Makosa kumi kabla wakati na baada ya kususia bunge maalum la katiba.......!!!!

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
images2.jpg
Ndugu zangu Watanzania popote msomapo Makala haya: Wiki iliyopita katika makala yangu nilizungumzia Uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) hata bila ya kuwa na hati za awali za makubaliano ya muungano. Hoja yangu niliijenga katika misingi kwamba, Muungano wetu una misingi ya kindugu na kitamaduni zaidi kuliko vile ambavyo ungedhaniwa kuwa ulijikita katika sheria, uchumi na siasa. Mahusiano ya miaka mingi na mapitio ya historia ya mapambano ya uhuru hadi Mapinduzi, yalibeba sura nzima ya kutaka maunganiko kati ya Jamhuri hizi mbili. Katika Makala yale nilizungumzia hata mahusiano mabaya yaliyokuwepo kati ya waafrika walio wengi kule Unguja na Pemba na mahusiano ya waafrika hawa na wenzao wa Tanganyika.

Wakati Bunge maalum la Katiba likiendelea na mchakato wake wa majadiliano kwa ajili ya ama kukubaliana na Rasimu ya Katiba, ama Kuiboresha ama kuibadilisha na kuja na mapendekezo mapya, kumeibuka malalamiko miongoni mwa wajumbe wa bunge hilo ambao wameamua kujigawa katika makundi kujaribu kuelezea hisia zao. Haya yametokea kwa sababu nyingi, lakini chache ni ama kutaka kufanya ni eneo la siasa za kiuchaguzi, ama kuiga mahali kwengine, ama kutaka kuvuruga tu Mchakato kwa makusudi ama kutokuwa na maandalizi ya kutosha. Ya maandalizi inaweza kuwa nzito maana kukusanya watu wenye hulka tofauti (wanasiasa na wasio wanasiasa) kwa pamoja na kuwaambia sasa fanyeni utaratibu muandike rasimu, ni sawa na hapa Tanzania Uvichukue Vilabu vya SIMBA na YANGA kisha uwaambie waunde Katiba ya TFF. Hilo halitakaa litokee.

Katikati ya wiki Jumatano iliyopita tarehe 15/4/2014 wakati bunge likiwa katika kikao chake cha mchana kuna jambo la ajabu kidogo lilitokea. Nasema la ajabu kwa sababu halikutakiwa kutokewa, lakini kidogo kwa sababu lilitarajiwa hata lisingetokea wiki iliyopita lingetokea tu. Wajumbe ambao wanajipambanua kuwa ni wa vyama vya Upinzani wakiongozwa na CUF na CHADEMA waliamua kutoka nje. Lakini kutoka kwao hakukuwa jambo baya sana, ubaya ni Pale ambapo sababu ya kutaka kutoka na kuamua hivyo ni Ubaguzi kama alivyosema mwenyewe muwasilisha hoja Prof. Ibrahim Lipumba. lakini Lugha aliyotumia ni ya Ubaguzi wa hali ya Juu na kuwalinganisha wale walioamua kubaki na kundi Halifu la Kivita la INTALAHMWE. Hili lilikuwa neno gumu la mwisho ambalo Profesa Msomi wa kariba yake na mwanasiasa mkongwe Ibrahim H. Lipumba angeweza kulitumia.

Huko kutoka na namna ya walivyotoka na tangazo la kutoka lilivyowekwa, lilitengeneza kosa ambalo kwa mchanganuo wangu mchakato mzima ulikamilishwa na makosa kumi ya msingi ambayo kuna maswali watanzania wanatakiwa wajiulize kwa undani ili kuleta hali ya utulivu na maridhiano kuelekea kutengeneza katiba mpya.

1. Kosa la Kwanza. Kumtukana Mwalimu Nyerere na Kudhihaki Muungano.
Kila Raia wa Dunia hii anajua vema Mchango wa Mwalimu Nyerere katika Ukombozi wa Bara la Afrika na Ukombozi wa Mwanadamu. Njia kuu ya kumkomboa mwanadamu aliyotumia ni Umoja. Na kwa falsafa hiyo alienda mbali na kwa ushirika mzuri wa Sheikh Abeid Amani Karume waliunda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa kutumia nguvu nyingi, Tundu Lisu amefanya kushawishi bunge na wananchi kuonyesha kuwa Mwalimu alikuwa Mlaghai na kwamba Muungano huu si halali. Huu ni WENDAWAZIMU. Je, Wanataka kutueleza kuwa watoto wetu na vizazi vijavyo wasifundishwe jambo lolote kuhusu Mwalimu Nyerere na Karume? Ama Kuna chuki gani wanaisambaza dhidi ya Mwalimu?

2. Kosa la Pili. Kuanzisha Kundi Haramu ndani ay Bunge.
Ninaliita kundi Haramu kwa sababu lina sura ya Ubaguzi na Unafiki ndani yake. Wapinzani wa Muungano unaoongozwa na CUF na CHADEMA uliamua kuanzisha kundi la UKAWA (Umoja wa Ktaiba ya Wananchi). Swali la kujiuliza kama hili kundi ni halali, Je linawakilisha wananchi Gani ambao hawawakilishwi na wengine? Au Je hao ambao hawamo katika kundi lao, wanamuwakilisha nani ikiwa hawapo kwa ajili ya wananchi?

3. Kosa la Tatu. Kujaribu kuhodhi Mjadala wa Katiba.
Hili ni kosa jingine lililofanywa na wajumbe hawa. Mjumbe ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri Mwigulu Nchemba alizungumzia kuhusu dhana ya "Give and Take". Lakini akatahadharisha kwamba wao "UKAWA" wanataka "Kutake" tu bila "Kugive". Hii ni kujipambanua kuwa wao walikuwa ndio wenye Mjadala kuliko wengine. Swali la kujiuliza, Je ni jambo gani wao wanaridhia kulipoteza ili kujenga mustakabali wa kupata katiba?

4. Kosa la Nne. Kuzuia kujadili Mantiki ya Rasimu ya Katiba kama kwamba hiyo rasimu ndiyo Katiba yenyewe.
Ndugu zetu hawa wamejaribu kwa nguvu zote hata kuleta lugha ya utata kwa kujaribu kuwazuia wajumbe wasijadili uhalisia wa rasimu kama tayari tuna katiba. Si haki hata kidogo kwa kuwa, rasimu inatakiwa ijadiliwe, iboreshwe, na ikiwezekana ikataliwe. Na kwa mamlaka ya Bunge hili, linaweza hata kuikataa na kuanzisha rasimu mpya. Ikiwa Wenzetu hawa walitaka Rasimu ndiyo iwe document ya mwisho ya katiba ilikuwaje wakubali kuingia bungeni kwa ajili ya majdiliano? Ilikuwaje wakubaliane na Kanuni ambazo kwa kiwango kikubwa ziliwapendelea wao?

5. Kosa la Tano. Kupotosha Umma kuhusu Hotuba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wa kundi Haramu la UKAWA wote ni wajumbe wa Bunge maalum la Katiba. Mapema kabisa baada ya Rais kuhutubia Bunge waliibuka kesho yake kuwa Hotuba ya Rais haiko sawa. Kulikuwa na taarifa kwamba walitaka wagomee Rais asihutubie Bunge. Upotoshaji wao upo katika minajili kwamba Rais alikuja na Rasimu Mpya. ikiwa walikataa ile hotuba ya Rais, Je wao walitaka aseme nini? Na hicho walichotaka Rais aseme kinaleta tofauti gani kutoka kile walichosikia?

6. Kosa la Sita. Kuleta kauli za Kejeli.
Hili limedhihirika kwa kauli kedekede "Vijembe" dhidi ya Rais na na viongozi wa serikali waliopo madarakani. Katika matamshi yake, Mh. Mbatia alijaribu kudanganya umma kwamba takwimu alizotumia Rais ni tofauti na zile alizotumia Rais na ni tofauti na zile za Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Ukipitia katika moja ya maandiko yangu katika mitandao ya jamii facebook.com na jamiiforums.com utakutana na ufafanuzi niliotoa wa takwimu zilizotumika na hadi kurasa zinakopatikana. Ikiwa hata takwimu zilizoandikwa kwa usahihi kabisa na kusomwa kwa usahihi kabisa zinaweza kubadilishwa. Je kuna lipi ambalo hawa waheshimiwa wanaweza kuaminiwa kwalo?

7. Kosa la Saba. Kashfa dhidi ya Muungano.
Linaloshabihiana na Kosa la Kwanza. Amesikika Tundu Lisu si mara moja, kuanzia alipopewa nafasi ya kufafanua mawaidha ya wachache kutoka katika kamati yake. Uhojaji wa Muungano, Mchakato wa Muungano miaka 50 zamani na hata kukdiriki kusema muungano si halali ni vitendo vya kihuni visivyoweza kuvumilika. Ni kauli ambazo zinasadifu maneno ya Mh. Mwigulu Nchemba kwamba "Wamevimbiwa Demokrasia". Ieleweke wazi, demokrasia isiyo na Sitaha haina maana. Ikiwa hawa wote tangu hata huu mchakato wa Ktaiba wameanzisha vyama, wamejiunga katika vyama na wamefanya kazi za siasa kwa vyama vilivyosajiliwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Je wanawezaje leo kusema Muungano si halali?

8. Kosa la Nane. Dhahiri ya wao kutoutaka Muungano.
Ni kama Kauli zinazotolewa kwamba CHADEMA wanaionea Huruma Zanzibar, na CUF wanaionea huruma Tanganyika huku NCCR Mageuzi wakisimama kama viranja vya Bwana huruma hawa wawili. Maneno ya Mh. Jusa Ismail Ladhu, na Mh. Juma Duni Haji yanalingana kwa tafsiri na yale ya Mh. Vincent Nyerere, Mh. Mkosamali na Mh. Moses Machali ambao wanaona uendelea kuwa na huu muungano basi upande mmoja wa muungano unaumia na unaumizwa na mfumo uliopo. Lakini katika hili kuna Ubaguzi mkubwa unaosimamiwa na kauli hizi kati ya wazanzibari wa Unguja na wale wa Pemba. Hapo ndipo wapata uhalisia wa Kauli ya Mwalimu, kwamba "Nje ya Muungano hakuna Zanzibar, nje ya Muungano kuna Unguja na kuna Pemba. Nje ya Muungano hakuna Wazanzibari, Nje ya Muungano kuna Wazanzibari na Wazanzibara" Tumeshayashuhudia haya humo Bungeni. Ikiwa kweli hawautaki Muungano, kwa nini basi wasingegomea kuanza mwanzo kwamba hawahudhurii Bunge kwa kuwa Muungano si sehemu ya Itikadi zao?
index.jpg

9. Kosa la Tisa. Mikakati kuzuia utendaji wa Bunge la Katiba.
Miongozo, kanuni na Taarifa imekuwa ni njia ya kujaribu kuzuia bunge lisifanye kazi yake. Wakati wa Marekebisho ya Kanuni namba 32(b)(d) ili kuwezesha kamati zile ziendelee na kazi bila kikwanzo cha uhitaji wa 2/3 ya wajumbe wote wa kamati badala yake iwe 2/3 ya wajumbe waliohudhuria, alisimama Mh. John Mnyika na kutumia nguvu nyingi kujaribu kujenga hoja hilo lisikubalike. Hapa nimpe haki yake Mh. Mkosamali ndiye aliokoa Jahazi Pamoja na Mimi paul makonda. Watuambie, Kwa nini wamekuwa wanahujumu Mchakato wa Bunge la Katiba?

10. Kosa la Kumi. Kuacha Bunge kwa mashinikizo.
Hali wakijua wazi kuwa hilo si kosa tu kisheria na kanuni za Bunge maalum lakini pia ni kosa la kimaadili wajumbe hawa WAKAWA wameamua kususia Bunge na kwenda kukaa Hotelini walikolipiwa kwa kodi halali za wananchi wanaowawakilisha na kuwaachia wale wasiowakilisha wananchi waendelee kujadili. Haya ni Maajabu, kwamba wewe unayewakilisha wananchi, unatoka nje unamwacha yule unayesema hawakilishi wananchi aendelee kujadili ya wananchi. Huu ni UKICHAA uliokomaa. Ikiwa Nyie ni Wawakilishi wa Wananchi (Lakini kuna wateule wa Rais), Na Ikwa Mjadala unaendelea, Na ikiwa kwa kuendelea na Mjadala mwisho wa siku tutatengeneza Rasimu, Je Nyie huko nje mnawakilishaje wananchi? Je Mikutano ya Hadhara kama mlivyoamua, inawezesha kutengeneza Katiba? Tafakarini!
images.jpg

Mwisho, Wananchi ndio mtahukumu. Na ninajua mtahukumu kwa haki.Na kwa yeyote mwenye mapenzi mema na nchi hii talaani vikali uhuni wa waheshimiwa hawa. Kwa mwingine ataona ni sawa tu. Usiwe miongoni mwao.

