Makombora yatua nyumbani kwa Pinda - Askari Wafuta Picha

Du hata Baraza kivuli (la wabunge wa Upinzani) nalo wajiuzulu haiwezekani watanzania wakafa kwa mabomu tena ya mjini kabisa
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA WALA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA KUONGEZEKA: KWA HILI SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI

Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

Yalianza na vifo vya raia kule (1) Pemba, baadaye (2) Unguja, Kisha (3) Mbagala, nako Arusha Mjini, (4) mauaji ya wakulima kule Mashamba ya mpunga kule Mabuki Mbeya na sasa (5) Gongolamboto.

Ajabu ni kwamba licha ya wananchi wengi kuuaua na mali zao kuteketea, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuwajibika wala kuwajibishwa serikalini. Kote ni kiburi na jeuri tu mbe ya kupotea uhai wa mtu na watoto kubaki miyatima!!!

Jukumu la msingi halijazingatiwa; kuna watu wanasinzia kwenye majukumu nyeti na sasa kutugharimu kiasi hini, wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwani hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????

Gongo1.jpg

Gongo2.jpg

_51307856_munition_ap.jpg

_51307454_bus_ap.jpg

Debris and arms were hurled across the Tanzanian of city of Dar es Salaam on Wednesday night after an accident triggered a series of explosions at Gongola Mboto military base.
_51310264_lostchildren_ap.jpg
Tanzania's Red Cross says about 200 children who lost their parents during the confusion of the blasts are being cared for at the city's stadium.

_51312030_cherehani.jpg

attachment.php
 
kwa hakika serikali KUU inawajibika tena 'kikamilifu' kwa hili la mabomu, nilikwepa mabomu 2 hiyo juzi na kujinusuru.
 
Jamanii kuna habari za kiintelijensia zinasema jeshi lilishakuwa tayari kwa milipuko dalili zilishaanza kuonekana tangu saa 5 asubuhi....waliwapigia simu wastaafu wa vyeo juu...woote wanaokaa ukonga na gmboto kuwa waondoke.....kuna mstaafu mmj ambae ame pooza anaishi ukonga aliondoka saa 9,,.....,wanajeshi walishajiandaaa wakawa on high alert hajafa hata mmj....walijua...fanyeni utafiti

Mh, sasa kama walijua mapema na wakafanikiwa hata kuwataarifu kwa njia ya simu wastaafu wao, walishindwa nini kuwapa taarifa wananchi waishio jirani na kambi ili nao wahame angalau kuokoa maisha?
 
Mkuu,

Kuna wanajeshi zaidi ya 4 wamepoteza maisha. Ngoja niendelee na intelijensia yangu nitakuja na majina kabisa. Kuna malalamiko ya ufanyaji kazi katika mazingira magumu hasa kwa sakari wa vyeo vya chini. Kifupi ni uzembe tu ndicho kilichopelekea maafa hayo.

