner up. Sasa hivi ni wazi kabisa kuwa mazingira yamepevuka kwa kila hali kwa upinzani kucapitalize, bado hatuoni kitu substantial kutoka kwa upinzani kinachoweza kubadilisha balance of power 2010.

Inaonekana bado yale ya kugombea madaraka ndani ya chama yanaendelea, members wa baadhi ya vyama kutumiwa. Hope inayoonekana sasa ni ya kumeguka kwa CCM, upinzani utakaotokana na kumeguka kwa CCM huenda ndio ukawa firm kuliko wa sasa hivi.

Naweza kuwauliza wakuu wangu hapa Dr Kitila na Mh Zitto, kama Chadema wana strategies zozote au hopes hata za kuchukua majimbo 50 au hata 100 nina wasiwasi majibu yanaweza kuwa si ya kuridhisha.

Sijui kama kuna hata idea ya kukusanya nguvu zao na kupambana na CCM kwa kuachiana majimbo ambayo wanaona chama fulani kina nguvu, and ndio bado wanaplay by the CCM book of divide and rule.

Sasa hivi CCM imepoteza ile hali ya kuaminiwa, na imepoteza hata hali ya kuaminiana kati ya wanachama wake
 
Mfano wa akina Raila kwa Tanzania hauwezekani. Alijaribu Mrema kuutumia akashindwa. Na sio mfano mzuri wa kuigwa. Ni bora twende Ghana tuone wapinzani kule wanafanyaje mambo yao
 
Mh Zitto umetoa uchambuzii mzuri kwa kuitazama vema historia yetu..

Ni vizuri kujifunza kutokana na historia ila mara nyingi huwa hatujifunzi chochote kutokana nayo.

Capacity ya kujenga upinzani imara ni muhimu sanaa..Kwa wananchi na viongozi ila hasa viongozi imara wa upinzani wanahitajika ili kutoa mwanga wa mabadilko kwa jamii.
 
Mfano wa akina Raila kwa Tanzania hauwezekani. Alijaribu Mrema kuutumia akashindwa. Na sio mfano mzuri wa kuigwa. Ni bora twende Ghana tuone wapinzani kule wanafanyaje mambo yao

Ghana ni mfano mzuri. Lakini kumbuka kuwa historia ya Ghana ni tofauti na ya Tanzania kwa kiasi kikubwa sana. Wamepinduana sana na kutawaliwa kijeshi na kuuana. Wanajua machungu ya udikteta. Tanzania tunaambiwa na wataalamu wa siasa kwamba tulikuwa na soft dictatorship na hivyo hakuna hayo machungu.

Pia Ghana kuna middle class kubwa kuliko Tanzania na role ya middle class katika ujenzi wa demokrasia ya kiliberali kama tunayojaribu kujenga ni kubwa.

Hata hivyo katika kila case kuna jambo la kujifunza. Twaweza jifunza Kenya, Ghana na kwingine kokote. Swali ni je tunapata muda huo wa kuangalia mifano hiyo na kulinganisha na mazingira yetu?

Umesoma ENDING SINGLE PARTY DOMINANCE? Mwana JF mmoja alinitafutia na ngoja nishare nanyi. Namtumia Invisible awawekee. Tunaweza kufanya mabadiliko, lakini twahitaji kufikiri vya kutosha!
 
Ndani ya CCM hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa Rais ajaye kati ya Membe na Lowasa. Hakuna ajenda ya Taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe Mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.

Juzi nilisema hapa JF, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee Sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri - Ignore CCM
Kama mnaziona hizo opportunities, mnawashawishi vipi wananchi kuwa mna uwezo wa kuongoza bila pasipo shaka?
Hata hivyo, Mh Zitto failure comes from within na waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako. Muuaji wa upinzani ni upinzani wenyewe kuendekeza mambo yanayoipa system uwezo wa kuwafanyia hujuma. Sidhani kama Mrema alikuwa hajui uwezo wa serikali baada ya kutoka nje. Ila ndo hivyo tena ajilaumu mwenyewe
 
Ghana ni mfano mzuri. Lakini kumbuka kuwa historia ya Ghana ni tofauti na ya Tanzania kwa kiasi kikubwa sana. Wamepinduana sana na kutawaliwa kijeshi na kuuana. Wanajua machungu ya udikteta. Tanzania tunaambiwa na wataalamu wa siasa kwamba tulikuwa na soft dictatorship na hivyo hakuna hayo machungu.

