Makonda ataka mkataba wa Machinga Complex kati ya Jiji na NSSF uvunjwe na wahusika wachukuliwe hatua

Angepaswa ashauri mamlaka zinazo shughulikia fraud ziungalie mkataba husika na kujiridhisha kuwa haujakiuka maadili! Na endapo itagundulika kuwa maadili yamekiukwa then wachukue hatua stahiki!​
kwani kasemaje, hajasema TAKUKURU wahusike?

Au ameagiza mtu akamatwe? Which he probably should have said for all I care.

Kuna wakubwa walidhani wana title deed za miaka 99 za nchi hii, tukalazimishwa kuwaimbia nyimbo za kuabudu kumbe ni wabadhilifu wakubwa.

Wamechezea kamali michango ya wafanyakazi wa Tanzania kwa uzembe, au kwa maslahi yao binafsi. Hiyo ndio text book definition ya kusababishia serikali hasara.

Ramadhani Dau akamatwe!
 
Nimegundua sababu ya serikali kushindwa Kila kesi inayofungua mahakamani!! Eti gharama ilipanda kutoka 12.14 hadi 12.7!! Mumeiona hiyo?Infact kama mwendesha mashtaka wa serikali atachukua taarifa hii na kwenda nayo mahakamani basi hakimu anaweza kuitupilia mbali hata kabla hajamaliza kuisoma!! Hebu. Angalia hapa

Ulikimbia hesabu? Kosa hapo liko wapi au hujui kwamba 12.7 ni kubwa kuliko 12.14 kwa ongezeko la 0.56?
 
Tatizo la nchi yetu ni wanasaisa kuingilia taaluma za watu hata kama hawana ujuzi wowote, mwanasiasa wa africa yeye ni Daktari, mhasibu, engineer, mwalimu, n.k. Mikataba ya ujenzi iko very straight kuhusu mgawanyo wa majukumu ya kazi katika mradi, hakuna mkataba wala form of contract hapa duniani inayomtambua mwanasiasa au kiongozi katika mradi. Mwenye authority ya maamuzi kwenye mradi ni yule aliyetajwa kwenye contract kama contact person. Tofauti na huyo akitokea mwingine akatoa maelezo anakua ni kama anapigia mbuzi gitaa.
Wanasiasa wanaweza kuongea maneno mengi lakini hayana mantiki yeyote, wewe unashindwa kulipa deni ontime na kwenye contract umesign kama ukichelewa kulipa deni utalipa interest, siasa zinaingia interest inakua kubwa mnaanza kulalamika kuwa deni halilipiki. Hilo deni mtalipa tu hata kwa kuweka bond mali zote zinazomilikiwa na jiji hadi kufidia hilo deni. Watu wanampongeza mkuu wa mkoa, lakini tungesubili tusikie na upande wa pili tuone ni kwa nini deni limefika hapo.
Kama jiji walisha take over project wakatoa na certificate of compliance, kushindwa kulipa deni sio kosa la mkopeshaji ni kosa lao la kukosa namna bora ya uendeshaji wa hayo majengo. Nilitegemea mkuu wa mkoa angewashuri jiji namna bora ya kulitumia hilo jengo ili liwe na tija, lakini nae amekata tamaa kuwa deni halilipiki, hii sio sifa ya kiongozi. Kiongozi anatakiwa apambane kuhakikisha lisilowezekana linawezekana kwa manufaa ya watu anaowaongoza.
 
wakaguzi huwa hatupersonalize report kama huyu makonda,standards hazitaki hivyo...."nimegundua,nimebaini" what the heck is that!!!
kwanza hiyo special auditing wamefanya wengine yeye kapelekewa taarifa mezani.
Kwani amekwambia yeye ni mkaguzi? aliwatuma wamemletea taarifa na amei''own'' kisawasawa wewe inakuhusu nini au ni mfaidika wa ufisadi?
 
Nafikili wewe hujaelewa na hujui, katika utangulizi kaeleza namna anavyoingia pale. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilipewa jukumu la kusimamia mradi huo ulitaka afanyeje. Halafu unafikili mkataba ni bible au quran kwamba kilichoandikwa humo hakiwezi kubadilishwa. Kama sheria za nchi hutaelewa utakuwa umesoma chuo cha kata ili nisikuweke katika wasomi wa nchi hii???
 
Haya bana mfipa wa fyengeresya. Naona bado una fikra za kwamba kiongozi ana power above the contract, ila haipo hivyo contract is contract na ndo mana kuna declaration kwamba umeuelewa vizuri na una akili timamu. Hakuna kitu kinachoitwa ofisi ya mkuu wa mkoa kwenye contract, ila kunakuwa na appointed person ambaye anaujuzi wa hiyo project na ndo atarepresent hiyo ofisi ya mkuu wa mkoa.
 
TAARIFA YA MRADI WA MACHINGA COMPLEX

1.0 Utangulizi

Mnamo tarehe 19 Aprili, 2016 ofisi yangu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ilipokea barua ya agizo la waziri wa nchi TAMISEMI juu ya kusimamia uendeshaji wa mradi wa Machinga Complex. Ambapo katika kutekeleza agizo hilo nilichukua hatua ya kwanza na ya muhimu ya kuupitia mkataba wote wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya haki na wajibu wa pande mbili zilizohusika kwa maana ya Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kimsingi, tathmini yangu ya mkataba ililenga kubainisha na kujiridhisha juu ya mambo sita yafuatayo; aina ya jengo lililotarajiwa kujengwa, usimamizi wa fedha za mkopo, usimamizi wa ujenzi wa mradi, gharama za mradi, utaratibu wa urejeshaji wa deni na kiwango cha riba kilichoainishwa. Ikukumbukwe tu kwamba, wakati halmashauri ya jiji ikikabidhiwa mradi siku ya kwanza ilikuwa tayari inadaiwa kiasi cha bilioni 19.7 huku mpaka Machi mwaka huu deni lilishafikia kiasi cha bilioni 38 za kitanzania, kutokea kwenye mkopo wa bilioni 12.7

2.0 Uchunguzi

Baada ya kupitia kwa umakini mkataba mzima na kukagua mradi wenyewe, zoezi ambalo lilihusisha kulinganisha kati ya kilichofanyika baada ya mradi kukamilika na taarifa ya upembuzi yakinifu (feasibility study) uliofanyika kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi nimebaini yafuatayo;-

2.1 Ukubwa halisi wa jengo

Nimebaini kwamba majengo ya sasa ya machinga complex hayakujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walikubaliana kwenye mkataba na kupitia kifungu cha 1.1 cha barua ya makabidhiano kinachoeleza kwamba jengo lililokabidhiwa lina sehemu yenye ghorofa 5 na ghorofa 6 ili liweze kumudu idadi ya machinga wasiopungua 10,000 wakati hali halisi baada ya kutembelea jengo hilo ni kwamba jengo lina ghorofa 4 zinazobeba machinga 4,000 tu. Kwahiyo, pamoja na kwamba barua ya makabidhiano ilisainiwa na pande zote mbili licha ya ukweli kuwa maelezo ya jengo yalikuwa tofauti na jengo lenyewe.

2.2 Usimamizi wa fedha za Mkopo

Kwenye usimamizi wa fedha za Mkopo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ni mkopaji hakuhusika na usimamizi wa fedha za mkopo, hivyo mkopeshaji hakuwa na udhibitisho wa gharama halisi, jambo ambalo si tu limefanya mkopaji kutojua gharama halisi za jengo bali pia kulipokea likiwa limechelewa na likiwa halina ukubwa ulioelezwa kwenye mkataba. Kimsingi, haya yote yanazaliwa na maelekezo ya kifungu namba 4.1 kinachoeleza kwamba, mkopeshaji kusimamia mradi kuanzia hatua ya usanifu hadi kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na kufanya malipo moja kwa moja kwa mkandarasi na mshauri wa mradi, kwa maneno mengine pia ni kwamba kifungu hiki kinakinzana na vifungu namba 2.1, 2.2, 10.1 na 11.1 vya mkataba huohuo ambavyo vinaelekeza kwamba mkopeshaji (NSSF) atatakiwa kutoa fedha kwa mkopaji (Halmashauri ya Jiji) kwa ajili ya kugharamia mradi pekee na kuusimamia kama ulivyokubalika kwenye mkataba.

2.3 Kuhusu gharama za mradi

Nimebaini kuwa fedha za mkopo ziliongezeka toka shilingi bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 560, nyongeza ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji, hali ambayo haimtendei haki mkopaji. Kwa faida tu ya wanadar es salaam na watanzania wenzangu ni kwamba, halmashauri ya jiji ilitiliana saini ya makubaliano na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) ya mkataba ambao unalenga kuipatia halmashauri ya jiji mkopo wa bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ingawa baada ya muda kidogo mkopeshaji (NSSF) alisema kuwa bilioni 10 na hivyo kufanya marekebisho ya mkataba na kuongeza mkopo wa bilioni 2.14

2.4 Urejeshaji wa deni

Suala la urejeshaji wa mkopo unazua utata pale mkataba unapoainisha kuwa, mkopaji ataanza kulipa marejesho ya deni kuanzia tarehe 31 Desemba, 2008 tarehe ambayo mradi ulikuwa unatarajiwa kuwa tayari umeanza lakini mkopeshaji (NSSF) alikuwa hajamaliza ujenzi, na cha ajabu mkopaji (Halmashauri ya Jiji) alitakiwa kuanza kulipa deni hata kabla ya muda wa grace period kuisha wakati jengo likiwa bado lipo mikononi mwa mkopeshaji ambaye alijitwisha jukumu la ujenzi huku akiwa bado akang’ang’ania kulipwa riba.
mara tu tarehe hiyo ilipofika hata kama mpokeshaji mwenyewe alikuwa bado hajakamilisha ujenzi huku akidai pesa ya riba.

Uwezo wa Mradi

Uwezo wa jengo hilo lililopo hata kama litafanya kazi kwa uwezo wake wote kwa maana ya kujaza nafasi zote zilizopo ni kasi cha sh124,796,666.666 kwa mwezi ambazo ni sawa na kiasi cha sh1,497,560,000 kwa mwaka. Pungufu ya 60% ya lengo la Mradi kama ilivyokuwa kwenye upembuzi yakinifu.

3.0 Mapendekezo

3.1 Baada ya uchunguzi huu ulionifanya kuamini mambo makubwa matano niliyoyaainisha hapo chini na ambayo yameniongoza kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;-

• Deni halilipiki – ukweli ni kwamba, ukizingatia kiasi cha pesa kinachodaiwa kutoka kwa halmashauri ya Jiji ambacho mpaka sasa ni zaidi ya bilioni 38 utagundua kuwa, halmashauri haiwezi kulipa deni hilo. Ikilinganishwa na uwezo wa jengo hilo deni hili litalipwa baada ya miaka isiyopungua 24

• Mkataba wote huu ni wa hovyo na haukupaswa kusainiwa hata kidogo.

• Kitendo cha kusaini mkataba huu ni hakika na bayana kuwa rushwa ilitumika pande zote mbili, kwa maana haiwezekani ukaacha taaluma yako kwa kiwango hicho cha kutoona udhaifu huu wa wazi wa mkataba huu kama hujapofushwa macho na rushwa.

• Mkataba huu hauna tija kwa upande wowote ule: sio NSSF kwasababu halmashauri ya Jiji hawana uwezo wa kulipa deni, wala sio kwa Jiji lenyewe kwani halina uwezo wa kutekeleza mkataba kwa kufanya malipo yanayotakiwa na hauna faida vilevile kwa machinga kwa sababu gharama ya kupanga ni kubwa.

3.2 Mapendekezo

1. Kuvunjwa kwa mkataba na NSSF kuchukua eneo lao, kwa makubalino ya kwamba, Halmashauri ya Jiji walipwe kodi ya ardhi jambo ambalo linaweza kufanyika kwa urahisi kupitia NSSF na halmashauri ya Jiji kumiliki hisa kwa pamoja.

2. Au NSSF wakabidhi jengo kwa halmashauri ya Jiji, lakini wakae na kukubaliana upya na hivyo kuandika mkataba tofauti na ule wa mwanzo.

3. Mwisho, wahusika wote wa pande zote mbili wachukuliwe hatua kwani hatuwezi kutumia fedha za mifuko za hifadhi ya jamii ambazo ni fedha za wanyonge wa taifa hili kwa faida ya wachache waliotanguliza ubinafsi,.

Imetolewa na:
Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam

.View attachment 371344

Kwahiyo ile kamata kamata ya wasiyo na kazi imesha expire?
 
wakaguzi huwa hatupersonalize report kama huyu makonda,standards hazitaki hivyo...."nimegundua,nimebaini" what the heck is that!!!
kwanza hiyo special auditing wamefanya wengine yeye kapelekewa taarifa mezani.
Mkuu wewe ulitaka aseme vipi wakati anapalilia kibarua?
 
Hivi hawa jamaa wanajitekenya wenyewe au??Hili swala JJ Mnyika alilisemea sana kwenye vikao vya Madiwani,akahamia bungeni na baadae wakarirudisha mtaani kuwa Machinga Complex ni mradi wa wiziii...Mdee alipiga kelele kina Makonda wakati wakiwa vibaraka wa Samweli Sitta wakapinga kwa nguvu zote.

Mwizi mkuu katika mradi huu ni CCM ya Masaburi Dsm na yule aliyetutengenezea ARV fake,ambaye kila siku Makonda anaambatana nae...Hawa jamaa ndio waliofisidi mkopo na ujenzi wa Machinga Complex

Makonda wewe kama RC tuliza kithembe na pua yako...Mamlaka yako katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ina mipaka yake,hili suala lipo mikononi mwa Meya,na alikuwa anakamlisha report yake aje amwage hadharani..Sababu ya aibu umewahi ili ionekane sio UKAWA waliotumbua hili....Wewe utaishia kutoa tamko huna mamalaka,Mamalaka ipo kwa Meya wa Jiji na Madiwani wake...Hawa ndio watasema na kutenda wewe utaishia kusema tu.

Masaburi turudishie UDA yetu na ulipe mkopo wa Machinga Complex....
Asante sana kwa kutukumbusha mkuu na mungu akubariki
 
Hapo ndipo ninapowachukieni wanasiasa yaani.
kwani akilisema meya au mkuu wa mkoa suala hilo hilo katika uhalisia kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi tatizo linakuwa nini?
Wote si ni viongozi wa kuwatumikia wananchi?
Shida iko wapi?
sisi tusio na vyama tunawatizamaje?
maendeleo yanabagua chama au nini?
wanasiasa
 
Back
Top Bottom