Makongoro Nyerere: Lowassa nisamehe sana, ila ni Lazima tukuvue gamba haraka!

Hey Jf kumekucha,

Hali si shwari kati ya kapteni Makongoro Nyerere na Edward Lowassa. Taarifa za kina zinaeleza vuta nikuvute hiyo imezidi kupamba moto huku safari hii Makongoro akiamua kuvunja ukimya na kuweka bayana maamuzi yaliyofikiwa na NEC ya kumvua gamba Lowassa ni lazima yafanyike mara moja pasipo kusita.

Taarifa zaidi ambazo tumezinasa kwa njia ya simu kutoka huko Dar es salaam maeneo ya Kinondoni Biafra kutoka kwa mwandishi mmoja wa gazeti la Dira ya Mtanzania zinabainisha kuwa ni Makongoro Nyerere ndiye aliyeanika taarifa za Lowassa kutaka kuyaanika maovu ya Kikwete wiki moja iliyopita na huku wiki hii Makongoro huyohuyo akiibuka na madai mengine mazito kuhusu azma ya Kikwete kuwakingia kifua Lowassa na Chenge ili wasitemwe kwenye kikao kijacho, Makongoro amekaririwa akisema "hata kama kiwete akitaka amlinde huyu lowassa, kweli kaka yangu lowassa atatusamehe ni lazima tumng'oe bila kusita, itabidi tupinge hoja za kikwete kwa maana hana ubavu wa kutulazimisha"

Ha ha ha hawa CCM mwaka huu tutasikia mengi
 
Mimi nauliza ni kosa au jambo gani alilofanya Lowassa ambalo CCM wengine hawakufanya??????????

Good question dear. Yaani mi si mwanasiasa ila nashangaa sana kundi kubwa la watangaza nia wa Chama Tawala wanampiga vita Lowassa! Mi naona sio fair kabisa kujisafisha wewe kwa kumchafua mwenzako, inahuu??... Hata Mungu hapendi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom