Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere

Makongoro hana maana hata kidogo.WanaCCM Mara watakuwa vichaa kukubali kuongozwa na mhuni.Nakumbuka Mwl Nyerere mwaka 1995 alituita wapiga kura wa Arusha wahuni kwa kumchagua Makongoro mbunge wa Arusha mjini naanza kuamini Nyerere alikuwa sahihi kabisa.
Baadae akatinga na jeans bungeni...
 
mila za mkoa wa mara katika ndoa huwa hakuna talaka hata kama mwanamke akizaa nje ya ndoa watoto wanatambulika kuwa ni wa mume aliyetoa mahari, kama makongoro anaona ni kero aende kortini kudai jina la baba yake
ni kweli mkuu ndoa za Mara hazivunjiki. hata kama Leticia akifa leo atazikwa Butiama.kuna maza mmoja walitengana na mumu wake more than 10yrs lakini watoto walikozaliwa baada ya kutengana walitumia jina la yule mume wake halisi. makongoro ni mlevi wa kutupwa itakuwa amevuta mlungula kwa shanif(MOIL)
 
Tunapokwenda kuna siku shule, viwanja na taasisi zenye jina la Nyerere zilizopo kwenye maeneo yanayoongozwa na vyama visivyo CCM watalazimisha kubadilisha majina. Wait and see, watu wame m-Trade Mark Mwalimu as theirs!
 
Huyu mtu nilisoma naye Tabora School miaka ya sabini mwishoni.Ni mahiiri wa kuongea hasa kitu kikiwa pumba ,Ulevi ni sifa yake kubwa kwani nakumbuka aliwahi kupewa suspension akarudi Msasani JK akamfukuza kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu wakati ule ndiye alimleta shuleni akatandikwa mboko sita za nguvu kwa utovu wa nidhamu.Kwa hiyo hana nidhamu hadi kesho.Kama angekuwa mtu makini tusingeshangaa wakati dunia ikitunuku watoto wa viongozi waliotangulia madaraka ya kuongoza nchi zilizoongozwa na baba zao yamkini hata yeye angekuwa kiongozi wetu wakati huu.Lakini kwa sababu ya ulevi na utovu wa nidhamu hata kwa wazazi wake basi ndo maana CCM huko Mara haishi kupigwa mwereka.Huyo ndiye Charles Makongoro JK Nyerere.
 
Huyu aliwahi kukimbia kulipa bili ya bia pale Fourways ya zamani kule masaki....tukamlipia kwa heshima ya babaye na kwa kuwa alikuwa Anakunywa SAFARI...

Hahahaha na ndo kinywaji chake huyu jamaa, sasa sijui zinampunguza akili?
 
Kwani sheria ya ndoa ya Tanzania inasemaje? Na ile ya kanisa, kama walifungia kanisani inasemaje? Majina ya watoto wao hamna mwenye jina la babu au bibi (maanake sijui jinsia yao)? Je, angekuwa mjane ingekuwaje?
 
Ujumbe wangu kwa Makongoro kwa yeyote mwenye simu yake - shemeji yake akifanikiwa na hata wale watoto watatu wanaomwita Baba Mkubwa watafanikiwa kimaisha. Kitu cha kufanya hapa ni kumpigia ndogondogo shemeji yake ili ashinde badala ya kwenda kumsaidia mtu baki.
 
Iyo comment ingekuwa imetoka kwa mtu mwingine atleast ningeweza comment but of all the people kumbe imetoka kwa Makongoro
 
Viongozi wa CCM hovyooo! Makongoro anadhani kila mwenye jina la Nyerere basi anaenziwa? hizo ni fikra za kijinga kabisa, Akienda kule kwa jamaa zangu wamakonde si atashangaa sana maana kule majina kama Nyerere, Mungu,Yesu, serikali nk sio ya ajabu. Sasa utamtukuza Mmakonde mmoja kwa vile kajipa jina MUNGU?
 
MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Makongoro atambue kuwa jina huwa halina haki miliki( copyright) na huwezi kumzuia mtu asitumie jina la mtu maarufu. Akianza kufuatilia atakonda maana kuna watu wengi wanatumia jina nyerere wengine kambarage. Wengine wapo tanzania wengine wapo nje ya nchi mbona hajawashukia hao?????

Akiwa jukwaani aeleze kuhusu CCM na mafanikio yao sio kuanza kuchambua majina ya watu.

Leticia ana haki ya kutumia jina hilo hata kama angekuwa hajaolewa na mtoto wa nyerere.
 
Viongozi wa CCM hovyooo! Makongoro anadhani kila mwenye jina la Nyerere basi anaenziwa? hizo ni fikra za kijinga kabisa, Akienda kule kwa jamaa zangu wamakonde si atashangaa sana maana kule majina kama Nyerere, Mungu,Yesu, serikali nk sio ya ajabu. Sasa utamtukuza Mmakonde mmoja kwa vile kajipa jina MUNGU?

Mbona amekaa kimya kuhusu steve nyerere anayelitumia jina hilo kibiashara, naona CCM wameishiwa kwelikweli
 
Yaliyofanywa na Makongoro ni unyanyasaji mkubwa kijinsia. Leticia anazo haki zote za kutumia jina la Nyerere kwa sababu alifunga ndoa takatifu katika kanisa Katoliki. Kuingiza mambo ya ndoa ya mtu kwenye mambo ya siasa ni dalili za kufilisika. Mwacheni Leticia ahukumiwe na achaguliwe na wananchi kwa uwezo wake binafsi. Naamini kabisa Mzee Kambarage Nyerere angelikuwa hai wala Makongoro asingethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumchafua shemejiye. Makongoro amejiaibisha sana!
 
Makongoro anafrustration kuropoka upupu kama huo, kwani watu wangapi dunia hii wanatumia jina la Nyerere kama jina na wala si ukoo wa JK Nyerere. Alitakiwa aeleze mapungufu ya mgombea na siyo kueleza umma private issues, huenda alikuwa haelewani na huyu shemeji yake na pia unaweza kuta yeye Makongoro ndio chanzo cha mgogoro wa shemeji yyake huyu na mumewe
 
Yaliyofanywa na Makongoro ni unyanyasaji mkubwa kijinsia. Leticia anazo haki zote za kutumia jina la Nyerere kwa sababu alifunga ndoa takatifu katika kanisa Katoliki. Kuingiza mambo ya ndoa ya mtu kwenye mambo ya siasa ni dalili za kufilisika. Mwacheni Leticia ahukumiwe na achaguliwe na wananchi kwa uwezo wake binafsi. Naamini kabisa Mzee Kambarage Nyerere angelikuwa hai wala Makongoro asingethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumchafua shemejiye. Makongoro amejiaibisha sana!

Msishangae, CCM maji ya shingo yaani wamebanwa kila mahali
 
Back
Top Bottom