MAKINDA: Swala la Lema sitalirudisha bungeni (Amehofia nini?)

Hamna kitu kama hicho,yule mama ana umuhimu wake mkubwa tayari kwetu wanawake,ndo kwanza ameanza kazi, si rahisi kuwa spika wa bunge kama la sasa.....
watu wako tu kwenye PC zao wanaandika as if ingekuwa wao wangeweza zaidi,Makinda is more of a man kuliko wanaume wengi wanaosahau kuwa yeye ni binadamu na anakosea pia.....let her be,mng'oeni Ngeleja kwanza na Pinda ndo muende kwa yule mama.....si kujitafutia umaarufu kwa yule mnayemuona dhaifu na pengine kwa kuwa ni mwanamke.....Pinda has to go first and not Makinda.....

getrude mongela alifanya nini kule bunge la africa?namuona makinda anafuata nyayo za mwanamama mwenzake.
 
Akili zako kama m.a.k.a.l.i.o
Huwezi kuhalalisha mauaji ya watu wasiokuwa na silaha. Siku ukifiwa na mtu wako wa karibu jaribu kufananisha na kama hawa ndugu wa arusha walivyouawa, au ukifiwa na mwanao, mkeo, baba yako, mama yako,....., nasema tena "*.,*

Wakati mwingine kusema neno au jina sahihi la kitu ni bora zaidi kuliko kutumia lugha ya kupotosha au ya kificho. Napenda kusema kuwa hakuna neno "makalio" katika Kiswahili ila ****** na ndivyo tunatakiwa kuyaita.
 
bila shaka amemuepushia mtoto wa mkulima kulia tena bungeni, cunajua akibanwa hana hoja zaidi ya kulia!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Anamatatizo mengi huyu mama ni bora akae pembeni maana huko mbeleni sijui kama ataweza mchakamchaka
 
Kweli kabisa! Hapo umenena! CHADEMA hasa ndio walisababisha hiyo tafrani ya Arusha. Pia kuna ushahidi dhahiri kwamba CHADEMA imekuwa ikila njama na wafanyabiashara ili bei za vitu mbalimbali zipande, JK na CCM waonekane hawafanyi kazi. ni wazi pia wao ndio wanachochea migomo vyuo vyote vilivyogoma. na pia kuna watu wao kule hazina wanakula njama mishahara icheleweshwe ili wafanyakazi nao wagome! yaani we acha tu, hawa CHADEMA! unajua hata kule DAWASA wamejiingiza, maji hayapatikani. hata kule Mtera, walikula njama na yule jamaa anayefungulia bwawa, maji kayafungulia yamekwisha yoote! ndio huu mgao wa umeme unatuumiza. nimepata tetesi hata hii milipuko ina mkono wa CHADEMA! nadhani tuilaani CHADEMA na tuandamane ili ifutwe kwenye daftari ya msajili wa vyama, baada ya hapo nadhani tutaishi raha mustarehe na Maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana!

Lugha yako ni tamu sana kwa mwenye kuelewa, ina sanaa nzuri, nadhani jamaa kaumbuka kwa kusingizia Chadema vitu visivyo kweli.
 
ambacho sijajua ni kwamba baada ya kuupitia huo ushahidi atafanya nini? je, atatoa uamuzi kwamba ushahidi wa lema si sahihi na anastahili adhabu? na je,wabunge watamhukumu Lema bila kuuona na kuusoma huo ushahidi? na je, akiuona ushahidi wa Lema ni kweli,atafanyaje? kubwa zaidi, atausoma na kuufanyia uamuzi peke yake?
 
PM yuko sahihi kabisa na hakusema uwongo, nyie CHADEMA mliisha pewa agizo la kuacha maandamo, kwa utovu wenu wa nidhamu, kujitafutia umaarufu kwa gharama za maisha ya watu na kujifanya wajuzi kama sio wajuvi, ndiko kuliko sababisha mauaji na vurugu za Arusha.

Crap,

You are Genius Bomu.
 
Usitake ionakane wanawake hawawezi Mheshimiwa!!

Wanawake wanaweza wakipata nafasi kwa kuzingatia uwezo binafsi wa mtu na sifa stahiki. Lakini siyo kwa mizengwe na kubebwa bila kuwa na sifa wala uwezo. Tuna mifano ya wanawake wengi walioweza bila kubebwa wala kupendelewa (mfano Profesa Tibaijuka).
 
Kwa maneno haya ya spiker Ana makinda anataka
kuwaambia nini watanzania na watu wa Arusha?
Je hii sio mwanzo wa kushindwa kuliendesha bunge?
Je atahimili au yeye ndie atakuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani? Nawasilisha :source magazeti ya Leo.

Tumpe muda Mh Spika na jopo lake wapitie utetezi na kisha watatoa maamuzi.

Kuwa na Subra
 
Kama fomu ya uspika alichukuliwa na mafisadi wakampelekea njombe aijaze unategemea nini???lazima alipe fadhila hana lolote huyo mama.....amewekwa kulinda mafisadi na yeye fisadi mkubwa ametutia aibu wana iringa

Huyu hatoki Iringa tena mkuu; mafisadi wenzie wamekwisha mtengenezea mkoa wake kule Njombe; NJOLUMA!!
 
Kauli kwamba hatalirudisha hili swala bungebi imekosa uzalendo na imejawa na muhemko wa kisiasa.Kwamba akirudisha bungeni pengine Lema tashinda na wakati yeye hataki kuona hilo likitokea.

Anasahau kwamba yeye ndo alimwambia lema kwamba """ Ni lazima tuwe na heshima hapa bungeni ,kweli kwa waziri mkuu na ahadi alizoweka anaweza kudanganya? nakupa siku tano uje uwasilishe ushahidi wako hapa bungeni '''' akamsomea na adhabu ambayo angeipata kama angeshindwa kuthibitisha.

Lema na jopo la CDM wakajipanga.Mwanasheria Tundu Lissu na Mnyika wakatambua sentensi 23 zinazoonesha kwamba waziri mkuu alilidanganya bunge na taifa.

Mojawapo ya sentesi ni kwamba wakati waziri mkuu anasema waliokufa ni watanzania 3 ukweli ni kwamba waliokufa ni watanzania wawili na mkenya mmoja.Hivyo toka tukio limetokea waziri mkuu amekosa takwimu sahihi.Sio mtu makini.

Ni wazi makinda atatumia ubabe kuzima swala hilo lakini ni vizuri akatambua kwamba Bunge ni kubwa kuliko tofauti au misimamo yetu ya kisiasa.Ni vizuri akaeshimu haki kwani haiombwa bali kudaiwa.
 
PM yuko sahihi kabisa na hakusema uwongo, nyie CHADEMA mliisha pewa agizo la kuacha maandamo, kwa utovu wenu wa nidhamu, kujitafutia umaarufu kwa gharama za maisha ya watu na kujifanya wajuzi kama sio wajuvi, ndiko kuliko sababisha mauaji na vurugu za Arusha.

Mfia CCM utamgundua tuu kwa kukurupuka kulinda uchafu wa chama hata kama upo bayana, naona upo tayali kubishana hata kima ukweli upo wazi, tuwe wa kweli Pinda kalidanganya bunge na ushahidi umetolewa waziwazi na Lema, kama Lema amemkashifu Pinda nadhani atachukuliwa hatua za kinidhamu mda si mrefu, lakini ukiona Lema haadhibiwi ujuwe anayetakiwa kuadhibiwa ni Pinda na kwasababu sheria Bongo sheria zipo biased nina kuhakikishia Pinda hato omba radhi wala kuadhibiwa
 
ME nadhani Anna Makinda ajipange tu kuachia ngazi kwa hayo anayoyafanya mmmmh siju kama atamaliza 2yrs kwenye ichokiti kwani vurugu zitatokana na yeye kwa jinsi atakvyo lipeleka bunge. Umakini na uadilifu ukimpiga tu chenga basi ndio mwisho wa Amani wanao ililia kila siku bila kuitendea haki na hiyo dhambi itawasurubu wao na sio Raia ngojeni mtakuja ona tuuu.
 
Makinda anafikiri watanzania mpaka sasa ni
mabwege hakuna ***** Tena sasahivi. Yeye tayari
ameshajiunga na makamba kuhakikisha ccm inakufa na
kuzikwa, natoa wito kwa watanzania tusimvumilie
makinda na madudu yake.
 
Makinda hoja ya lema watanzania wote
umetukasirisha umeahirisha bunge bila
kufanya jambo hata moja la muhimu
 
Back
Top Bottom