Makongoro Mahanga Aanza Kujitetea Leo

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Dk Makongoro aanza kujitete leo
Send to a friend
Monday, 26 March 2012 13:34
0digg (Mwananchi)

James Magai
MBUNGE wa Jimbo la Segerea , Dk Miltoni Makongoro Mahanga leo anaanza kujitetea katika kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Katika utetezi wake, Dk Mahanga anatarajiwa kuwa na kibarua kigumu kupangua tuhuma au madai yalitolewa mahakamani hapo na mashahidi wa upande wa utetezi dhidi yake, jambo ambalo linasubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wanaofuatilia kesi hiyo.

Hatua ya Dk Mahanga na wadaiwa wengine katika kesi hiyo kufika mahamamani leo ili kuanza kujitetea inatokana na amri ya Jaji Profesa Ibrahim Juma , anayesikiliza kesi hiyo aliyoitoa, Machi 21, baada ya upande wa madai kufunga ushahidi wake.

Kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2011 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo katika jimbo hilo, , kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe, akipinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Mahanga wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mbali na Dk Mahanga ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambaye ni Msimamizi wa Uchaguizi wa majimbo ya Ilala (mdaiwa wa tatu).

Wakati Mpendazoe akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala, Dk Mahanga anatetewa na Mawakili Jerome Msemwa na Aliko Mwamanenge wakati AG na Mkurugenzi wakitetewa na Mawakili wa Serikali David Kakwaya na Seith Mkemwa.

Tuhuma kubwa iliyotolewa na mashahidi karibu wote dhidi ya Dk Mahanga ni ile ya kukamatwa na wananchi Tabata Kimanga akiwa na masanduku ya kura na kisha kukabidhiwa katika kituo cha Polisi Buguruni.

Mbali na Dk. Mahanga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala pia anatarajiwa kukabiliana na changamoto kubwa katika ushahidi wake wa utetezi kutokana na malalamiko mengi yaliyoelekezwa kwake na mashahidi wa upande wa madai.

Wakati wa ushahidi wao mashahidi hao wa upande wa utetezi walidai kuwa kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi, ambazo mdaiwa huyo alishindwa kuzipatia ufumbuzi na nyingine kuzisababisha yeye mwenyewe.

Ukiukwaji huo ni pamoja na kutokutangaza matokeo ya kituo kimojakimoja, kuyapatia ufumbuzi matokeo ya vituo mbalimbali yaliyopotea katika kata ya Kiwalani naVingunguti pamoja na kudaiwa kushuhudia masanduku mengine ya kura yakiwa matupu.

Upande wa mashtaka ulifunga ushahidi wake Machi 21 baada ya kuwaita mahakamai jumla ya mashahidi 13 ambao walitoa ushahidi katika kesi hiyo.

Hata hivyo hadi upande wa mashtaka unafunga ushahidi wake haukuweza kuwasilisha mahakamani kielelezo chochote kuwa sehemu ya ushahidi wake, baada ya upande wa utetezi kupinga baadhi ya vielelezo ambavyo Mpendazoe aliyetoa ushahidi wake akiwa shahidi wa kwanza.

Wakati akitoa ushahidi wake, Mpendazoe aliomba mara mbili kuwasilisha mahakamani hapo vielelezo viwili kwa nyakati tofauti ili viweze kuwa sehemu ya utetezi wake lakini akagonga mwamba baada ya mawakili wa upande wa mashtaka kumwekea pingamizi.


Jaji Juma alikubaliana na hoja za utetezi na kuukataa kuwa haujakidhi vigezo vya kuwa nyaraka ya umma.


Katika kesi hiyo , Mpendazoe analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi katika jimbo hilo akida taratibu na sheria za uchaguzi zilikiukwa. Hivyo anaiomba Mahakama hiyo itengue ushindi wa Dk Mahanga na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo, au yeye atangazwe mshindi.

 
Hapo kama atakutwa na hatia, huyo mkurungezi wa Ilala, apigwe mvua kadhaa! ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom