Makosa makubwa kutengua matokeo ya Ubunge kwa ushahidi wa kusikia-Jaji Moses

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia bila kutoa vielelezo dhahiri vunavyoonyesha tukio husika.

Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.

Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.

Source:Mwananchi Jumamosi
 
Mmh asante kwa somo zuri, nafikiri ni somo zuri pia kwa jaji aliyetengua ubunge wa Mh. Lema Arusha manake kule hakukua na ushahidi ulio wazi wala vielelezo visivyotia shaka.
 
Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia.Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.
Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.

Source:Mwananchi Jumamosi

... Kwa mtazamo huu, natumai kipenzi cha wana -A-town atarudi mjengoni soon...
 
Hivi majaji km huyu wanafika 10 tz?.....ingekuwa hivyo basi ccm ingenyooka na isingesubiri rungu la mahakama kuiadhibu cdm.......mungu mkubwa kwenye msafara wa mamba na kenge wamo pia
 
Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia.Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.
Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.

Source:Mwananchi Jumamosi
Nani ana email address ya jaji alie hukumu kesi ya Lema nimtumie maneno haya....
 
Huo ndio ukweli nilishangaa sana pale jaji alipohukumu kesi kwa ushahidi wa kusikia halafu anaukubali. Hongera jaji kwa kufuata principles bila woga wala biases.
 
fi sana jaji ubarikie kwa kuonyesha msimamo wako na taaluma yako inavyopaswa kuheshimiwa kwa maamzi magumu
 
Judge ana rule kesi kwa dakika tano na kutokomea???

Na ushahidi wenyewe wa kuambiwa na wajinga wawili wa magamba???

Hongera Judge umezungumza mambo ya msingi sana kisheria na bila ushabiki...

CDM, reload TL kwenye rufani ya Lema!!
 
Ujaji si vyeti, madaraka na mahakama tu, bali ni hekima ya kumuogopa Mungu. Mwishowe haki itaonekana imetendeka mbele ya jamii kutokana na hukumu.
 
Mara baada ya CHADEMA kukamata dola mwaka 2015, Jaji Moses asisahaulike.Kwa vile ametenda kinyume kabisa na kile ambacho watawala wachovu walitamani kiwe itafaa ikiwa atapewe nafasi inayoendana na uwezo wake..siijui kwa sasa.. ila iwe kati ya nafasi za juu kabisa zinazohitaji weledi wa kisheria.
 
Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia.Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.
Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.

Source:Mwananchi Jumamosi
Ni wachache wenye kuweza kufafanua na kupangua hoja kitaalamu kama huyu jaji alivyofanya kwenye hukumu ya kesi. Sishabikii lakini alivyokuwa anazipangua zile hoja kwa mantiki bila shaka kila mtu aliondoka pale ameridhika.
 
mimi ni mchadema lakini namshukuru jaji wa kesi ya lema coz m4c imezidi kushika kasi..by the way lema mjengoni kurudi ni lazima..
 
Back
Top Bottom