Makongoro Nyerere yuko wapi? Mbona hatumsikii akitetea uadilifu wa baba yake?

Bweru

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
213
49
Kwa muda mrefu nimekuwa simsikii Makorgoro Nyerere akisema lolote juu ya Serikali ya chama chake -ccm - kubomoa misingi ya utu na uadilifu aliyoiweka baba yake Mwl. Nyerere. Mbona baadhi ya wana-ccm wenzake, angalau wanajitutumua kulalamikia baadhi ya mambo yanayoenda mrama nchini?

Ndiyo tuseme amelishwa limbwata la Mafisadi wa Chama cha Magamba kiasi kuwa hawezi kusema lolote juu ya mateso ya wananchi ndani ya utajiri wa nchi yao?

Je, anaogopa kuutema uenyekiti wa Magamba Mkoa wa Mara.

Wenye kufahamu lolote wanifahamishe.
 
"Je, anaogopa kuutema uenyekiti wa Magamba Mkoa wa Mara." Kumbe unajua aliko sasa unauliza nini yarabi!!!

macinkus
 
Kwa hili Bweru unakosea! Uadilifu wa baba wa Taifa asiyeweza kuutetea, na anayeweza kuubeza katika Nchi hii ni punguani tu, ambaye hazimtoshi. Suala hilo sio la kusuburiwa hadi Makongoro aseme kitu. Dunia nzima inafahamu Kuwa Mwl. Nyerere alikuwa mwadilifu, na alijengea Nchi yetu imara. Misingi ambayo sasa inabomolewa taratibu na mafisadi na walafi.

Kulipigia kelele suala hilo ni jukumu la watanzania wote wanaoitakia mema Nchi yetu.

Tatizo letu kubwa ni woga ambao unatufanya katika mambo ya msingi kuogopa kuweka msimamo wetu.

Jambo lingine watanzania tusahau haraka. Ebu angalia sakata la posho ya wabunge, kila mmoja kwa sasa linamgusa, analizungumzia, lakini litasahaulika muda sio mrefu, na tutarukia jambo lingine, wabunge kwa ubinafsi wao, na kwa kuongozwa kwao na spika asiye na uwezo na kiti hicho wataendelea kuchukua posho, hata kama itabidi wananchi katika majimbo yao wanakufa njaa.

Hili sio suala la kupigiwa kelele na Makongoro ni lako na letu sote.
 
Kachasu amuachie nani??hana jipya yule alishapoteza muelekeo longtime......ulevi nomaaaa...
 
Kwani ni lazima aseme?
This time na wewe ongea tukusikie kuliko kumsubiri yeye....
 
Unataka kutoa '' Ilmu" gani mpya jemedari?

Unajua mkuu sisi wote ni watoto wa mtu fulani kibailojia, utaalamu na mafundisho

Kwa mfano ni rahisi sana kusema Sokione alikuwa mtoto wa Nyerere kimafundisho......mafundi mekanika wengi wana watu wanawaita baba zao..kwa kufundishwa ufundi.....hali kadhalika kwenye fani zingine zote..let call them mentors

sometime baba na watoto wake huwa wanatofautiana kwenye beliefs na maamuzi fulani fulani......ndio maana Okonkwo alisema hataki kuwa mvivu kama baba yake mzazi na akawa mfanya kazi hodari

Makongoro angekuwa mtoto wa Nyerere ungemsikia tu....asingejificha......lakini kama Nyerere ni baba wa taifa basi hata yeye ni mtoto wa Nyerere kimafundisho ya uadilifu! ambapo imekuwa proved wanafunzi wengi wa Nyerere wame-end up kuwa corrupt na kujivua sifa ya kuwa watoto wa Nyerere...

hali kadhalika Makongoro anaweza akawa sio mtoto wa Nyerere kimafundisho kwani either alikuwa against na misimamo ya baba yake....kwa hiyo siyo mtotot wa kimapokeo...kama wengi walivyo!

Ukija kwenye kibaiolojia...mtu anayemjua baba yake halisi wa Makongoro ni mama Maria Nyerere! kufanana siyo nongwa...wako watu walioonekana kufanana na baba zao kumbe ni watoto halisi wa 'mdogo wake baba' au shemeji wa mama!


wakatabahu
 
Alishasema na anasema sana katika vikao vya chama bila woga kuwa Lowasa, Chenge na Rostam kule Site hawatakiwi, wanaharibu taswira ya chama na wanatakiwa kutoka

Uzuri yeye halopoki nje ya vikao anafuata maadili na kanuni za chama
 
Tatazo la Makongoro linaeleweka kuwa gongo imemuharibu sana jamaa. Pia Nyerere alikuwa na roho mbaya sana kiasi cha kuwaacha watoto wake bila maisha yanayoeleweka. Hawa watoto wa Nyerere wote walipaswa kuwa mawaziri hasa ukizingatia muda ambao baba yao amekuwa madarakani. Lakini saa hizi wanaishia kupewa vyeo vya ajabu ajabu tu. Nyerere ana roho mbaya yule jamaa.
 
Uadilifu gani aliokuwa nao Nyerere? Makongoro anajua kuwa baba yake alikuwa kimeo ndio maana hawezi kumtetea kwa lolote. Nyie mnayemuona Kifimbo kama mtu mwadilifu endeleeni kuamini hivyo. Yule babu ndiye aliyeweka misingi ya ufisadi tunaouona hivi sasa. Tunabaki kulaumiana tu. Ushahidi mwingi juu ya mabaya ya Kifimbo ushaongelewa humu si zaidi ya mara moja lkn kwa kuwa ss WaTZ ni watu wa kulishwa kasumba hatuambiwi kitu kuhusu huyu babu. Mungu wahurumie WaTZ.
 
Suala la uadilifu wa Mwalimu halihitaji ufafanuzi toka kwa cha P Makongoro, suala ni yeye jee yuko upande gani, wa mafisadi au wapinga ufisadi? Na kwa vile yeye ni mwana CCM hakuna ubishi yeye ndiyo wale wale,yuko pale kuganga njaa yake.CCM ni saratani inayoliangamiza taifa hili, yeyote anayeiunga mkono ni adui wa wana wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom