Elections 2010 Makongoro Nyerere azitia doa kampeni za Kikwete

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

·Makongoro Nyerere azitia doa kampeni za JK


Na Mwandishi wetu, Bunda

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, ambaye ni motto wa Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, jana alizitia doa kampeni za Rais Kikwete, baada ya kuwahoji watu kama watampa kura mgombea huyo wa urais, lakini alijibiwa kuwa hatapewa kwa kuwa ameshindwa kuliondoa taifa kwenye lindi la umasikini.

Sakata hilo lilitokea jana kwenye uwanja wa stendi, wakati rais Kikwete akiwa katika kampeni wilayani Bunda akitokea katika jimbo la Mwibara, ambapo Makongoro alisimama limkaribisha mgombea huyo huku akitoa vijembe na maneno ya kejeli kwa vyama vya upinzani.

Makongoro alianza kwa kuigiza salamu za vyama vya upinzani, ambapo alianza na ile inayotumiwa na Chama cha Wananchi (CUF), kwa kusema: "Hakiii…" Wananchi wakanyamnyamazia na alipoona kimya, aliamua kuisema ile salamu ya Chadema ya ‘Peoples…' na kujibiwa ‘Power!'

Mwenyekiti huyo aliendelea na majigambo kwa kuwauliza wananchi kama watampa Kikwete kura zao, ndipo ziliposikika sauti kuwa hawampi, kwa sababu ameshindwa kuutokomeza umasikini.

Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye mkutano huo walionekana wakionyesha alama ya vidole viwili, alama ambayo ipo kwenye bendera ya Chadema, jambo lililosababisha mkutano huo kutawaliwa na kelele za kupingana.

Makongoro pia aliutumia mkutano huo kuwabeza wagombea wa vyama vya upinzani kwa kuwafananisha na wapiga debe na makondakta wa daladala, ambao mwisho wa siku wataendelea kuishuhudia CCM ikishinda kwa kishindo.

"Si mnajua wapiga debe na makondakta? Kazi yao ni kupiga kelele za kuita abiria, hivyo hata kwenye kampeni kuna wapiga debe na makondakta nao wanataka kuwa marais," alisema.

Hata hivyo, Makongoro hakuweza kuendelea kunadi sera za mgombea wa CCM kutokana na kelele zilizokuwa zikipigwa na wananchi kuonyesha kukerwa na kauli zake, hivyo kuamua kumkaribisha Kikwete aendelee na mkutano huo.

Akiwahutubia wananchi katika mkutano huo, Kikwete aliwataka kuachana na waigizaji na wanung'unikaji, kwani CCM ina sera nzuri ambazo zinadumisha amani na utulivu nchini………..

Chanzo: Tanzania Daima.
 
Hata Jk atakuwa amezomewa, waandishi wamemstahi tu. Mikoa yote huko kanda ya ziwa mgombea CCM atakuwa amezomewa na wananchi wamemkebehi, ndugu zetu huko hawana unafiki wa kijinga. Hata uwe mtoto wa Nyerere!
 
Hiyo ni Mbulu ingine, wananchi hawako tayari kuitikaitika jambo ambalo wao wanaona sio sahihi, wnaelewa na demokrasi imekomaa hapo. Nawapongeza sana
 
CCm imekwesha,, hawana jipya

JK anasema amani na Utulivu... hii amani ni ipi???? na huu utulivu ni upi??????

yaani watanzania tudanganye na amani wakati Tanzania ni nchi maskini,, elimu mbovu,, miundo mbinu mibovu.. utawala wa kifamilia na urafiki na takrima umetawala,,, huduma za afya mbaya,,, kodi zimekuwa nyingi,,,<<<< HAKUNA HILO,, TUNAFANYA MABADILIKO...>>>

Watanzania tusidanganyinge na utawala huu wa ccm haufai tuupige chini sasa...
 
hahahahaha pipos pawa kazi kweli kweli kila nikipita maeneo ya Chuda hapa anaongelewa Dr. Slaa tu kama mkombozi wao.
 
Gazeti la Tanzania Daima kwa CCM ni sawa na Uhuru kwa Chadema. Ni uongo mwanzo mpaka mwisho!
 
Hata Jk atakuwa amezomewa, waandishi wamemstahi tu. Mikoa yote huko kanda ya ziwa mgombea CCM atakuwa amezomewa na wananchi wamemkebehi, ndugu zetu huko hawana unafiki wa kijinga. Hata uwe mtoto wa Nyerere!

safi sana maana wameshachoka ubabaishaji wa CCM kila siku porojo tu
 
Back
Top Bottom