Makosa ya kuepuka uwapo katika usaili

Aug 17, 2016
73
39
- Kutokuwa nadhifu; kuingia kwenye usaili ukiwa na nywele chafu na zenye muonekano mbaya hukuletea picha mbaya kwa wasaili.

-Nywele za rangi rangi: dada zetu nywele zenye rangi rangi za ajabu au zilizo na mwonekano usio nadhifu zitakugharimu. Hivyo kuwa makini.

-Kutokujali mavazi; mavazi yako yasifanane na mtu anayekwenda kwenye harusi ama ufukweni,Bali vaa vizuri, nguo zitakazotunza heshima na kukupa muonekano mzuri. -Mkao; nazungumzia jinsi ya kuketi kaavyema usiketi kama mtu aliyepoteza uwezo wa kuketi kitini.Pia ukumbuke kumwangalia msaili wako usoni na sio kukwepesha macho kama hujui unachokitafuta.

-Simu ya mkononi; simu zinapaswa kuwa zimezimwa weka katika mkoba ama mfukoni.

-Kuna wale wanajifanya wajuaji, wanaojikweza;sio vizuri kujionyesha kwa wasaili wewe ni mtu wa namna gani.

-Kutafuna big G,peremende,pipi, na vinavyofanana na hivyo wakati wa usaili; nikosa kubwa sana, na kwa wale wavutaji wa sigara Epuka kuvuta kabla ya kuingia kwenye usaili, si kila mtu ataweza kuvumilia harufu ya nicotine.

-Swali kwa mwajiri; mwishoni mwa usaili waajiri hukuuliza "Je unaswali kwetu?" Ukiwa huna swali si vibaya ila utapunguziwa maksi..ukiwa nalo kuwa makini sana na utakachouliza huenda kikakupatia kazi ama kukukosesha...

CVPEOPLE AFRICA TANZANIA NI WAKALA NAMBARI MOJA WA AJIRA AFRICA NZIMA. IKIWA NA UMRI ZAIDI YA MIAKA ISHIRINI. NI WAKATI WAKO SASA KUJISAJILI NASI BURE KUPITIA TOVUTI YETU .

NA KUWEZA KUCHAGUA AJIRA UIPENDAYO. CVPEOPLE AFRICA HAITOZI JOBSEEKER GHARAMA YOYOTE. EPUKA MATAPELI.
 
Back
Top Bottom