Pia Ghana kuna middle class kubwa kuliko Tanzania na role ya middle class katika ujenzi wa demokrasia ya kiliberali kama tunayojaribu kujenga ni kubwa.

Hata hivyo katika kila case kuna jambo la kujifunza. Twaweza jifunza Kenya, Ghana na kwingine kokote. Swali ni je tunapata muda huo wa kuangalia mifano hiyo na kulinganisha na mazingira yetu?

Umesoma ENDING SINGLE PARTY DOMINANCE? Mwana JF mmoja alinitafutia na ngoja nishare nanyi. Namtumia Invisible awawekee. Tunaweza kufanya mabadiliko, lakini twahitaji kufikiri vya kutosha!

In a nutshell,we are passive people and our history backs us up.
Where did cowards of the Nguni people run to?
And where did losers in the Bantu succession disputes flee to?
The skulkers of Bantu leaders' harsh control?
Need I say more?
 
Ghana ni mfano mzuri. Lakini kumbuka kuwa historia ya Ghana ni tofauti na ya Tanzania kwa kiasi kikubwa sana. Wamepinduana sana na kutawaliwa kijeshi na kuuana. Wanajua machungu ya udikteta. Tanzania tunaambiwa na wataalamu wa siasa kwamba tulikuwa na soft dictatorship na hivyo hakuna hayo machungu.

Pia Ghana kuna middle class kubwa kuliko Tanzania na role ya middle class katika ujenzi wa demokrasia ya kiliberali kama tunayojaribu kujenga ni kubwa.

Hata hivyo katika kila case kuna jambo la kujifunza. Twaweza jifunza Kenya, Ghana na kwingine kokote. Swali ni je tunapata muda huo wa kuangalia mifano hiyo na kulinganisha na mazingira yetu?

Umesoma ENDING SINGLE PARTY DOMINANCE? Mwana JF mmoja alinitafutia na ngoja nishare nanyi. Namtumia Invisible awawekee. Tunaweza kufanya mabadiliko, lakini twahitaji kufikiri vya kutosha!
Na ndio maana niliwahi kutoa maoni yangu humu kwamba kuna makundi mawili hapa nchini hatujayatumia vizuri.

Moja ni wafanyakazi wa Nchi hii. Tangu walipoondoka CCM ambako ilikuwa ni Jumuia kama UWT wamebaki yatima. Matokeo yake kila mfanyakazi na lwake. Baadhi wamejiunga na mafisadi wa CCM kuambulia angalau makombo.

Kundi la pili ni wanafunzi na wanavyuo mbalimbali. Nadhani wewe Zitto ulijiunga na CHADEMA ungali chuoni. Sasa hivi tumewakatisha tamaa wanavyuo wetu. CCM bado wana CHIPUKIZI wao. Watoto wadogo kabisa wanaiimbia CCM, wanazima Mwenge, wanacheza halaiki. Upinzani hamlikemei hili. Watoto wetu wanazaliwa na vyama kama wanavyozaliwa na KABILA na DINI za wazazi wao.
 
Kumradhi wakuu,

Kwenye 1st post ya Mwanakijiji nimeambatanisha na kitabu cha Ending One Party Dominance kilichoandikwa na Dorothy Solinger. Naamini kitasaidia kwenye mjadala huu
 
Ndugu zanguni, wengi wetu naona tunaanza kuongea kwa kukata tamaa. Kwa mbali nina detect a lost hope kwa Mkjj na hata Mh. Zitto. It's justifiable kuwaona mko katika hali hii, kwa yote mliyojaribu kufanya, kwa yote mliyojaribu kufikia na matarajio yote ambayo yameshindwa kufikiwa kifikra, kiuchumi na kisiasa katika Taifa letu. Ina frustrate na kukatisha tamaa.

Kimoja ninachotaka kusema hapa ni udhalimu na uhujumu uliofanyika katika hii nchi yetu tusiusahau kamwe. Kwa mbali ninahisi CCM watakuja na sera za RECONCILIATION around 2015 ili kufukia na kuondoa hasira na chuki iliyojijenga miongoni mwa wananchi wengi dhidi ya watawala wetu. Kwa miaka takribani 8 iliyopita hili Taifa limekuwa raped in broad daylight na tumeshindwa kuwafikisha wahalifu lupango wasitahilipo. Mwamko na mbinu iliyotumika kuleta mabadiliko katika nchi kwa kuibua grand scandals unaonekana kutozaa matunda. Na tunaonekana kukata tamaa, hata wapinzani nao; Nasaha zangu ni kwamba - KAMWE TUSIYASAHAU MAOVU YA HALI YA JUU YALO TENDWA DHIDI YA TAIFA HILI HATA BAADA YA MIAKA 100 IJAYO!! TUHAKIKISHE MALI ZA TAIFA HILI ZINARUDISHWA!
 
Cha AJABU kabisa ni kuona VIONGOZI ndani ya CCM sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote wanachukiana sana lakini HAKUNA anayetaka kutoka humo akasaidiane na akina Zitto! Tutafakari.
 
Jamani lazima tutambue kuwe Kinywa kina nguvu sana, tunapotamkakuwa upinzani umeshindwa au ni dhaifu haitatokea siku utaenda kinyume na vinywa vyetu.Na bahati mbaya shetani anajua kanuni za mungu kuliko hata sisi ambao kanuni hizo tumewekewa na anazitumia kutuangamiza. kama hamamini hebu tujaribu kusema maneno positive kuhusu upinzani, ghafla tutaumba kitu kipya.

Hii inaitwa nguvu ya kinywa
 
Punje ya mharadani au sio?
 
Zitto,

Tatizo la upinzani ni kuiga mambo mengi kama wanavyofanya CCM. Sasa kama mimi natakiwa kuchagua, si ni bora nibaki huko CCM ambako nimekuzoea?

Kuna haja gani ya vyama vya upinzani kuwa na muundo ule ule wa CCM? Kamati kuu, halmashauri kuu, mkutano mkuu, secretariati nyingi nk. Gharama ya kuendesha chama cha namna hiyo mtatoa wapi? Wenzenu wanaweza kuchota KAGODA, je nyie mtatoa wapi? Matokeo yake mnategemea familia moja au mbili wafadhili lakini ubaya wake hao watu wakikosea hamuwezi kuwaadhibu, ni kama CCM wanavyoshindwa kuwaadhibu akina Roastam.

Chama kwa juu lazima kiwe kidogo na badala yake kitanuke kwa chini. Linganishe na mrembo mwenye miguu mikubwa, wowowo la nguvu na juu kachongeka, huwa wanapendeza kuliko limama lenye tumbo kubwa na bichwa kubwa. Samahani kwa kutumia analogy ya namna hiyo. Ninachotaka kusema ni kwamba lazima chama kijijenge kwenye mizizi. Raslimali ya chama lazima itumike zaidi kujenga nguvu kwenye vijiji, kata na wilaya na sio kuendelea kununua magari ya makao makuu na kuajiri watu kibao makao makuu.

Uchaguzi wa serikali za mitaa, mimi nimeshiriki hapa Kyela kuendesha kampeni kuisaidia CHADEMA (sina mapenzi na CHADEMA, tulitaka kuwatungua wapambe wa mbunge wetu) na nimeona udhaifu mkubwa wa CHADEMA huku wilayani. Ilibidi sisi CCM tuchukue uongozi wa kuwaandalia kila kitu na kweli vitongoji vyote ambavyo tuliamua CCM ishindwe, kweli CHADEMA wakashinda. Sasa kama hiyo ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, inaonyesha chama chenu pamoja na publicity kubwa magazetini bado huku vijijini hamna watu na nyenzo za kufanyia kazi.

Jiandaeni kwa hilo mana nafasi ya kuitikisa CCM mwakani mnayo, tena kubwa sana. Vijana wakielemishwa huku vijijini wanaelewa.
 
Nafikiri hapa, Mh Zitto amefafanua vya kutosha, kwanza amesema tunahitaji kufikiri vya kutosha and then ukifikiri vya Kutosha IGNORE CCM. Jamani mimi nafikiri tumefikia wakati ambao Watanzania tunahitaji matendo zaidi kuliko kila siku kulalamika kuhusu siasa chafu za CCM, mimi nafikiri CCM wanatumia hiyo loop ya Watanzania kwa kuwa wanajua kuwa Watanzania ni watu wa kulalamika lakini end of the day ni watu wa kusahau malalamiko yao.

Mimi nasema hivi kutokana na kuwa na uzoefu kidogo kuhusu sisi wenyewe Wabongo, nimewahi kuparticipate kwenye kutengeza strategies pale Geita kutengeza Credibility ya chama, tupate nguvu, tutengeneze program ambayo ikifika 2010 basi ile program izae matunda, lakini cha ajabu watu wengine wakaanza kuona sisi wengine tutakuwa maarufu sana, cha ajabu yakaanza majungu, yaani mtu unaanza kufikiria kuwa hawa watu wana matatizo gani, mtu anataka kutafuta maisha fulani ndani tu ya level kama ile, sasa mtu unaanza kufikiria kuwa je huyu mtu akifika mbali anaweza kuijali familia yangu kweli, make huku tupo ngazi ya Wilaya watu wanaleta majungu what is happening.

Nafikiri Watanzania tunatakiwa kubadilika, tutengeneze taifa ambalo lina Vision, tuache umimi na familia yangu, nafikiri hata akina Odinga wangekuwa na umimi 100% Kenya kusingekuwa na hayo mabadiliko, wakina John Kuffo wangekuwa na umimi Ghana isingekuwa hii tunayoiona ni model for African Politics.

Tanzania tuna-lack sana Trust and accountability, nafikiri tunalack hivi vitu kwa 100% hatuko transparent na tunapenda sana Giza.
 
kwa utaalamu wangu nimegundua kuna matatizo makubwa matatu katika upinzani.

1-viongozi wengi wa upinzani ni ccm.chama hiki kimefanya kazi kubwa sana kuhakikisha vyama vya upinzani kuna mamluki wa ccm,na ndio maana kila upinzani ukija na mikakati fulani ccm wanapata habari na kuzima moto haraka sana,pia kama mnakumbuka wakati mfumo wa vyama vingi ccm ilianzisha vyama feki.,case study NCCR,Ramwai,Marando,nk.
2-Ubinafsi,udini,ukabila,umimi,uzushi,majungu na vikorombwezo kibao,wanasiasa wengi wa upinzani wapo kwenye siasa kwa ajiri ya kujinufaisha wao na masilahi yao binafsi au vikundi vyao,hivi kwanini chama kama CUF kinashidwa kuweka umoja wa kitaifa kwa kumuweka au kuweka viongozi wa kitaifa kutoka katika dini nyingine,mwenyekiti au katibu JOSEPH FRENK,au kwanini kama CUF inafanya vizuri Zanzibar wapinzani wasiwe kitu kimoja pale Cuf wanapoibiwa kula zao na kutetea haki na kuiambia CCM jinsi ilivyoiba au kutoa watu kutoka bara kupiga kura zanzibar kila miaka mitano CCM inachukua wanajeshi,polisi,wanausalama kwenda kupiga kura Zanzibar na kuwaamisha wanajeshi,polisi,na wana usalama wapemba kuwaleta bara,mabali na kufanya hivyo matokeo ni CCM inashinda kwa asilimia 0.5-10%lakini kwasababu tatizo la ubinasfi ,ukabila ,uzushi tunashidwa kusimama na kusema CUF wameonewa .Na inakuaje chama kiwe na viongozi wa juu wote kutoka kabira moja,au kanda moja kaskazini au kusini ,kwanini kusiwe na chama chenye umoja wa kitaifa.
3-Uwezo mdogo wa utawala katika upinzani,kuna wakati kama unawasikiliza viongozi wa upinzani wengi wao hawana sifa yoyote,hawana vipaji vya kuongoza,hakuna mikakati yoyote,matokeo yake vyama vimejichimbia mijini na viofisi vyao kuwepo mijini tu.

SULUHISHO:

Upinzani wa kweli utakuja hivi karibuni kutoka kwa vijana ambao watanzaisha chama cha kitaifa ambacho kitaundwa na vijana kutoka kila kona ya maisha ambao awajawahi kuwa na uongozi au uwanachama wa vyama vya sasa vya upinzani au CCM na kitakuwa na mvuto mkubwa sana mwenyekiti wetu atakuwa msomi kutoka chuo chochote kile ,makamu wa mwenyekiti atakuwa mdada mmoja mwenye kujua issu,na katibu wetu atakua katokea Zanzibar,na katibu msaidizi atakuwa mtanzania mwenye upeo kutoka chama kimoja chochote,na wajumbe watano watano kutoka kila mkoa,wajumbe wawili kutoka kila wilaya.na kampeni zitaanzia shule za secondari ,kupitia vyuoni na kuelekea kila kijiji mtindo kama wa obama ,hii itakuwa kama movoment fulani na CCM wanamiaka kama 10 .oh pengine ni ndoto lakini huu ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom