Making Him/Her ..a husband/Wife and a Friend

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Wapenzi natumaini wote mu wazima.
Nimekuwa nikisoma mawazo yenu hapa jamvini juu ya mahusiano na kujikuta nachanganyikiwa zaidi ya kuwaelewa. Picha niliyoipata kwa muda ni kutomfanya mpenzio kama mume/mke wako bali awe rafiki. Nilikuwa na mawazo potofu kuwa kunyenyekea, kuenzi mpenzi ndio njia ya kumfanya aelewe kuwa ninampenda but reactions za wengi ilikuwa ni no, no and no. Soulmate aligoma kuvuliwa viatu lol, Lizzy akagoma kunyimwa unyumba....................matokeo yake ni kuwa tunashauriwa mume/mke wako awe rafiki yako, rafiki zaidi ya mume/mke.

Najiuliza how do we make/turn our spouses/partners your friend?? Na wakati gani huu urafiki unaanza kujengwa, tukiwa marafiki au tukiwa tushakula viapo?

Making him/her your friend than your spouse.
 
Samahani sijui kama nimeuliza sawa, natanguliza samahani zangu but nilikuwa ninahisi kuwa one of the ways ya kumfanya mwenzi wako kuwa rafiki ni kuwa karibu yake na kujua yaliyojiri kwake kwa siku nzima mf. kuwa na desturi ya kudiscuss yaliyotokea wakati hamko pamoja au?
 
Ila heading ina utata kidogo, mimi ninasupport 'a husband who is also a friend'.
 
does being a husband spouse negate being a friend ?, I guess mtu anaweza kuwa vyote bila tatizo as rafiki anakuwa mume/wife..

Rafiki as you share everything na hakuna siri, mpo comfortable na kila mtu na mnaenjoy hobbies zenu wote.

Mume / mke as kuwa na heshima na kutokuvunjiana heshima yaani kumpa kila mtu nafasi yake.., kuna mambo unaweza kumfanyia rafiki yako lakini kamwe sio mume/wife.., as there are things you share which only a wife/mume can do
 
unafanya nini na unaishije na mtu mnaekutana ambaye si ndugu yako wala sio mpenzi? kama ambavyo una interact na ur best friends the same uinteract na ur boyfriend/galfrnd au wife/husband, kama ambavyo hupendi kuwapoteza marafiki zako ktk maisha ndivyo hvo hvo ufikirie kuhandle uliyenae the same way
 
nadhani huu urafiki unatakiwa ujengwe wakati mpo wachumba,yaani unamchukulia kama rafiki zako wengine tofauti kidogo kuwa yeye mtashare intimancy, ulivyo huru kwa waskaji wengine na kwa mme iwe hivyo hivyo,
 
Mamii kumfanya mtu rafiki ni kumfanya awe huru na wewe, na wewe uwe huru nae. Yani mnaweza mkaongea lolote (umbea usiwe mwingi) kwa uhuru, waweza kumweleza mambo yako akakusikiliza na kukupa kile unachohitaji kutokana na hilo jambo (faraja, support,mawazo na ushauri, na mengineyo).

Fikiria unavyokua na ndugu yako ambae unamwona kama rafiki na unavyokua na ndugu yako ambae ukaribu wenu unaishia kwenye undugu. . .Tofautisha mahusiano yako kati ya hao wawili, lazima kuna tofauti. Hivyo sasa!!!

Na muda mzuri wa kuanzisha huu urafiki ni tangu mwanzo wa mahusiano maana mkishazoea
Mama. . . "Shkamoo baba"
Baba. . ."Maji ya kuoga tayari?!"
Mama. . ."Ndio"

Na maongezi yanaishia hapo ni ngumu kuja kuanza urafiki. So. . .the earlier the better.
 
jamani Mwanajamii huko mnakompeleka siko,mme ni kichwa cha nyumba,lazima asikilizwe,aenziwe ndo nyumba itakuwa nyumba.Msitake kuleta mambo ya familia ya kambare hapa ambapo kila mtu ana sharubu.

Kwani ukiwa rafiki ndo heshima hamna? Acha hizo wewe. . .
Alafu kesho nakuja na thread ya Wanaune wa kiMassai nadhani utaipenda usotaka urafiki kati ya mke na mume.
 
Nadhani na naamini mume na mke wanapaswa kuwa marafiki. Kama alivyosema Lizzy uhuru ni jambo muhimu! Sasa inategemea mlianzaje! Mmepishanaje umri? Mnachukulianaje? Etc
 
Nadhani na naamini mume na mke wanapaswa kuwa marafiki. Kama alivyosema Lizzy uhuru ni jambo muhimu! Sasa inategemea mlianzaje! Mmepishanaje umri? Mnachukulianaje? Etc
 
Kaunga,Mrembo na Marry ( namwongezea na Lizzy nimemsoma hapa chini),jamani Mwanajamii huko mnakompeleka siko,mme ni kichwa cha nyumba,lazima asikilizwe,aenziwe ndo nyumba itakuwa nyumba.Msitake kuleta mambo ya familia ya kambare hapa ambapo kila mtu ana sharubu.

Bishanga bwana, sasa ukiwa kichwa cha familia ndio uwe adui (kinyume cha rafiki); look at ur relation with Kongosho na Lizzy, huoni kuwa mzaha/utani au uhuru kama huo ukiwa nao na mkeo, usipokuwa naye for few hrs unammiss?
 
Last edited by a moderator:
Mie nna neno la zaidi ya rafiki, 'mshkaji'. Mwenza anapaswa kuwa mshkaji wako. Its easy, akifanya jambi jiulize angefanya hivi babu dark city ningenuna? Ningesusa? Don't fuss around, jali feelings zake (mfano hata kama umekasirishwa kazini, would u take it out on king'asti?)

Many times tunajikuta tunawajali marafiki kuliko hata wenza wetu. Kuliko kutumia wakati wako na wengineo wasio-matter, why not kwa partner wako? (Muambie soulmate wako nae aache ushamba, viatu raha yake kuvuana banaa! Kuna zile evening dresses ukiinama kufungua viatu litapasuka kama pazia la hekaluni,lol)
 
Kwani ukiwa rafiki ndo heshima hamna? Acha hizo wewe. . .
Alafu kesho nakuja na thread ya Wanaune wa kiMassai nadhani utaipenda usotaka urafiki kati ya mke na mume.
unaleta udot com eh?si ndo hizo ndoa fasta wiki vimebaranguka?
 
Bishanga bwana, sasa ukiwa kichwa cha familia ndio uwe adui (kinyume cha rafiki); look at ur relation with Kongosho na Lizzy, huoni kuwa mzaha/utani au uhuru kama huo ukiwa nao na mkeo, usipokuwa naye for few hrs unammiss?
kwani mimi nawamisi konnie na Lizzy? Waende zao huko.
 
Last edited by a moderator:
Napenda na naamini inatakiwa kuw ahivyo
Kuwa rafiki na mwenza wako sidhani kama inaondoa ile heshima ya mwenye nyumba au inapunguza lolote kwenye heshima
bado yale ya kuwa wewe ni baba mwenye nyumba yapo tuu na hayatapungua na hayo ni wakati mkiwa pamoja
Maana sidhani kama mnaweza taniana au kuongea mambo ya ndani mbele ya house gal na watoto
Ni nzuri sana unapompa mwenza uhuru wa kujua kuwa yuko free mbele yako kuongea na kutaniana na wewe
Kuliko kuwa na ule uso wa mbuzi kila siku hakuna utani wala kujadiliana
Nafikiri hivyo kw aupande wangu (Bishanga please usiongeze neno)
 
Back
Top Bottom