Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 63,557
- 112,509
Kipele kimepata mkunaji haki a mama
View attachment 388265Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepiga marufuku viongozi wa dini kupanga foleni wanapokwenda katika ofisi za wakuu wa wilaya wa mkoa huo.
Makonda ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Baraza kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)
"Natoa wito kwa wakuu wa wilaya wote katika mkoa wangu, ni marufuku kumkuta kiongozi wa dini kupanga foleni katika ofisi zenu,hawa watu lazima waheshimiwe kama viongozi wengine wanavyoheshimiwa "alisema
Kuhusu ujenzi wa ofisi za Bakwata, Makonda amesema kuwa ujenzi huo umefadhiliwa na mfuko wa GSM.
" GSM foundation ndio inayojenga ofisi za Bakwata hivyo jamii inayonunua bidhaa za GSM ijue kuwa fedha wanazotoa zitarudi kwa jamii "alisema
Mufti mkuu wa Tanzania sheikh Abubakar Zubairy bin Ally, amewataka waumini wa dini ya kiislaam kuachana na dhana potofu ya kuwa jengo hilo si halali kutokana na jitihada za ujenzi wake kufanywa na muumini wa kikristo.
" Katu hatutashtushwa na kejeli za mitandaoni, Mkuu wa mkoa anayohaki ya kusaidia jamii ambayo imezungukwa na makundi mbalimbali ya dini "alisema.
Wasipange foleni wapiga kura wabadilishe uamuzi!Hata kwenye uchaguzi mkuu wagombea wote walipanga foleni hakuna aliekuja na kuingia kupiga kura eti yeye ni muhimu!
Naomba kujuzwa haswa hii GSM ni taasisi inayojihusisha na nini lengo lake???
Kwanini wanawatumia watu wenye ushawishi kwenye kutoa misaada kama wanasiasa wafanyabiashara tifauti wasanii wakubwa?
Ni kwanini watu wanawatumia kama agency ya kutolea au kupokelea misaada?
Ni shughuli gani hasa wanaifanya for a living na ownership yake ipo vipi???
hata wenyeviti wa jumuiya ni viongozi wa diniMi hapo hata sijamuelewa.... ni viongozi gani hasa anaozungumzia hapa??? Kiongozi wa dini mathalani kwa wakristo.... je ni Kadinali?? Askofu?? Mchungaji/padre? Sista?? Kiongozi wa jumuiya?? Mzee wa kanisa???Katekista??
Na utamjuaje hasa huyu ni kiongozi wa dini?? Atakuwa kavaa kitambulisho?? Kwa waislam kwa mfano kiongozi wa dini ni yule atakayevaa kanzu?? Ni viongozi wa bakwata au mashehe wa misikiti?? Au mashehe wa mikoa/wilaya?? maimamu??
Na nje ya wakristu na waislam... dini nyingine kama za babu yangu Mtuweta, ambaye yeye ndio kiongozi wake mkuu wilayani, atazitambua?? Au anazungumzia dini zilizoletwa na ndege/meli??
Ngoja tuendelee na hii sinema mpya maana zile za walimu kupanda bure daladala, kuondoa ombaomba, kufukuza machangudoa nk nk nk..... bado zinaendelea. Strerling hauwawi....
naskia ina uhusiano fulani na home shopping centerNaomba kujuzwa haswa hii GSM ni taasisi inayojihusisha na nini lengo lake???
Kwanini wanawatumia watu wenye ushawishi kwenye kutoa misaada kama wanasiasa wafanyabiashara tifauti wasanii wakubwa?
Ni kwanini watu wanawatumia kama agency ya kutolea au kupokelea misaada?
Ni shughuli gani hasa wanaifanya for a living na ownership yake ipo vipi???
Kwa mustakabali huo, hakuna atakayepanga foleni...hata wenyeviti wa jumuiya ni viongozi wa dini
Burudani itakuja pale ambapo kuna viongozi wa dini kama kumi hivi wanasubiri huduma... sijui watapanga foleni?
Mkuu wala usisikie, GSM ndo ilikuwa ikiitwa HSC.naskia ina uhusiano fulani na home shopping center
Afu kipele chenyewe kimeota sehemu hatarishi....Kipele kimepata mkunaji haki a mama
Ni shida aseeAfu kipele chenyewe kimeota sehemu hatarishi....
Kweli kabisaKwa mustakabali huo, hakuna atakayepanga foleni...
Wametula kwa nyuma sasa wanatutolea kwa mbeleMkuu wala usisikie, GSM ndo ilikuwa ikiitwa HSC.
Forget Abaut It!GSM NAWAAMBIA ITAMUONDOA MAKONDA U GUYS TRUST ME
Ni hii serikali au ni Mako...
Nilijua Serikali haina Dini
Ila naona hii Dar ya Mako...
Ina Dini
???
Thubutu Makonda hapo ni mpambe tu wenye share hapo ni vigogo wa serikali wajuu wa awamu ya 4!!View attachment 388321 View attachment 388322 View attachment 388323 View attachment 388324 View attachment 388325 View attachment 388326 View attachment 388327 View attachment 388328 View attachment 388329 alafu makonda ana intetest gani kwenye hii company mbona yupo kama nae ni shareholder?
KabisaFoleni ni utaratibu wenye haki.......kasoro tu wenye mahitaji maalum wangefaa wasipange foleni