Makinda "tayari" bado werema, muungano ni dhaifu kuliko wakati wowote uliopita "tundu lissu"

Ni pale aliposhindwa kuunganisha zanzibar na tanganyika kwa kuwatenga wahanga takribani 280 wa ajali ya meli kuzama kanakwamba ni "wazanzibari" mbaaaaaaali kabisa kuleeeeeeeee, na si chamwino wala karibu na dodoma (bara)!!!!
Akakataa hoja ya HAMADI RASHIDI mbunge kutoka zanzbar, kulitaka bunge liahirishe shughuli zake kutokana na kadhia hiyo na kukubali Emanuel Nchimbi mbunge na waziri kutoka bara aichomoe hoja mezani ili kulinyima bunge shughuli ya kufanya na kupelekea kuahirisha, ieleweke hapa kuwa bunge lilikosa cha kufanya, hapakuwa na hoja mezani!!!!!!!!

Kwa wasiofahamu, watambue sasa kuwa Tundu Lissu (munyampaa) alipata kuliambia bunge kuwa muungano wetu ni dhaifu kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya tanzania,
HEBU ONENI UDHAIFU HUU KUTOKA KWA KIONGOZI MKUU WA MUHIMILI!!!

Wafuatao walimpinga tundu lissu hadharani kwa nguvu na vijembe vikali hadi kufikia habib mnyaa kutafsiri jina tundu lissu "kizenji"

1) habib mnyaa
2) anna makinda
3) hamadi rashidi mohamed
4) selina kombani
5) jussa ladhu (spelling correction allowed)
6) . . . . .
7) . . . . .
8) . . . . .

Tukumbushane hivi Werema hajawahi tumbukia kwenye shimo alichimbalo kweli?

Please do me a fever niwekeeni ile pic. Makinda akicheza muziki na Tundu Lissu!
Yanayojiri baada ya MNYIKA (MB) kufika Polisi Singida!

weeweee, Lissu anamchezesha makinda muziki wa "muungano ni dhaifu saaana" makinda anaonekana kuufurahia sana!!!!
Kwa nini mlitaka Bunge liahirishwe badala ya kuzungumzia ajali ile na jinsi gani bunge linaweza kusaidia haraka iwezekanavyo kuokoa maisha ya wananchi?.

Wakati wa 9/11 Marekani watu walikuwa makazini na hakuna mahala waliacha kazi, sii ofisi za serikali wala mabunge ya states lakini tume, taasisi an asasi za kiserikali zilitishwa haraka mkutano kujadili tatizo lilokuwepo. Walioweza walienda moja kwa moja kwenda kuokoa sasa hawa wabunge walipoahirisha bunge walifanya nini cha maana ambacho tunaweza kukiwekea mfano kwamba Makinda ndiye alisababisha kisifanikiwe..
 
Tangu lini tukawaigiliza Marekani? Ingekuwa hivyo si watu wa EPA wangekuwa wanaozea Keko kama Ben Madoff?
 
Kwanza kabisa kama wewe ni mzanzibari, mtuwie radhi wabara kwani mawazo yake si yetu wote na mi binafsi kanikwaza nafikiri patriotism ya chama kwake ni kubwa kuliko ya nchi matokeo yake ndo hayo, sijui 2015 watatokea wapi hawa halafu jambo lenyewe limetokea kipindi hiki cha kutoa maoni juu ya mwali mtarajiwa(katiba)

Na kweli mpuuzi mmoja anaweza akatufanya tukaonekana sisi wabara ni wamoja kumbe ni ukurupukaji na ubinafsi wa lichama lao lilikosa mwelekeo na mvuto kwa waTz
 
IMG_4291.JPG

Jamaa hakwenda kulamba mzigo siku hiyo kweli maana si ni wa wote hana mwenyewe!
 
Makinda and Ndugai are incompetent for the post of the Speaker na hao wana mchango mkubwa sana ktk kulivuruga Bunge na kuiweka CCM ktk wakati mgumu zaidi 2015.

Hiyo ndo njema yetu wapenda mabadiliko na maendeleo
 
Kwa nini mlitaka Bunge liahirishwe badala ya kuzungumzia ajali ile na jinsi gani bunge linaweza kusaidia haraka iwezekanavyo kuokoa maisha ya wananchi?.

Wakati wa 9/11 Marekani watu walikuwa makazini na hakuna mahala waliacha kazi, sii ofisi za serikali wala mabunge ya states lakini tume, taasisi an asasi za kiserikali zilitishwa haraka mkutano kujadili tatizo lilokuwepo. Walioweza walienda moja kwa moja kwenda kuokoa sasa hawa wabunge walipoahirisha bunge walifanya nini cha maana ambacho tunaweza kukiwekea mfano kwamba Makinda ndiye alisababisha kisifanikiwe..

Jiulize ilikuwaje Makinda baadaye alikatisha shughuli za Bunge? Aligundua kitu gani tena na wakati alishafanya maamuzi?
 
hiyo ndiyo busara ambayo mnampandikizia kuwa nayo huyu mama ambayo angelishauri bunge kama mbadala wa pendekezo la kuahirisha kikao, ndiyo maana chadema wanapopeleka bungeni bajeti mbadala huwatoa kwenye mjadala wa bajeti ya serikali na kuanza kuijadili bajeti mbadala na kusahau kuishauri na kuielekeza serikali ya ccm. Hatimaye tunajikuta tuna bajeti jk na kundi lake huduma za afya kutengewa karibu mara mbili ya bajeti ya walala hoi.
 
Watanzania tusiumize kichwa juu ya huyu mama na msaidizi wake! tatizo hapa ni gamba! wangezama kule jimboni Iringa angesubiri waheshimiwa wabunge waombe kuahirishwa kwa bunge au angeondoka bila hata kuahirisha wala kuaga! amechemsha sana! Wazanzibar na wabara sote tupo pamoja katika raha na shida.:A S cry::A S cry:
 
Jiulize ilikuwaje Makinda baadaye alikatisha shughuli za Bunge? Aligundua kitu gani tena na wakati alishafanya maamuzi?
Kwa sababu gani? sasa mkikutana wote mna mawazo sawa yeye ataweza vipi kufikiria nje ya mawazo yenu?. BInafis yanug wlaa simtetei Makinda kwa sababu sielewi yeye alitaka kifanyike nini lakini kwa ujumla wake hata kuvunja Bunge ili kurudi mahoteli na kulia saana sijui imesaidia nini..
FJM;Tangu lini tukawaigiliza Marekani? Ingekuwa hivyo si watu wa EPA wangekuwa wanaozea Keko kama Ben Madoff?
Ndio nachoongelea sii kuiga Marekani isipokuwa kwa nini sisi kila kitu tunafanya kinyume hata maamuzi yetu ni ya ajabu ajabu..Tazama nchi kama Greece imepata matatizo ya Kiuchumi EU ndio wamegharamia hatukuona IMF lakini ije Afrika hata bila matatizo nchi yetu lazima ikachukue ushauri na kupangiwa mikopo IMF wakati wanajua wazi kwamba tutapewa masharti ili nchi tajiri zirudi kutawala uchumi wetu, na tunapongezana kwa kuvuta nyingi zaidi.
 
Haha, huyo babu hapo pembeni haamini, alijua tundu lisu anatafuta kinacho fanana na jina lake. Huyu kijana wa town bwana acha kabisa. kamanda huyo.
 
Kwa sababu gani? sasa mkikutana wote mna mawazo sawa yeye ataweza vipi kufikiria nje ya mawazo yenu?. BInafis yanug wlaa simtetei Makinda kwa sababu sielewi yeye alitaka kifanyike nini lakini kwa ujumla wake hata kuvunja Bunge ili kurudi mahoteli na kulia saana sijui imesaidia nini..
.
Mkuu labda hapa hatuelewani. hebu niambie unafikiri kwa nini Bunge lilikatishwa baada ya ajali hiyo? Ili Wabunge wakashiriki katika uokoaji? hebu niambie wewe mkuu unafikiri kwa nini Bunge lilikatisha shughuli zake?
 
Umeona eee! Huyu mama hajijui kabisa. mimi naona anawaaibisha tu wanawake wenzie badala ya kuwa kioo chao
 
Mkuu labda hapa hatuelewani. hebu niambie unafikiri kwa nini Bunge lilikatishwa baada ya ajali hiyo? Ili Wabunge wakashiriki katika uokoaji? hebu niambie wewe mkuu unafikiri kwa nini Bunge lilikatisha shughuli zake?
Mbunge sio Zimamoto, lifeguard wala mwana usalama ni mkata issue kwa siasa kupitisha sheria na kujadili matumizi ya serikali. Kujadili maswala kama haya na kuyapatia ufumbuzi.
Walipoahirisha Bunge sikuona sababu na wala sioni sababu iwe wabunge wa vyama vya Upinzani, CCM au Makinda nachotaka kuelewa walipovunja Bunge waliweza vipi kusaidia uokoaji..Ama walirudi mahotelini mwao na kuanza kupiga simu wakati sii Watendaji wa serikali yaani sielewi nini hasa sababu ya kuvunja wakati Emergiency ipo mezani! Unaikimbia au unakabiriana nayo?
Waziri wa mambo ya ndani mh. Nchimbi alikuwepo bungeni hapo ndipo alitakiwa kubanwa na maswali maana Meli imetokea Dar..
 
Nimesoma maelezo ya Candid Scope inaonyesha mkuu wangu jogi umejaribu kuupotosha Umma hapa. Mbunge wa Wami alilitaka bunge lijadili swala la ajali na Makinda ndiye aliyekataa kujadili swala hilo na sii kwamba Hamad Rashid alitaka bunge liahirishwe..

Kwa hiyo ulituchanganya wengi kiasi kwamba nikaziweka lawama zangu kwa wabunge wa upinzani kumbe kilichotokea ni kinyume...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom