Makongoro Nyerere dhidi ya Mapacha watatu (RACHEL)

Kwamza ni aibu aibu kwa hao wakina RACHAEL kusubiri mpaka wapewe barua na Secretarieti, hadhi yao hata kwa wananchi wanao waongoza katika majimbo yao itashuka.
Kuna mmoja kati yao alipata stroke mala baada ya kuukosa u PM, sasa akipata barua itakuwa vp? washauri wao wanawadanganya kwa kupenda vijipesa na ahadi za kupata madaraka hapo watakapo fsnikiwa. Huyo mwingine tunasikia kisha kimbia nchi na amekuwa akiishi huko kusini mwa africa kwa muda sasa.hapa kwetu anaonekana kwa matukio tu, eti kwasababu hamamini Rafiki yake coz anytime anaweza kubadilika.
 
hana lolote naye mlevi tu huyu...


Yupi mlevi kati ya Lowasa, Rostam, Makongoro na Policaprito?
Upo ulevi wa aina nyingi lakini bora, ni heri uwe mlevi wa pombe kuliko ulevi wa madaraka na kujikusanyia mali bila kujali wananchi unaowaongoza
 
- Mkuu sana hakuna anayekataa kwamba Makongoro ni mwananchi na kwa sasa ni mmoja wa viongozi wa ngazi ya chini kitaifa wa CCM, HOWEVER; kuwa mtoto wa Mwalimu haimfanyi kuwa na uwezo flani wa ajabu sana mpaka kumuweka kwenye level ya baba yake kama unavyojaribu kufanya sasa hivi, ni athari sana kwa siasa za taifa kujaribu kumtukuza mwananchi kwa sababu ya uwezo wa uongozi wa baba yake, no! kila mwananchi aonyeshe uwezo wake binafsi wa uongozi!

- Sikubaliani na wale wanaojaribu kumkandia kuhusu maisha yake binafsi, hapana lakini at the same token siamini kwamba kwa sababu yeye ni mtoto wa Mwalimu, basi ana uwezo flani wa ajabu wa kumfanya kuwa na nguvu flani ndani ya CCM na kuweza kuamua anything for the party, hapana na pia kuyakumbatia mawazo yako kuna hatari sana ya huyu bwana kutumiwa na makundi flani ndani ya siasa zetu katika kupitisha agenda mbovu kwa taifa, Makongoro ni Makongoro, na aheshimiwe kama nafasi yake aliyonayo kiuongozi, lakini ya kumtukuza beyond his position ni hatari sana kwa siasa za taifa, kama Makongoro is that great kama baba yake basi agombee nafasi kubwa za taifa na kuweza kuongoza akiwa kwenye hizo nafasi, haya ndio tunayoyakataa sasa ndani ya CCM na ndio kujivua gambas kwenyewe,

- yaani mbunge anakua na nguvu almost sawa na Rais eti kwa sababu anafahamiana na Rais, au in this case ni mtoto wa Mwalimu, hatuwezi kujivua gambas na this kind of ideas!

- Heshima Yako Sana Mkuu Wangu! ila kujivua gambas sio siasa za kuoneana huruma kwa the expense of wananchi and the nation!

FMeS!

Makongoro uwezo kama kiongozi anao. Lazima atafananishwa na baba yake kwa sababu he has taken the same path. Sasa kama unao uwezo wa baba yake au hana, that is open to debate. Na sidhani kuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa ni kiongozi wa chini katika chama. Sidhani kuwa mjumbe wa NEC ni kuwa kiongozi wa chini katika chama. Huyu, ikumbukwe kuwa ni kiongozi wa kuchaguliwa, na ndio maana kuanzia kule Butiama na hata Dodoma, alikuwa mara kwa mara akimkumbusha Kikwete kuwa yeye naye ni mwenyekiti, lakini yeye yuko "site". Waliokuwa ndani ya mkutano huo wa Dodoma, walisema kilichowashtua wengi ni kuwa wanajua Makongoro hakutumwa na mtu yeyote, na mengi aliyosema wengi walikuwa wanataka kuyasema lakini walikuwa hawana ubavu. Sasa, huo ni ujasiri, ambao Johnson Mbwambo kwenye makala yake alisema unaweza kummaliza ndani ya chama, au kumjenga sana. Huo ndio uwezo unaongelewa hapa. Makongoro aligombea na kushinda ubunge, jimbo la Arusha mjini kwa kupitia NCCR Mageuzi, wakati baba yake yuko hai. Na ni baba yake huyo huyo alimwambia kuwa CCM hawatapitisha jina lake, akitaka kugombea ubunge kupitia CCM.
 
Shida moja aliyonayo Makongoro ni kumtegemea kwa kila kitu Mh Nimrod Mkono. Hata hiyo nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kafadhiliwa na huyu jamaa ambaye naye hatazimiki vizuri kwa wengi. Na hii sio shida ya Makongoro peke yake. Kwa CCM ya sasa mtu safi kabisa hawezi tena kuwa kiongozi.


Acheni hizo ...makongoro na wenzake sio watu wa kuabudu pesa kama kina Rizwan na CADET .......wanaweza kuwa na udhaifu wao..lakini kunyenyekea wenye pesa sio moja yao...kunyenyekea inahusisha kukubali pesa ichezeshe kichwa chako....,sasa kama ukiona mtu anaenda kwenye karamu ya mtu ina maana ndio amenyenyekea..Lini huyo makongoro ametetea tabia za Mkono???....nadhani anayo mawazo huru..na amemudu kusimama yeye mwenyewe bila kutegemea sana umaarufu wa babake tangu NCCR.....
Huyo mkono mnayesema hawezi kuacha kuwa karibu na familia ya mwalimu kwa sababu ni distant causin....lakini jiulizeni kwanini Mkono wakati wa utawala wa mwalimu amepata kuhama nchi kwa muda akaishi UK.....inaonyesha kuwa alikemewa!!
 
Ukweli kuwa kwa sasa kuna msuguano ndani ya ccm kati ya viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu ufisadi ...

Ni hatua muhimu ambayo haiwezi kuupuuzimwa... !
Lazima patokee chochote cha maana kutokona na kinachoendelea ccm kwa sasa tofauti na kama msuguanao usingekuwapo!!
 
Jasusi Butiama mkulu alikuwa occupied sana na muafaka wa Zanzibar, lakini there is one thing he did kule bila makelele wala watu wengi ku-notice, alimuondoa Rostam kwenye uweka hazina wa CCM bila kumfahamisha mapema, tayari alishaweka msingi kuanzia pale, inasadikwia since then jamaa hajawahi kuwa na access naye tena!, it is just politics, alikuwa anasubiri the right time awatose na sasa sio siri anawatosa, sasa hivi utasikia Rostam amekimbia nchi! Watch!

- Nildokezewa hii na mkuu mmoja aliyekua amekaa next to Rostam, anasema jamaa alihaha haijawahi kutokea, kwa kutoamini, muungwana is very good at political games, hakuna mtu yoyote wa kuwatoa wale mapacha isipokuwa ni yeye tu, sasa tizama alivyoifanya ionekane ni Makongoro!, kama alivyoifanya kule ionekane ni Mwakyembe, sasa uliza aliyemrudisha ubunge Mwakyembe ni nani? Ndio utaelewa hizi siasa za taifa sio mchezo!

- Kosa kubwa walilokosea mafisadi na they are paying for na kuelekea mwisho wao, ni pale waalipomtoa six kwenye U-Spika kwa kuwatumia Wa-Zanzibari, ndipo walipoanza kujipigilia misumari ya mwishoni kwenye jeneza lao, I mean understand hizi National politiics lini umewahi kuwasikia Wapinzani wakiwalalamikia hawa mapacha? au Mkapa? WHY?

FMEs!
mkuu nambie kwann wapinzam hawapig kelele kuhusu

NO.

