Makonda: Atakaevaa sare ya CCM kesho, hapandi Daladala

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Chama cha makonda mkoa wa Dar-s-salaam (CHACHAMADA) na baadhi ya wamiliki wa mabus hayo ya usafiri ndani ya jiji la Dar wamekutana leo alfajiri somewhere(secret meeting) na kwa pamoja wameridhia kuwa kesho siku ya Jumamosi mtu yeyote atakaevaa
vazi(nguo)yeyote inayoashiria sare ya CCM(kijani au njano) hatoruhusiwa kupanda daladala yoyote....zoezi hili litaanza kesho kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa mbili usiku.

Baada ya mda huo unaruhusiwa kuvaa nguo yenye rangi yeyote na ruksa kupanda daladala yeyote.

Angalizo:


Siyo watu wengi wanaoingia na kutumia mtandao wa JF. So ikopi hii message kama inavyojieleza kwa kutumia simu yako ya mkononi na uwatumie ndugu na marafiki zako wote wanaoishi ndani ya Dar na wanategemea usafiri wa mabus (Dala dala).

Najua kuna baadhi ya watu watapinga habari hii....lakini mdharau mwiba mguu huota tende.

Source
- ni mtu wangu wa jikoni anaemiliki daladala 5 zenye route tofauti hapa Bongo...UTAKI UNAACHA.
 
Ni uamuzi mzuri sana maan ugumu wa maisha yetu unasababishwa na uatajiri wa vigogo wa CCM
 
sasa hii sio safi, huwezi kumzuia mtu kufanya anavyotaka

let them be, hatujafika huko
 
Mkuu BashaDido kwenye taarifa hiyo kuna kitu umesahau hao wamiliki wa Daladala wamesema hata muda huo wa saa mbili usiku ile picha ya Jembe na Nyundo ibadilishwe iwe Kijiko na Uma au Kisu ili kufikisha maudhui halisi ya hicho chama cha Magamba
 
Biashara kama kawa tena kutakuwa na punguzo la nauli kwa watakaovaa nguoa hizo
 
Hii imetulia,ni meseji kwa chama tawala kwamba kama hawataacha ngonjera leo basi ni bora waachie madaraka leo 2015 mbali taifa linaweweseka
 
Hii sio sawa! Mi binafsi siungi mkono, kila mtu anahaki ya kuchugua chama anachokipenda. Msilazimeshe mtu afuate unavyoamin wewe, wacha waende wakisilize pumba na uwongo wa CCM!
 
R.I.P ccm,mmeiga ya chadema jangwani i5a itawatokea puani.

Since 2005 when it comes to campaigning! CCM is the best to now, BUT WHEN IT COMES TO RULING AND SOLVING PEOPLES PROBLEM CCM is the worst so far! by mkira
 
Wanakuja kwa matembezi ya mshikamano toka maeneo mbalimbali ya jiji si kwa daladala.Polisi wao,mwema wao kova wao,mwamnyange wao,serikal yao
 
Hii imetulia,ni meseji kwa chama tawala kwamba kama hawataacha ngonjera leo basi ni bora waachie madaraka leo 2015 mbali taifa linaweweseka
Mkuu, copy hiyo meseji kwenye simu yako ya mkononi na uwatumie ndugu na marafiki wote.
 
Mkuu BashaDido kwenye taarifa hiyo kuna kitu umesahau hao wamiliki wa Daladala wamesema hata muda huo wa saa mbili usiku ile picha ya Jembe na Nyundo ibadilishwe iwe Kijiko na Uma au Kisu ili kufikisha maudhui halisi ya hicho chama cha Magamba
Copy hiyo meseji kwenye simu yako na uwatumie ndugu na marafiki wote kabla ya kesho. Binafsi hadi sasa nimeshatuma
kwa watu 16.
 
Hii imezidi bana. Tuacheni twende tukaserebuke na TOT. na kula wali wa bure ndio sikukuu yetu hii, Hatuna pesa ya kwenda hotel wala kulipa kuangalia TOT. Hatuendi kupiga kura jangwani hivyo sioni kama kuna sababu ya maana ya kuto kwenda
 
Makondakta si wamiliki wa daladala.....na wala makondakta hawana huu uzushi unaoenezwa,wao wantafuta pesa......!
Propaganda mfu za wasipenda MAPINDUZI!!!!
 
Ingekuwa nzuri sana kama habari hii ingekuwa ya kweli. Nina mashaka na mtoa mada pale alipojishuku na kujitilia shaka yeye mwenyewe. Hali tusiwe tunasapoti kila kitu, yaani konda na dereva walaze njaa familia zao kwa sababu ya CCM. Nadhani kesho ndo nafasi yao ya kuwakamua magamba.
 
Back
Top Bottom