Asante Rev. kwa taarifa. Hata hivyo inasemekana wanajeshi wengi walikuwa wamehamisha familia zao. Mimi naamini huu nu ugaidi wa ndani. Kwenye ugaidi watu hutishia kupewa kitu fulani na kutishia kulipua au kuua mateka wasipotimiziwa haja zao. Isije ikawa waheshimiwa wa Dowans wametishia kuwa wasipolipwa watafanya kweli na hayo ndiyo maafa yake na kuwa wanasubiri kufanya zaidi. Hivi Watz tuko salama kweli kwa ugaidi huu?
Ni mahali gani Tz ambako jeshi halina kikosi? Kwa D'Salaam tu ni karibu kila mahali. Fikiria Kimara, Kigamboni, Kunduchi, Boko, Kibaha, Bagamoyo, nk. Je, tutaaminije kuwa serikali yetu si mu-bia wa ugaidi huu kwa majibu na hoja nyepesi nyepesi wanazotupa?
Serikali inaposhindwa kulinda raia wake hasa kuwatoa hofu kuwa si ya uwezekano wa vita bali kuwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama (walivyoviajiri na kuwalipa mishahara) viko makini katika kulinda usalama wa wananchi. Leo hii mtanzania hana hofu ya mipaka ila ana hofu kuwa walinzi wake kikatiba watafanya uzembe ambao utasababisha vifo kwake na kwa familia yake na kuleta maafa mengine. Huu ni ugaidi. Viongozi wetu ni vema wajue hivyo na wawajibike
Kwa vile taarifa za jeshi ni siri kubwa huwezi kujua kilichomo ndani. Utakachojua baadaye ni taarifa kama za Kagoda na Meremeta kuwa ni mambo ya kiusalama. Wizi unapohusishwa na usalama ni ugaidi. Leo tunazungumzia maafa ya watoto wetu kufeli mitihani kwa kiwango cha 88.5% ambao wamepata madaraja ya iv na O; hata kabla hatujatulia na tukiwa kwenye mgao usio na ukomo watz wanuawa si kwa majeshi kutoka nje ila kwa uzembe wa walinzi wao. Halafu tunapewa lugha nyepesi kabisa kwa mambo mazito kama hayo. Spika wa Bunge tukufu, anasema si dharura na hapo hapo anaahirisha bunge. Hii maana yake ni nini? Kwa nini Spika asite kuruhusu mjadala wa jambo zito kama hili? Anaufanyia mjadala huu kadablakadabla kama alivyoifanyia hoja ya Mh. Lema? Huu ni Ughaidi. Nitaendelea kuamini hivyo mpaka nitakapopata majibu ya msingi.
 
Mtumishi wa mungu Masa na wengine: Inawezekana kabisa kuwa hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyekufa na hiyo inawezekana tu kama yafuatayo ni sahihi.

1. Wanajeshi kama watunza silaha na watu waliokuwa karibu kabisa na mlipuko siku ya tukio hawakuwa wanalinda maghala hayo

2. Wanajeshi walikuwa na perfect information juu ya ulipukaji wa mabomu hayo, yaani siku, saa na mahala patakapolipuka mabomu hayo

3. Kwa kuwa wanajeshi wao wamefundishwa mbinu za kujilinda na mabomu vitani haswa pale yanapolengwa kwao basi ni dhahiri kuwa wanajeshi walichukua tahadhari ya kujilinda na mabomu hayo hata kabla hayajalipuka vinginevyo yangewakuta kama wenzao wa Mbagala ambao hawakuwa na taarifa rasmi ya ujio wa milipuko

4. Wanajeshi walipoona yanakaribia kulipuka wakaamua kuingia kwenye mahandaki yao yaliyozagaa kambini na kuyaacha mabomu yalipuke mpaka yatakapotulia ndipo wakatoka na kutangaza wameyadhibiti.

Kama hayo yote hapo juu ndivyo ilivyokuwa basi ni dhahiri mlipuko huu ulikuwa ni wa makusudi na wenye lengo la kuwadhuru wananchi wasio na hatia ili kutimiza malengo fulani, kwa definition ya kuua raia wasio na hatia kwa malengo ya kisiasa, huu unastahili kuitwa ni UGAIDI japo si wakujitoa muhanga. Vinginevyo ni lazima out of control milipuko ianze na kudhuru from the source kabla ya kule yatakapotua mabomu hayo kama ni perimeter ya 10 kilometer au below.

Nashukuru Hofstede kwa kuungana nami ... HUU NI UGAIDI MKUBWA SANA. Ikiwa wanajeshi walijua mapema, naamini amiri Jeshi mkuu pia alijua, kwa nini haikuchukuliwa tahadhari? Kwanini wananchi waachwe wakifa na kuhangaika. Kulikuwa na uwezekano mkubwa kabisa wa kupunguza maafa hayo kwa kuwaonya wananchi mapema ili wahamishe familia zao, kuliko zile patashika za usiku.
 
KWA KWELI KWA UCHUNGU MKUBWA, NAWAPA POLE WALE WOTE WALIOKUMBWA NA MAAFA HAYA, MWENYEZI MUNGU ALAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, NA WALIOJERUHIWA HAWAPE MOYO WA UVUMILIVU,

ila serikali hii naifananisha na senene, kufunika kichwa kuacha makalio wazi.....:A S 20:
 
Ndugu wanaJF kua kitu kinanishangaza, hivi katika milipuko ya mabomu Gongo la Mboto hakuna wanajeshi aliojeruhiwa na kufa? Mbona hatuambiwi?

Ukishangaa ya musa utaona ya F....... hii serikali nyie chubirini tu. Ukweli utadhihirika tu.
 
Nashukuru Hofstede kwa kuungana nami ... HUU NI UGAIDI MKUBWA SANA. Ikiwa wanajeshi walijua mapema, naamini amiri Jeshi mkuu pia alijua, kwa nini haikuchukuliwa tahadhari? Kwanini wananchi waachwe wakifa na kuhangaika. Kulikuwa na uwezekano mkubwa kabisa wa kupunguza maafa hayo kwa kuwaonya wananchi mapema ili wahamishe familia zao, kuliko zile patashika za usiku.

nawashukuru sana wana JF kwa kuumiza vichwa vyenu kujadili hili jambo lililo sababishwa na wapumbavu wachache na kusababisha maafa na ulemavu kwa raia wasio na hatia. ILA NDUGU ZANGU HII ISSUE KAMA KWELI WANAJESHI HAWAJAFA, BASI HUU NI MCHONGO SIO BURE, TENA MCHONGO HUU INAWEZEKANA UMEHUSISHWA NA UUZWAJI WA SILAHA NJE YA NCHI KWA MAHARAMIA, NA KUCHOMA GHALA LA SIRAHA KUPOTEZA USHAHIDI KWA MA'AUDITORS WA SILAHA. huu ni mtazamo tu, wala sina ushahidi na hili jambo.:A S 13:
 
Dar Simanzi Send to a friend Friday, 18 February 2011 08:46 0diggsdigg

*MAKOMBORA YAUA 40, YAJERUHI 300
Waandishi Wetu
MILIPUKO ya mabomu iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika ghala la kuhifadhia silaha la JWTZ, Kambi ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, imesababisha vifo vya watu 39 na majeruhi 292, Mwananchi limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa maiti na majeruhi hao walifikishwa kwa nyakati tofauti jana katika Hospitali za Wilaya ya Ilala (Amana), Temeke na Muhimbili za jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi jana mchana ilikuwa imepokea maiti 18 na majeruhi 80, Amana maiti 19, majeruhi 138 na Temeke maiti wawili na majeruhi 74.

Hata hivyo, Serikali ilisema waliokufa katika milipuko hiyo ni watu 20 na majeruhi ni 300.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshaki Shemweta aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, hospitali hiyo ilipokea majeruhi 157.
"Majeruhi 40 walifanyiwa uchunguzi na kuruhusiwa, wengine 63 bado wanaendelea na matibabu hapa na majeruhi 19 walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini hapa," alisema Shemweta na kueleza kuwa hata hivyo, idadi hiyo inaendelea kuongezeka.

Majina ya waliokufa
Shemweta aliwataja waliofia hospitalini hapo kuwa ni watu watatu wa familia moja; Neema, Tina na Stela Nyigiogo. Kwa mujibu wa mganga huyo, wengine waliokufa ni Zahari Imamu, Ally Chambusa na Hadija Ally.
Wengine ni Sofia Salumu, Mwindini Mamla, Hansi Ibrahimu, Neema James, Vivian Suma, Mainda Ismail, Salehe Musa, Amina Kihiyo, Rose Anthony na Sia Salum.
Shemweta alisema kuwa miili ya wanaume wawili haijatambulika, hivyo bado jihada za kuitambua zinaendelea ambapo kati ya marehemu, wanaume ni 8 akiwamo askari magereza mmoja na wanawake ni 11.
Hata hivyo, Shemweta alieleza kuwa maiti kumi zilitarajiwa kupelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi
"Miili hiyo inahamishwa pamoja na majeruhi 35 wanaopelekwa katika kitengo cha mifupa cha MOI kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kufanyiwa upasuaji," alisema Shemwela.
Hosipitalini Muhimbili
Habari kutoka Muhimbili zimeeleza kuwa hospitali hiyo imepokea maiti 18 na majeruhi 80 waliotokana na milipuko hiyo.
Afisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha aliliambia gazeti hili kuwa kati ya maiti hao, wanawake ni saba na wanaume 11.
"Jana (juzi) tulipokea maiti tano na leo hii tumepokea maiti 13 kutoka Hospitali ya Amana na jumla yake kuwa 18 kati yao wanawake ni saba na wanaume ni 11,"alisema Aligaesha.
Aligaesha aliwataja marehemu hao kuwa ni Zainabu Mohamedi kutoka trafiki makao makuu, Baba Lyaiya ambaye ni mkazi wa Kivule, Hadija Aly, Sofia Salumu, Mwidini Mwaule, Hamisi Hasani na Zaharani Imamu wote wakazi wa Gongo la Mboto Mwisho pamoja na Aly Chambulo, Neema James, Theolas Katombo na Aly Ibrahimu.
Hata hivyo, ofisa habari huyo alieleza kuwa badhi ya maiti zilikuwa bado zinaletwa na polisi katika hosipitali hiyo na kwamba zilikuwa bado hazijatambuliwa.
"Miongoni mwa majeruhi 80 tuliowapokea na waliopo wodini mpaka sasa ni 18 na madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wanaendelea kuhakikisha wanapata huduma sitahiki,"alisema na kueleza kuwa majeruhi 44 wamepelekwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hosipitali ya Temeke
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke, Marium Malliwah alisema hosipitali yake ilipokea majeruhi 74 na wawili kati yao walifariki dunia.
Alisema baada ya matibabu, majeruhi 34 waliruhusiwa na wengine wanane wakapelekwa katika Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Wengi wavunjika mikono, miguu

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu huyo, wengi wa majeruhi waliofikishwa hospitali hapo walikuwa wamevunjika mikono na miguu na baadhi yao walikuwa kwenye hali mbaya.

"Katika hospitali yetu tumepokea majeuhi 74; wawili wamepoteza maisha, wagonjwa wanne tumewapeleka Muhimbili baada ya kuonekana kuvunjika mikono na miguu na kuwa katika hali mbaya. Majeruhi waliobaki tumewapeleka katika kambi ya majanga ambapo wamelazwa kwa ajili ya matibabu zaidi," alisema Malliwah.

Kauli ya JWTZ kuhusu vifo
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa JWTZ, Luteni Kanali Kapambala Mgawe alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa watu 20 wamekufa katika tukio hilo.
Aidha, alisema watu 500 wamejeruhiwa katika tukio hilo na wanatibiwa katika hospitali tofauti za jijini Dar es Salaam.
Mgawe amewataka wananchi kutoondoka kwenye maeneo wanayoishi kwa kuwa mabaki ya mabomu yaliyozagaa mitaani hayawezi kulipuka.
"Ninachowaambia wananchi ni kwamba msiondoke kwenda kokote, mabomu hayawezi kulipuka tena, ila msiyaguse yaacheni hadi askari watakapokuja kuyachukua," alisema.

Mabomu yazagaa ovyo
Mwananchi lilishuhudia mabaki ya mabomu yakiwa yamezagaa ovyo huku mengine yakiwa ndani ya nyumba katika eneo la Gongo la Mboto.
" Wanatuambia tusihame, hivi unaweza kuendelea kulala katika kitanda huku pembeni kukiwa na bomu, wasituletee siasa tunaondoka ili kuokoa roho zetu, " alisema Hamis Chande ambaye nyumba yake imetobolewa na bomu.
Alisema pamoja na bomu kubomoa sehemu ya nyumba hiyo, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika familia hiyo yenye watu watano.

Kina mama, watoto wahaha Dar

Mamia ya wanawake na watoto walionekana wakitembea kwa miguu wakitokea Gongolamboto kwenda katika maeneo mbalimbali ili kunusuru maisha yao.

Kauli ya Wizara ya Afya
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni, aliwataka wananchi waliopatwa na mshituko uliotokana na milipuko ya mambomu hayo, waende hospitali ili wakapimwe afya zao.

"Wito wangu ni kwa wananchi wote ambao kwa namna moja ama nyingine milipuko ya mabomu imewaathiri, wasijifiche majumbani waende hospitali kwa uchunguzi ili kubaini kama wameathirika pia, tumeandaa mazingira mazuri ya kukabiliana na mahitaji yote ya tiba kwa wahanga hao," alisema Nyoni.

Watoto 300 wapotea Dar

Zaidi ya watoto 300 wamepotea jijini Dar es Salaam kutokana na milipuko hiyo ya mabomu, polisi wamesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime aliliambia Mwananchi jana kuwa, katika Uwanja wa Uhuru walikohifadhiwa waathirika wa milipuko hiyo kuna idadi kubwa ya watoto waliopotezana na wazazi wao wakati wakiyakimbia makazi yao.

"Idadi ni kubwa, watoto zaidi 300 hawajulikani walipo, lakini tunafanya kila iwezekanavyo ili kuhakikisha watoto wanapatikana na kuwaleta kwenye makambi ya hapa uwanjani kwa ajili ya kutambuliwa na wazazi wao,"alisema Misime.

Mmoja wa waathirika hao aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Ndwanga alisema alipotezana na watoto wake wawili alipokuwa akikimbia kutoka Pugu hadi Uwanja wa Uhuru.
"Nilipofika hapa nilimwona mwanangu mmoja, lakini sijui hatma ya mwanangu wa pili.,"alisema Mariam.
Uwanja wa Uhuru ndio ulioteuliwa na Serikali kuwa eneo la muda la kuwahifadhi waathirika hao. Tayari mahema kadhaa yamejengwa katika uwanja huo ijapokuwa hayakidhi haja kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuhitaji msaada.

Kamanda Misime alisema wanaendelea kupokea watoto kutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwarahisishia mawasiliano kati yao na wazazi wao.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Shirika la Msalaba Mwekundu, Julias Kejo alisema idadi ya watoto waliopokelewa uwanjani hapo usiku wa kuamkia jana ni 179, ambapo baadhi ya watoto hao walitambuliwa na wazazi wao.
Kejo alisema zaidi ya wazazi 254 waliofika kwenye kambi hiyo ya muda ili kuwatambua watoto hawakuweza kuwaona watoto wao hivyo walilazimika kukaa na kuendelea kusubiri wakati polisi na watu waokoaji wa chama cha msalaba mwekundu wakiendelea kuwaokota watoto na kuwapeleka kwenye makambi.
"Wazazi endeleeni kusuburi kwa kuwa watoto wengi wanaendelea kuokotwa sehemu mbalimbali, na watapoletwa mtaweza kuwatambua watoto wenu ili muweze kuondoka nao mnachotakiwa muwe wavumilivu,"alisema Kejo.

Wizara kuwahudumia waathirika
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nyoni alisema Serikali imejiandaa kutoa huduma kwa waathirika wa mabomu ikiwa pamoja na dawa ,chakula na maji ili kunusuru afya zao hadi watakapotambuliwa na ndugu zao au kupata hifadhi.

"Wengine tangu milipuko ya mabomu ilipotokea hawajala kitu chochote hadi sasa, hivyo Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha waathirika hao wanapata huduma muhimu kama maji, chakula na dawa,"alisema Nyoni.
JK tangaza msiba wa kitaifa

RAIS Jakaya Kikwete amesema mabomu yaliyolipuka kwenye maghala 23 juzi usiku katika Kambi ya Jeshi 511 Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam jana ni Maafa ya Kitaifa.

Akizungumza wakati alipotembelea kambi hiyo, Rais Kikwete alisema kikosi hicho ndio makao makuu ya hifadhi za mahitaji ya kijeshi, hivyo kilichoteketea sio silaha tu, bali hata sare za wanajeshi.
"Haya ni maafa ya kitaifa, kwa sababu kikosi hiki ndio makao makuu ya hifadhi ya kijeshi, ikiwemo silaha na mavazi yao ambayo mpaka sasa hivi naongea vyote vimetekelea kwa moto,"alisema Kikwete.
Aliongeza kutokana na hali hiyo msiba uliojitokeza kwa wananchi, ni msiba wa kitaifa, hivyo basi wapo pamoja nao katika kuomboleza na kuwaondoa hofu juu ya hilo.

Alisema, mpaka sasa Baraza la Taifa la Usalama litafanya kikao ili liweze kujua ukubwa wa tatizo, kisha kuchukua hatua stahiki za kuwaeleleza wananchi juu ya tukio hilo.
"Tumepoteza ndugu zetu, mali za kijeshi ambazo zote zilikuwa zinahifadhiwa humu ndani, lakini mpaka sasa kuna watalaam tayari wameanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo,ninawaomba wananchi watulie ili waweze kufanya kazi yao,"alibainisha.

Kwa mujibu wa Kikwete, baada ya kupata taarifa za milipuko hiyo aliitisha kikao cha dharura Ikulu na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, majira ya saa 9:00 usiku kwa ajili ya kujadili tatizo hilo.
Alisema kutokana na hali hiyo, mkuu wa kambi hiyo, aliwapa taarifa kwamba, maghala hayo yameungua na vifaa vyote vilivyomo ndani yake, lakini askari mmoja ndiye aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
"Kwa taarifa nilizonazo ni askari mmoja aliyejeruhiwa, hivyo basi ninawaomba wananchi waondoe wasiwasi juu ya tukio hilo, Serikali iko pamoja nao kuhakikisha kuwa hatari zilizopo zinadhibitiwa, na kwamba wananchi wanarudi katika hali yao ya kawaida,"alisema Kikwete.

JWTZ yaunda tume
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Meja Generali Abdulrahaman Shimbo alisema wameunda tume ya kijeshi ya kuchunguza tukio hilo na kuokota mabomu yaliyodondoka kwenye makazi ya watu.
Alisema tayari askari wameanza kupita kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kutafuta mabaki hayo ili waweze kuyawasilisha kikosini kwa ajili ya kuyatekeleza.

"Tumeunda tume ya kijeshi ya kuchunguza tukio hilo, na kwamba tayari askari wameanza kupita kwenye makazi ya watu kwa ajilii ya kuokota vipande vilivyobaki ili waweze kuleta kikosini kuyatekeleza,"alisema Shimbo.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wametakiwa kuondoa hofu juu ya tukio hilo kwa sababu hayawezi kulipuka tena, hivyo basi mabomu hayo wawaonyeshe askari hao ili waweze kuyachukua.
Alisema, taarifa zilizotolewa na wananchi juu ya kulipuka kwa mabomu mengine ni uvumi wa uongo, hivyo basi wananchi wametakiwa kuondoa wasiwasi juu ya hali hiyo.

Nauli za Gongo la Mboto zapanda ghafla
Nauli za kuelekea Gongo la Mboto kutoka Ubungo jana zilipanga ghafla kutoka Sh250 hadi Sh1000 kutoka Ubungo.
Nauli ya Bajaji na pikipiki ilikuwa Sh20,000 hadi Sh30,000 kutoka Ubungo kwenda Gongo la Mboto.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema gharama hiyo ni kubwa, na kwamba inawaumiza kutokana matatizo waliyopata.

"Hatuna budi kupanda kwa sababu mpaka sasa tumetembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta usafiri ambao hivi sasa ni gharama na magari hakuna,"alisema Mwajuma Omary(40) mkazi wa Gongo la Mboto.
Aliongeza kuwa gharama ya kukodi pikipiki au bajaji katiya Gongo la Mboto na Ubungo ni kati Sh 20,000 hadi 40,000 wakati nauli ya daladala Sh1000 kwa mtu mmoja.

Alisema kutokana na hali hiyo magari hayo yamepandisha nauli hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo vituoni jambo ambalo limewafanya wapandishe nauli hiyo ghafla.
Nao baadhi yawaendesha piki piki na Bajaji aliozungumza na gazeti hili walisema kuwa, tukio hilo ni sawa na "kufa kufaana", kwa sababu abiria waliopo vituoni ni wengi, jambo ambalo limewafanya wapandishe nauli ili waweze kupata faida zaidi.

"Kufa kufaana,lazima tupandishe nauli ili na sisi tuwezen kufaidika, kwa sababu gharama ya mafuta ni kubwa, na kwamba sisi tunatoa msaada tu,"alisema Juma Abdul(31) mkazi wa Buguruni.

Habari hii imeandaliwa na Alphey Athanas, Hidaya Kivatwa, Edom Mwasamya, Elias Sichalwe, Pamela Chilongola, Patricia Kimelemeta, Hussein Issa na Raymond Kaminyoge
 
Kufikia hitimisho haraka namna hii wengine tunapata wasiwasi, the motive behind andiko lako. Mimi nikuulize kama umeweza kuandika haya yote kwani usipate ushahidi hata wa mwanajeshi mmoja aliyekufa? Hawa wanajeshi wana ndugu, misiba yao lazima itawaguza na ndugu zao. Sasa unataka tuamini kuwa kunamwanajeshi amekufa ndugu zao na waliohudhuria msiba wake wote wafungwe mdomo na serikali wasiseme? Kwanini mbagala waseme kuwa wanajeshi wamekufa na gongolamboto waamue kuwa kimya? Wewe unataka tuamini kuwa wanajeshi wanaweza kukubali vifo vya wenzao viweze kutumika kwa maslahi ya mtu au kikundi cha watu? Pengine unaweza kuwafanya watu wengine kukuamini lakini sio mimi.

Ni rahisi kuficha vifo vya wanajeshi kwa mabomu la Gongo la Mboto kuliko yale ya Mbagala. Ya Mbagala yalilipuka mchana na ingekuwa ngumu kusema kuwa hakuna mwanajeshi aliyekufa wakati wangetakiwa wawe kazini. Yaani hata kichaa asingekuba kuwa hakuna mwanajeshi aliyepoteza maisha yake kwenye mabomu ya Mbagala.

Ya Gongo la mboto yalilipuka usiku na ni rahisi kusema kuwa kilikuwa hakuna mtu. Pamoja na hayo still it does not make sense kusema kuwa hakuna hata mwanajeshi mmoja aliyefariki. Kwanza, ina maana hayo magala ya silaha hayalindwi? Hao wanaoshi huko kambini walikimbiaje? Tumeambiwa mabweni yote ya wanajeshi makapera yaliungua pamoja na vitu vyao vyote lakini hakuna hata mmoja aliyefariki.

Pili hata tuseme hakuna wanajeshi wanaoishi huko kambini lazima wapo wanaoishi eneo la Gongo la Mboto. Ina maana mabomu yalikuwa selective kuua raia wa kawaida? Sina nia mbaya na wanajeshi lakini nashindwa kuelewa how come ripoti zinasema kuwa hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyefariki. Very unusual.

Kama hakuna mwanajeshi aliyepoteza maisha yake then kama alivyosema Hofstede walikuwa wanajua kuwa hayo mabomu yatalipuka muda wowote ule.
 
Tanzania will remain as Tanzania as it is! no body will act and you will never get the truth and there will be no consequences out of it!! it is sad and sickening! Mungu ibariki Tz!
 
Tanzania will remain as Tanzania as it is! no body will act and you will never get the truth and there will be no consequences out of it!! it is sad and sickening! Mungu ibariki Tz!
Wananchi wenzangu huu utamaduni wa kutokujiuzulu mtu hata iweje ni jambo ambalo tunalo nia ya dhati na uwezo pia wa kuubadili kwa kuchukua hatua sasa hivi.

Loyal-Citizen, futa machozi haraka na tuongoze vita mbele!!
 
Back
Top Bottom