Makomandoo wetu wa Tanzania

Makwarukwaru

Member
Mar 10, 2012
66
25
Napata ukakasi sana hasa nikiwaza hichi kitu. Komandoo ni askari aliyepitia mafunzo ya kijeshi na ya hali ya juu mno.

Zamani ilikua ukisikia Komandoo mpaka damu inasisimka na wengi wao katika jeshi letu walikua wanapata mafunzo yao nje ya nchi kama Cuba, Misri na Israel. Je sasa hawa wanaotoka pale Morogoro wana sifa kama zile za wale?

Au ndo wale waliotufanyia show ya kupasua tofali kwa kichwa pale uwanja wa taifa siku ya miaka 50 ya kupata bendera? (Kwani siamini kama bado tuko huru)..
 
Umeulizia wale wanaotoka pale Morogoro tuu?
Wapo makomandoo wetu wengi ambao hupelekwa nje ya nchi kupata mafunzo na wapo fit sana.
Nikutoe shaka, hata wale wanaomaliza pale Morogoro wapo fit mno yaani usije ukafikiria otherwise brother.
Kumbuka Ulinzi wa nchi ni first priority katika nchi yeyote especialy Tanzania, so when it comes to comandos, aisee hakuna utani wala ufisadi kama kwenye madini au mali asili.
 
Napata ukakasi sana hasa nikiwaza hichi kitu.Komandoo ni askari aliepitia mafunzo ya kijeshi na ya hali ya juu mno. Zamani ilikua ukisikia komamdoo mpaka damu inasisimka na wengi wao katika jeshi letu walikua wanapata mafunzo yao nje ya nchi kama Cuba,Misri na Israel.Je sasa hawa wanaotoka pale Morogoro wana sifa kama zile za wale? Au ndo wale waliotufanyia show ya kupasua tofali kwa kichwa pale uwanja wa taifa siku ya miaka 50 ya kupata bendera(kwani siamini kama bado tuko huru)?
Utaumia bure ndugu yangu, mambo mengine waachie wenyewe....:tape2:
 
Nimesema hivyo wandugu kwasababu kuna mtu ameniambia kwa sasa nchi za jirani na sisi wako vizuri mno na wanajifua mno ki military sasa sijui nia yao ni nini...
 
Kwenye suala la jeshi na mafunzo yake acha kabisa hasa ukitaja comando ndio kabisa wale jamAaa hawana kazi ingine zaidi ya mafunzo na kushiriki kwa vitendo sehemu zenye vita wanalinda amani...wamekaa sana lebanon,ivory coast,sudan kusini darfur sanaa..... Wanaenda huko kila leo wanabadilishana tu muda kukaa huko achana nao kabisa!!!
 
Ila kuna mzee moja nilimkuta mlale songea alikua kipofu sio totaly blind alikua anona kwa mbali sana nikaambiwa chanzo chake ni mafunzo ya ukomandoo kwamba zamani walikua na mafunzo ya kutia sugu mikono hasa kwenye tip of the finga kiasi walikua na uwezo wa kuchimba hata ukuta! Bila kujua walikua wanaua nerves ambazo zinz uhusiano na macho kabisa ndo maana akaishia kuwa hivyo,kama kuna mwenye jibu la uhakika katika hili pls...
 
Achan na makomandoo ,mi nimepitia madojo si rasmi tokea enzi za miaka 80 -kwa watu wa dar watawakumbuka akina kiringo , Santana , (MwambaZero Jimmy Castro- marehemu hawa )Abdala Master sikuwa na rank yeyote zaidi ya kuwa najua kutifua ugomvi wa haja, miaka ya mbele uzeeni kwangu nika kutana ni vijana na mikanda yao kamasi ziliwatoka nawengine wakijidai wamechukua mafunzo kutoka nje au walimu wa nje.
In short wale vijana pale morogoro usiwatanie ni wadudu kamili ktk mpango wa vurugu.
 
Dah safi sana kiongozi.
 
Ila kuna mzee moja nilimkuta mlale songea alikua kipofu sio totaly blind alikua anona kwa mbali sana nikaambiwa chanzo chake ni mafunzo ya ukomandoo kwamba zamani walikua na mafunzo ya kutia sugu mikono hasa kwenye tip of the finga kiasi walikua na uwezo wa kuchimba hata ukuta! Bila kujua walikua wanaua nerves ambazo zinz uhusiano na macho kabisa ndo maana akaishia kuwa hivyo,kama kuna mwenye jibu la uhakika katika hili pls...

Haiwezi fanyika oversight ya ki hivyo.....
 
Morogoro ni sehemu tu ya training ya Awali ambao hata walinzi wa viongozi wanakwenda >baada ya pale kuna Zanzibar halafu ndo nje.Lakini hilo zoezi linalopigwa Mor si la kitoto.Wale jamaa kwa siku nadhani wanakimbia 40-50 km, kuogelea umbali nusu ya huo na mambo mengine mengi sana.Akikupa moja lazima ukae chini
 
napata ukakasi sana hasa nikiwaza hichi kitu.komandoo ni askari aliepitia mafunzo ya kijeshi na ya hali ya juu mno. Zamani ilikua ukisikia komamdoo mpaka damu inasisimka na wengi wao katika jeshi letu walikua wanapata mafunzo yao nje ya nchi kama cuba,misri na israel.je sasa hawa wanaotoka pale morogoro wana sifa kama zile za wale? Au ndo wale waliotufanyia show ya kupasua tofali kwa kichwa pale uwanja wa taifa siku ya miaka 50 ya kupata bendera(kwani siamini kama bado tuko huru)?

kaka umesema kweli kabisa hawa jamaa ni wachovu sana nakushauri siku ukiwaona waambie live,
ila kabla ya hapo hakikisha umefanya yafuatayo
1. Umeandika urithi wako vizuri
2. Umevaa helmet
3. Kunywa dawa za maumivu mapema
4.
lipa madeni yako(binafsi +mgao wako kwenye deni la taifa)
5. Nunua sanda na jeneza lako mwenyewe usituachie gharama ni vema ukienda huku umevaa sanda kabisa
6. Chimba kaburi lako mwenyewe
7. Acha taratibu za usafiri wa mwili wako vizuri
8.
kodisha wa2 wakukulilia
9.ungama dhambi zako
10. Nk

siku nyingine bwana mdogo usichezee taaluma zinazotumia akili nyingi na nguvu nyingi.

Rip
 
bila shaka utakua moja wao maana badala ya kunifafanulia with facts kama wenzako wewe unanitisha!!!
 
Wana bodi.
Hawa makomandoo wa Tz si tuliwaona uwanja wa taifa jinsi wanavyopasua tofali kwa kichwa.
Yani wana mambo ya miaka ya 47, wakati wenzao wapo kwenye level za SEAL...
 
na wakitoka zanzibar wanakuja kufundishwa kulenga shabaha wakiwa mwendokasi wa spidi 200 kwa saa kwa kutumia boti maalum kutoka china,nna maana baada ya hapo wanauwezo wa kusimama na kulenga shabaha sahihi kwenye mwendo huo popote pale kwenye gari,majini au hata treni
msiwachezee waoneni kama wanawakiwa hivyo hivyo na hawafanyi kitu bila ya amri kama askari magereza walivyo na nidhamu ya juu
 
Wana bodi.
Hawa makomandoo wa Tz si tuliwaona uwanja wa taifa jinsi wanavyopasua tofali kwa kichwa.
Yani wana mambo ya miaka ya 47, wakati wenzao wapo kwenye level za SEAL...

hahaha wanapasua mawe kwa vichwa! U made my day.
 
mkuu usiwe na mashaka sana, vijana wako sawa kule hakuna siasa.
Lengo la maonyesho halikuwa kutisha watu, bali zaidi ni kusherehesha, na kunogesha sikukuu.

Kama hawa mabwana wakifanya vitu serious tegemea yafuatayo
1. Dar haitakalika
2. Majirani zetu na maadui + mataifa ya nje watajua yale wasiyotakiwa kujua

note: Wataalamu wa kijeshi wa mataifa wanaweza kuusoma mchezo kwa kumuangalia mwanajeshi jinsi anavyo tembea, shika siraha, ruka na kujua mengi kuhusu kikosi cahke haya lazima yazuliwe yasitoke nje
 
Hata mimi awali nilikuwa nafikiri hawa wa kutoka Morogoro si lolote si chochote.
Niliwahi kukutana na mmojawapo kule Pemba, ingawa kwao ni huku Bara, aliwahi kufanya kitendo kwa vijana fulani wanajeshi walikuwa na chuki na sisi watu kutoka bara, nikaamini kweli wana mafunzo ya kutosha. Mengine huwa nayaona kwenye picha za akina Rambo, lakini niliyashuhudia kwa huyu rafiki yangu mara tatu.
Ni hatari na hakuna sababu ya kuwa na shaka na uwezo wao.
 
Back
Top Bottom