Katiba tunayotengeneza nai kwa ajili ya watanzania wote si kundi dogo la watu wenye mwavuli wa vyama vya siasa. Watanzania subirini muone rasimu itakayotoka katika bunge hili. Hamutalazimishwa kuikataa ama kuikubali bali mtashawishiwa kuamua hatma ya taifa. Msimamo wangu, Tuendelee na Mfumo wa Nchi Mbili zilizoungana na Kutengeneza Jamhuri Moja iliyoamua kukaa katika mfumo wa dola ya Serikali mbili yaani ile ya Tanzania Bara na ile ya Zanzibar. Ifahamike wazi, kwa sasa kwa namna yoyote kuendelea kudai Tanganyika ni uendawazimu maana hiyo tanganyika haipo duniani tangu 1964. Ili tusonge mbele, tutumie machinery ya serikali iliyopo kutatua migogoro michache iliyopo na tujenge taifa letu. Tukumbuke Uchumi wetu bado ni mdogo na kuendelea kuiweka nchi yetu katika kundi la mataifa maskini kabisa duniani. Hatuna sababu ya kuanza serikali mpya badala yake tutumie serikali zilizopo kusuluhisha migogoro iliyopo kwa maendeleo ya watu wetu.

Asante kwa kusoma na kunielewa


Mungu Ibariki Tanzania


Paul C. Makonda
Mjumbe - Bunge Maalum la Katiba
makondapaul@gmail.com
0716 6962 65
 

As much as I know you Makonda, sitashangaa nikisikia kuwa hata hii makala umeandikiwa.

Hakuna press release yako hata moja, achilia makala ya namna hii, uliwahi kuandika mwenyewe. Tangu ulipokubali kutumwa tumwa wakati ule tunakutana kwenye press pale Grand Villa, hujawahi kuwa na independent mind, tangu walipokufanya kuwa 'right hand person' not necessary trusted. Unajua kuwa ulikuwa unasema vitu vingi off records.

Mtu anayekufahamu vizuri anapaswa kukusamehe tu na kukuonea pole kwa sababu hujui unachokifanya...may be with time utaelewa wajibu wako kama kijana.

Kwa sababu ninakujua vizuri, sina haja hata ya kwenda in detail kulichambua andiko lako ambalo limeficha 'devils' wengi tu.

Haya. Timiza wajibu wako kama kijana wa CCM anyway.

 
nimekuwa nikisema unatumika vibaya na leo umedhihirisha hilo.hivi ww unawakilisha kundi gani kama sio mteule wa rais?vyuo vikuu hawakutambui ulimaliza kitambo sijui utatudanganyaje
 
Safi sana .wanawashwa watakuja tu.na matusi maso.sababu hawana hoja.ndo.mana wamekimbia mjadala.bungeni ..ukawa wahaini wanafuruga nchi........
 
Nimejaribu kusoma na kuelewa vizuri maandiko yako lakini bado naona sababu zako kumi zimekosa mashiko.Sababu zako hazina athari yeyote ile, kama mtu alikuwa anaamini kwenye serikali tatu(ukawa) na kama mtu alikuwa anaamini serikali mbili(ccm & co) basi ataendelea kuamini hivyo hivyo, hakuna hoja ya msingi uliyosema.
 

As much as I know you Makonda, sitashangaa nikisikia kuwa hata hii makala umeandikiwa.

Hakuna press release yako hata moja, achilia makala ya namna hii, uliwahi kuandika mwenyewe. Tangu ulipokubali kutumwa tumwa wakati ule tunakutana kwenye press pale Grand Villa, hujawahi kuwa na independent mind, tangu walipokufanya kuwa 'right hand person' not necessary trusted. Unajua kuwa ulikuwa unasema vitu vingi off records.

Mtu anayekufahamu vizuri anapaswa kukusamehe tu na kukuonea pole kwa sababu hujui unachokifanya...may be with time utaelewa wajibu wako kama kijana.

Kwa sababu ninakujua vizuri, sina haja hata ya kwenda in detail kulichambua andiko lako ambalo limeficha 'devils' wengi tu.

Haya. Timiza wajibu wako kama kijana wa CCM anyway.


Udhaifu mkubwa badala ya kujibu hoja unakuja na person attack? bora ungepiga kimya.Mbona wewe unapokua speaker ya Dr watu hawasemi.leo ni nimeona akili yako ilivyo bila Dr.
 
kinachoniumiza ni kwamba hawa wasaka tonge wa ccm wanafikiri watanzania hatuna akili, wao ndo wana akili tu! Makonda nenda kawaambie waliokutuma, kwamba kule site kuna watu wenye akili sana na wachambuzi wazuri ila hawana mpango wa kuja kupiga kelele huko kwa vile wanakimbizana na chapaa katika nchi hii muliyoiuza. Sioni anayeweza kujadili hapo ccm! period!
 
Mengi ya hayo ayaitayo makosa hayamo katika ile dhati ya makosa kwa msingi wa makosa! Na kwa makusudi amejitoa ufahamu, angekuwa FAIR hata ile mipasho mingi hasa kutoka CCM ingekuwa ndani ya orodha hiyo! Orodha iko biased!
 
Usitupe masharti endelea na bunge na genge lenu la intarehamwe! Tunawasubiri kura ya maoni. Mmepeleka lukuvi kanisani kutafuta kuungwa mkono! Mpelekeni na wasira msikitini. Wananchi tunataka maendeleo hata hiyo katiba mlioichakachua hatuitaki.bakini nayo dodoma. Umeamua kukimbilia jf kwani hapa ni ofisi ya ukawa?wafuate ukawaambie ukawa!!
 
Makonda wew ndo usiongee chochote kwanza unajenga hoja dhaifu sana msijifanye sa hivi mnakuja tafuta sympathy huku wakati ccm ndo watekaji wakubwa wa mchakato mzima wa katiba mmekaa mnang'ang'ania eti serikali tatu zitavunja muungano acheni unafiki ni ukwel usipingika ccm ni INTALAHMWE, na acha kutumika vibaya njaa zitawaponza
 
Safi sana .wanawashwa watakuja tu.na matusi maso.sababu hawana hoja.ndo.mana wamekimbia mjadala.bungeni ..ukawa wahaini wanafuruga nchi........

Katiba ya kiCCM CCM lazima ipingwe!
Nawapa hongera wajumbe na wabunge wa bmk wasioshobokea laki tatu tatu za kipuuzi!
Karma lazima ifanye kazi yake!
 
CCM na wajumbe wake ni MALAIKA hujazungumzia mapungufu yao(ubaguzi kama vile chama hicho hakina wenye asili ya Asia,kuzomea kimkakati,kumdhihaki Warioba,ku discuss Rasimu yenu ya ccm na hotuba ya rais)
 
Mnaokataa misingi yenu ni kubomoa , alichoongea makonzda ni sahii awe ameandikiwa ama amesema yeye ujumbe umeingia ndani ya vidonda vya wahaini wa muungano, kazi mnayo na tunawasubiri mtaani mje mtuongopee kama kawaida yenu.
 

As much as I know you Makonda, sitashangaa nikisikia kuwa hata hii makala umeandikiwa.

Hakuna press release yako hata moja, achilia makala ya namna hii, uliwahi kuandika mwenyewe. Tangu ulipokubali kutumwa tumwa wakati ule tunakutana kwenye press pale Grand Villa, hujawahi kuwa na independent mind, tangu walipokufanya kuwa 'right hand person' not necessary trusted. Unajua kuwa ulikuwa unasema vitu vingi off records.

Mtu anayekufahamu vizuri anapaswa kukusamehe tu na kukuonea pole kwa sababu hujui unachokifanya...may be with time utaelewa wajibu wako kama kijana.

Kwa sababu ninakujua vizuri, sina haja hata ya kwenda in detail kulichambua andiko lako ambalo limeficha 'devils' wengi tu.

Haya. Timiza wajibu wako kama kijana wa CCM anyway.

Ningeshangaa kama makene ungemwelewa na kumpongeza makonda kwa kile alichokiandika kwa kuwa wewe mwenyewe uelewa wako hata vijana wa bavicha wengi sana wanakuzidi.

Lakini pia kwa mda mrefu umekuwa ukiongozwa na hisia na ushabiki kuliko ukweli wa mambo.

Lakini pia nyie ndiyo mliochangia kuuwa chadema kwa kumshauri vibaya mzee slaa na kutoa uamuzi mbay ambao umeua chama.
 
Mnaokataa misingi yenu ni kubomoa , alichoongea makonzda ni sahii awe ameandikiwa ama amesema yeye ujumbe umeingia ndani ya vidonda vya wahaini wa muungano, kazi mnayo na tunawasubiri mtaani mje mtuongopee kama kawaida yenu.
Kweli kabisa mkuu tatizo la watu wengi kutoka bavicha ni kule kudhani kuwa wao wako sahihi sana kumbe some time hufanya vituko vingi kweli uwezo wao wa kuchambua mambo ni bure kabisa.
 
Elimu ya mjinga ni majungu (Banza Stone, miaka ya 2000). Nilitegemea kuona makala yenye hoja makini lakini nimepitia maandishi yote na kukuta hakuna hoja kwenye makala hiyo zaidi ya propaganda za kutaka huruma kwa wananchi. Jipange kijana bado sana.
 
Back
Top Bottom