Sioni mchezo, bali ni nguvu ya umma tu behind mtikisiko uliokikumba chama cha magamba-ccm.
Nguvu ya umma iliyokuwa nyuma ya SIX haingemruhusu JK kumtosa .Nguvu ya umma iliyokuwa nyuma ya Mwakyembe haingemruhusu JK kumtosa.Hii ina maana kwamba kuondoka kwa Six na Mwakyembe kungekibomoa haraka ccm kuliko hata wakina RACHEL kukibomoa chama.
JK alitikiswa na nguvu ya umma iliyokuwa nyuma ya watu hawa si vinginevyo.UONGO, UONGO.
Hata sasa kina RACHEL wanafukuzwa na hofu ya nguvu ya umma inayotishia kukitosa ccm,BASI.Analysis yako si ya kweli kwa maana ina lengo kuficha udhaifu wa JK kiuongozi. Usimpe hadhi asiyostahili.Huyu hajengeki ni tatizo kwa ccm na nchi nzima. Kumbuka wakati wa uongozi uliotukuka wa ccm, makundi yalikuwa ni dhambi kubwa.Huyu JK, ndiyo kaanzisha uongozi wa makundi ndani ya ccm, na sasa, ccm inalipa gharama kubwa, uongozi wake umekipasua chama makundi makundi.
Inawezekana wewe ni mmoja wapo walioshindwa kumshauri vema JK hadi kukifikisha chama hapo kilipo,kiko HOI.Sasa mnajaribu kumjenga kwa kumpachika personality asiyo nayo. After all makundi siyo sifa nzuri kwa kiongozi yoyote. The divide and rule unayoisema haisaidii taifa changa kama Tanzania bali inasababisha matatizo mengi kama, ukabila, udini, ukanda mambo ambayo yameinuka wakati huu wa kipindi cha utawala wa JK. Pole sana kwa hiyo PR job uliyopewa, angalia njia nyingine ya kumjenga na sio UBINGWA WA KUGAWA WATU KIMAKUNDI. Hapana.
Hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiii.
Bwana mdogo unataka wapinzani wapige kelele kiasi gani? Tell me matokeo ya kujivua gamba, ingawaje gamba lingine linachipuka, yametokana na nini ? Kama si wapinzani? The list of shame ilitajwa na kina nani au ni Nape ndiye aliyewataja?
Lete topic nyingine tujadili hapa, maana tatizo lako ni kwamba unapewa tu na unaowaita WAKULU,bila kuichambua vizuri.
 
Acheni hizo ...makongoro na wenzake sio watu wa kuabudu pesa kama kina Rizwan na CADET .......wanaweza kuwa na udhaifu wao..lakini kunyenyekea wenye pesa sio moja yao...kunyenyekea inahusisha kukubali pesa ichezeshe kichwa chako....,sasa kama ukiona mtu anaenda kwenye karamu ya mtu ina maana ndio amenyenyekea..Lini huyo makongoro ametetea tabia za Mkono???....nadhani anayo mawazo huru..na amemudu kusimama yeye mwenyewe bila kutegemea sana umaarufu wa babake tangu NCCR.....
Huyo mkono mnayesema hawezi kuacha kuwa karibu na familia ya mwalimu kwa sababu ni distant causin....lakini jiulizeni kwanini Mkono wakati wa utawala wa mwalimu amepata kuhama nchi kwa muda akaishi UK.....inaonyesha kuwa alikemewa!!
Phillemon,
Kumbe unalijua hilo la Mkono kuhama nchi? Nasikia Mwalimu alitaka kumweka detention kwa tuhuma za ufisadi. Akapewa taarifa na watu wa UWT na akakitimua.
 
hana lolote naye mlevi tu huyu...

Afadhali ya mlevi huyu kuliko hao wanafiki 500 wanaowazunguka RA, EL na AC wakitoa meno nje kwa ishara ya kicheko cha furaha kumbe ni kama mbwa anayelilia mfupa.
Heri ya mlevi huyu kuliko wanafiki 300 waliokula naye fedha za Richmond wakaogopa kumtaja
Heri ya mlevi huyu kuliko wanafiki 1000 wanaojifanya marafiki wa EL, RA na AC huku wakiwachonganisha kwa siri kwa JK.
Heri ya mlevi shujaa na mkweli BIG UPPPP Maky.
Wangekuwepo watatu wasingehangaika na Magamba na NGOZI kujichuna ovyooooo!!!!!!!
 
Makongoro si Mtu wa Kumwamini!Nakumbuka sana enzi zile alipokuwa NCCR(Mageuzi) alivyokidhalilisha Chama!Ukiwa na Upeo Mdogo utafikiri ni Hazina!
Kumbe nae si chochote zaidi aeleze kilichomtoa NCCR na Kurudi CCM na hiyo nguvu ya kupendekeza watu wafukuzwe Chamani ameitoa wapi wakati,Hatujawahi kumsikia Akitubu na hata baba wa Taifa aliwahi kumbeza na kututaadharisha dhidi ya Makongoro na NCCR yake!
 
Hapa umenena. Tatizo la wengi wetu ni kutokuwa na dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi bali ni kuleta majibu mepesi katika haja ngumu. Kila mtu alikuwa nawapigia kele kuhusu hawa jamaa, sasa wamefanyiwa kweli watu wanaanza kubeza hata ile juhudi iliyofanyika. Wengine kama vyombo vya habari vya ITV na Radio one badala kuendeleza mapambano venyewe mradi RA,EL na Vijisenti wametoswa wao kwao ufisadi umekwisha hata habari za magazeti kama Tanzania daima marangine wanazikwepa Mzee keshapata alichokuwa anakitaka. Ninachotaka kuweka wazi hapa wengi wa wanaojidai kupinga ufisadi wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi kwa kuangaliani nani anazuia makate wangu si kwa maslai ya Watanzania kwa mfano Makongoro katoa hoja ambayo kwa mtu mwenye dhamira ya kweli angeiunga mkaono lakini wapi ni ulevi tuu wa kuchumia tumbo.

Hata Makongoro inawezekana alipata ujasiri huo kwasababu labda hajawahi kufanya deal na any of the RACHELs. Wengi walikua kimya kwasababu walishakopa hela au kufanya deal na hawa watu kwanjia moja au nyingine. I know Makongoro very well, tulikua majirani miaka ya nyuma. He is not a good leader, watu wanamuheshimu kutokana na jina alilobeba ndio maana akigombania nafasi fulani anapata. Sipendi kuingilia maisha binafsi lakini part of my philosophy is that: Lazima uwe responsible na mambo madogo ndio watu wakuamini na big responsibilities. Naamini Makongoro hana uwezo wakuongoza lakini anaweza tumika vizuri kwenye propaganda.
 
Shida moja aliyonayo Makongoro ni kumtegemea kwa kila kitu Mh Nimrod Mkono. Hata hiyo nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kafadhiliwa na huyu jamaa ambaye naye hatazimiki vizuri kwa wengi. Na hii sio shida ya Makongoro peke yake. Kwa CCM ya sasa mtu safi kabisa hawezi tena kuwa kiongozi.
Huyu Mkono sina imani naye, nimeshamsikia kwenye kashfa za ufisadi wa mabilioni!
 
Phillemon,
Kumbe unalijua hilo la Mkono kuhama nchi? Nasikia Mwalimu alitaka kumweka detention kwa tuhuma za ufisadi. Akapewa taarifa na watu wa UWT na akakitimua.
Kàma yuko kwenye tuhuma za ufisadi toka enzi za mwalimu, why yuko kwenye timu ya Mako?

Halafu CCM Ina vituko sana! Hiki chama kinawaona watanzania wajinga sana!
 
Kàma yuko kwenye tuhuma za ufisadi toka enzi za mwalimu, why yuko kwenye timu ya Mako?

Halafu CCM Ina vituko sana! Hiki chama kinawaona watanzania wajinga sana!

Hujakosea..ni mburula kweli kweli...kama natoka 50yrs bado wanategemea miujiza ya maisha bora toka kwa watu walewale kama sio ujinga ni mini?
 
Dakika 15 za umaarufu wa Makongoro zilishapita.

Mwenyekiti wa chama Mkoa na Mbunge ya Taifa yupi yuko mbele? Makongoro alishakuwa Mbunge, sasa hivi kashuka kwenye vyama mikoani, kwa hiyo habari ya anaweza kufika mbali ni wishful illusion.
Bado una msimamo huu mpaka sasa?
 
Hujakosea..ni mburula kweli kweli...kama natoka 50yrs bado wanategemea miujiza ya maisha bora toka kwa watu walewale kama sio ujinga ni mini?
Population ya Tanzania sasa hivi vijana ndo wengi, lakini uelewa wa wengi ni wa mashaka!

Habari za udaku ie shigongo na issue za kina Diamond wako very interested and very well informed, lakini waulize swali dogo tu Kama vile nini maana ya rasilimali ama muulize tu rasilimali ni nini Kama utapata jibu!

Kuna mtu aliniambia nikiwa kwa kinyozi, sikuamini. Nikaamuwa kufanya kautafiti, kweli wengi wao hawajui maana ya rasilimali, sasa Huyu utamuelezaje umuhimu wa kuchaguwa kiongozi atakayesimamia vyema rasilimali za Taifa? Wengi wao wako kiushabiki tu!

Kama Taifa tuna kazi kubwa sana tu!
 
hana lolote naye mlevi tu huyu...
Mkuu mbona baba yako anakunywa mpaka anaoga pombe hatusemi?..pombe wengi sana wanakunywa hata mkapa alikuwa anakunywa,bushi, kenyatha ndiyo kabisa lakini wanapiga kazi.
 
Back
Top Bottom