MAKINDA: Swala la Lema sitalirudisha bungeni (Amehofia nini?)

Hamna kitu kama hicho,yule mama ana umuhimu wake mkubwa tayari kwetu wanawake,ndo kwanza ameanza kazi, si rahisi kuwa spika wa bunge kama la sasa.....
watu wako tu kwenye PC zao wanaandika as if ingekuwa wao wangeweza zaidi,Makinda is more of a man kuliko wanaume wengi wanaosahau kuwa yeye ni binadamu na anakosea pia.....let her be,mng'oeni Ngeleja kwanza na Pinda ndo muende kwa yule mama.....si kujitafutia umaarufu kwa yule mnayemuona dhaifu na pengine kwa kuwa ni mwanamke.....Pinda has to go first and not Makinda.....

Na wewe dada nilikuwa nakuheshimu sana. penye ukweli ni vizuri ukausimamia sio kushabikia makinda kwa vile ni mwanamke mwenzio. Hivyo unaonyesha udhaifu sana dada yangu. Muungwana husema yale yaliyo na ukweli na kuyasimamia. Ukweli Makinda Hili bunge litamshinda we subiri.
 
Ni dhahiri Makinda amegundua ya kuwa jazba zake zitampeleka kubaya.............................Lema alichomba ni mwongozo lakini yeye Anne akaamua kumlazimisha Lema amtuhumu Pinda kuwa kasema uongo wakati sivyo..........................Lema alichoomba ni mwongozo tu wa nini kifanyike wakati Mheshimiwa Mbunge amegundua ya kuwa PM amelidanganya Bunge........................................

Spika angelikuwa mwangalifu angempa Lema mwongozo siyo kumlazimisha kumtuhumu PM wakati hata hansard zinathibitisha ya kuwa hakufanya hivyo............................Jitihada za Mnyika kumnusuru Spika hazikuzaa matunda kwa sababu Anne Makinda alifikiri kwa wakati ule hili suala lingempa umaarufu wa bei ya chei baada ya kukutana na washauri wake wa karibu amegundua ni yeye na PM sasa wako kikaangoni..........................................kwa sababu ni ukweli usiopingika ya kuwa Pinda alisema uongo Bungeni alipodai Chadema ndiyo chanzo cha vurugu Arusha wakati hakuna ushahidi wowote ule alioutoa Bungeni kuthibitisha tuhuma yake hiyo....................

Kulingana na kanuni za Bunge huo ni uongo...................................

Anachofanya Anne hivi sasa ..........ni damage control................................lakini hilio bado litamlazimu Pinda aliombe radhi Bunge kwa kusema uongo kwa maana ya kutoa tuhuma dhidi ya Chadema huku hakutoa ushahidi wowote ule......................

Hapo kwenye RED, kama huo ndo uwongo wenyewe wa PINDA basi tunapoteza muda hapa. Na ni bora kodi yangu isitumike kujadili huo utumbo! NImekuwa nikiuliza mara kwa mara hapa Pinda kadanganya nini, kumbe ni Kusema Chadema ndio chanzo cha vurugu Arusha! Mbona huo ni ukweli tu. Chadema wanaandama agains agizo halali la polisi, polisi wanawazui kwa kutumia nguvu, vurugu zinatokea! Sasa hapo chanzo ni nani kama sio Chadema! Acheni ushabiki wa KIPUUZI!
 
Na Romana Mallya



17th February 2011

















Lema%283%29.jpg

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema)



Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema uamuzi kuhusu suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema), hautarudishwa bungeni na badala yake anakusudia kulimaliza mwenyewe.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu uamuzi wake baada ya Lema kuwasilisha vielelezo vyake vya kutetea hoja yake kama alivyotakiwa na Spika.
Alisema taratibu zinazoendelea ni za ndani na hataziweka hadharani kuanzia sasa kwa kuwa ana uwezo wa kulimaliza mwenyewe.
“Jana (juzi) Lema aliwasilisha vielelezo kimaandishi kama Bunge lilivyomtaka, kuhusu hatua gani atachukuliwa, hizi ni taratibu za ndani siwezi kuziweka hadharani,” alisema.
Lema alitakiwa kutoa ushahidi wa alichokisema baada ya kuomba mwongozo wa Spika akitaka kujua hatua ambazo mbunge anazoweza kuchukuliwa iwapo atagundua kiongozi mkubwa wa serikali kama Waziri Mkuu, amelidanganya Bunge.
Akitoa ufafanuzi wa mauaji yaliyofanywa na polisi Arusha Janauri 5, mwaka huu, katika kipindi cha maswali na majibu siku hiyo ya Alhamisi iliyopita, Pinda alisema Chadema ndiyo chanzo cha vurugu hizo kwani walikataa ushauri waliopewa na polisi.
Pinda alikuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, (Chadema) kutaka kusikia kauli ya serikali juu ya mauaji hayo, kama serikali ilikuwa tayari kuunda Tume kuyachunguza na kuwawajisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema.
Katika maelezo yake, Pinda pamoja na kueleza kusikitishwa na mauaji hayo huku akisema hayakuwa na sababu, aliwalaumu viongozi wa Chadema kwamba walikuwa kiini cha kutokea kwake kutokana na kukaidi ushari wa polisi wa kutumia ruti (barabara) waliyoelekezwa.
Pia alisema chama hicho kiliwahamasisha wananchi kwenda kuvamia kituo kikuu cha polisi cha Arusha ili kuwakomboa viongozi wa chama hicho waliokuwa wakishikiliwa hapo kwa kushiriki maandamano.
Baada ya majibu ya Pinda ndipo Lema aliposimama na kuomba mwongozo wa Spika, lakini Spika hakuridhika na maneno yaliyotolewa na Lema hivyo akampa siku tano awe amewasilisha ushahidi wa kile alichosema.
Lema aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni namba 64 ya Bunge kutaka kufahamu iwapo Waziri Mkuu atakuwa ametoa maneno ya uongo bungeni, Mbunge anapaswa kuchukua hatua gani kuhusu suala hilo.
Spika Makinda akitumia kanuni namba 63 na vipengele vyake vyote vinane, alimtaka Lema kuwasilisha uthibitisho kwamba Waziri Mkuu alikuwa ametoa maelezo ya uongo bungeni alipokuwa akielezea kiini cha mauaji hayo na alimtaka awasilishe vielelezo hivyo ndani ya siku tano.
Makinda alisema mbunge akishindwa kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni anaweza kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kushiriki vikao vitano.
Kadhalika, alisema iwapo wabunge wataona adhabu hiyo ni ndogo wanaweza kupendekeza adhabu kubwa zaidi kuchukuliwa dhidi yake.



CHANZO: NIPASHE

Ndg zangu sasa imedhihirika waziwazi kuwa Waziri Mkuu Peter K. Pinda ni mwongo tena laghai.
Kama si hivyo angerudi kwa Spika na kuuliza kulikoni ili atoe majibu sahihi kwa swala hili la ARUSHA na awaombe wananchi na mbunge wa ARUSHA samahani kwa kutoa taarifa za uongo.
Yeye aliamini taarifa za kiinterigensia za Mwema za chakachua bila kutumia vyombo vyake ipasavyo. Sasa wameumbuka yeye,SPIKA, SISIEM, serikali na wapambe wake wabunge kwa kushabikia upuuzi na mauaji ya ARUSHA. Damu za wana Arusha waliokufa zitawalaani. Shame on u people!!!!!!!!
 
Bomu la CHADEMA kwa Pinda hadharani

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Februari 16, 2011
rC.jpg

bul2.gif
Polisi wamchuuza kwa taarifa zao

bul2.gif
Mbunge Lema awasilisha hoja 10


bul2.gif
Spika ataka iwe kwa maandishi


SAKATA la vurugu na mauaji yaliyotokana na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha linaelekea kumuelemea Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Hiyo inatokana na taarifa ya kuwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda ya wiki iliyopita iliyokituhumu CHADEMA kuhusika na vurugu hizo zilizoishia katika mauaji ya watu watatu, ilitokana na maoni ya Polisi ambao katika matukio hayo wao ni watuhumiwa.
Baada ya Pinda kutoa taarifa kuhusu tukio la Arusha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, aliomba Mwongozo wa Spika, akitaka kujua mbunge anaweza kufanya nini akibaini ya kuwa “kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Taifa na Bunge ”.
Baada ya kuomba Mwongozo wa Spika, Spika Anne Makinda, alimtaka Lema kuwasilisha bungeni ushahidi wa “uongo wa Waziri Mkuu”, ifikapo juzi Jumatatu.
Hata hivyo ilipofika Jumatatu Spika Makinda aliliambia Bunge kwamba badala ya kuwasilisha bungeni, sasa Lema alitakiwa awasilishe utetezi wake kwa Spika mwenyewe kwa maandishi.
Habari za ndani na nje ya Bunge zinasema kwamba suala hilo la Lema na Waziri Mkuu Pinda limeibua makundi ambayo yameanzisha kampeni za siri zikilenga kuonyesha kuwa kwa kauli yake kuhusu vurugu na mauaji ya Arusha ambazo zilielemea utetezi wa Polisi pekee, yeye si mtu makini.
Taarifa za hakika zinasema tayari Lema amekwishakuwasilisha utetezi wake unaopingana na yale aliyoeleza Waziri Mkuu Pinda bungeni akianzia na taarifa ya kuwa waliofikwa na mauti katika vurugu na mauaji hayo ni Watanzania watatu kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda ingawa ukweli ni kwamba waliofariki dunia ni Watanzania wawili, Dennis Michael Shirima na Ismail Omary, na Mkenya, Paul Njuguna.
Hoja nyingine katika utetezi wa Lema inaelezwa ni juu ya utaratibu wa maandamano ya Arusha kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda kwamba Jeshi la Polisi lilipendekeza njia moja ya maandamano itumike lakini viongozi wa CHADEMA walikataa.
Katika utetezi wake Lema anadai kwamba si kweli kwamba Polisi walielekeza hivyo, na kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imafanikiwa kuona, Lema anasema si kweli pia kwamba waandamanaji walikaribia mita 50 kutoka Kituo cha Polisi ambako ndiko kulikozuka mauaji yale kwa vile CHADEMA kina ushahidi wa picha za video zinazoonyesha ya kuwa mmoja wa waliouawa alifikwa na mauti eneo la mbali na Kituo cha Kati cha Polisi.
“Kama ni kweli hatua zote zilichukuliwa na Jeshi la Polisi basi ni wazi kwamba watu waliouawa au kujeruhiwa waliuawa au kujeruhiwa kwenye uzio au mlango wa Kituo cha Kati cha Polisi mjini Arusha,”anasema mwanasiasa mmoja ambaye ameona sehemu ya utetezi wa Lema akirejea taarifa ya Polisi inayoashiria kuwa waandamanaji walikaribia kabisa eneo la Polisi.
Anaongeza mwanasiasa huyo: “Taarifa ya Jeshi la Polisi (aliyonukuu Pinda bungeni) haisemi ukweli wa jinsi matukio yalivyokuwa Arusha. Kwa ushahidi wa picha za video uliopo marehemu mmoja aliuawa eneo la Mianzini ambalo liko zaidi ya kilometa tatu kutoka Kituo cha Polisi cha Arusha.

“ Aidha, marehemu wa pili alipigwa risasi katika eneo la Kaloleni ambalo nalo liko zaidi ya kilometa moja kutoka kituo hicho. Ushahidi wa video unaungwa mkono na ushahidi wa watu walioshuhudia mauaji hayo wenyewe”. Kwa mujibu wa vyanzo kasha vya habari Lema atakosoa pia utaratibu wa jinsi Meya wa Arusha alivyopatikana, utaratibu ambao kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda ni halali.
Anasema Lema katika utetezi wake kuhusu utaratibu huo: “ Chini ya kanuni ya 8(3) ya Kanuni za Halmashauri, akidi katika mkutano wa kawaida wa mwaka na mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri.

“ Kwa kusoma kanuni ya 8(3) pamoja na kanuni ya 9, ni wazi kwamba Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wanatakiwa kuchaguliwa na mkutano wa kwanza wa Halmashauri.
“ Ili kukidhi matakwa ya kanuni hizi, mkutano wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Arusha ulipaswa kuwa si chini ya wajumbe 21 ambao ni theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri hiyo. Kwa maana hiyo, mkutano wa tarehe 18 Desemba haukuwa mkutano halali na viongozi wa Halmashauri
waliochaguliwa na mkutano huo hawawezi kuwa halali”.
Kipengele kingine cha utetezi wa Lema kinahusu kauli ifuatayo ya Waziri Mkuu aliposema; “Mheshimiwa Spika, yaani hata kwa hesabu tu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza hakuna namna ambavyo kwa hali ilivyokuwa kwamba mna CHADEMA wajumbe 14, mna CCM 16, utashindaje?”
Anajibu kauli hiyo Lema akisema: “Hapa Waziri Mkuu alitaka kuaminisha Bunge kwamba hata kama wajumbe wa CHADEMA wangehudhuria kwenye mkutano huo
bado wasingeshinda kwa sababu wajumbe wa CCM walikuwa wengi zaidi ya wajumbe wa CHADEMA”.
Anaendelea: “Lakini kwenye hotuba hiyo hiyo Waziri Mkuu alitoa kauli kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo ya Arusha: ‘ wakaingia awamu ya pili ya kumtafuta Naibu Meya, wakapiga kura, mjumbe wa kutoka TLP akashinda, CCM alishindwa hakupata kura
hata moja, CHADEMA hawakupata kura hata moja’. “Kama iliwezekana kwa mgombea wa TLP ambaye yuko peke yake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kupata kura za wajumbe wote wa CCM na kumshinda mgombea wa CCM
ambaye – kwa kauli ya Waziri Mkuu – hakupata kura hata moja, je, ingeshindikanaje kwa mgombea wa CHADEMA yenye wajumbe 14 kushinda? “Swali hili ni muhimu hasa kwa vile chini ya kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Arusha inasema kwamba kura ya kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake itakuwa ni ya siri! Na kama inavyofahamika, katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Hai, ni mgombea wa CHADEMA ndiye aliyeshinda pamoja na kwamba CCM ina wajumbe wengi zaidi katika Halmashauri hiyo.”
Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema mjini Dodoma, wamesema hakukuwa na sababu kwa Spika kumlazimisha Lema kuwasilisha ushahidi na badala yake angetumia busara zaidi kuimaliza hoja hiyo bila kuathiri pande zote.
“Spika ameteleza ama anakusudia kumdhalilisha Waziri Mkuu kwani hakuwa na haja ya kumlazimisha Lema awasilishe ushahidi maana hakuwa amesema Waziri Mkuu ni muongo bali aliomba mwongozo. Sasa ndiyo maana tena amebadili na kumtaka awasilishe ushahidi kwa maandishi,” anasema Mbunge mmoja wa CCM, ambaye ameomba asitajwe.

RAIA MWEMA 16/02/2011
 
Tangu zamani huyu mama alitumwa na akina Lowassa na yule kibaka mwingne Rostam, na sasa anawatumikia lakini moto wa wananchi ataupata tu
 
Watanzania tunataka kujua muongo ni nani, Sasa huyo mama anaficha nini, mwongo ndiye anaye wajibika kufuta kauli yake na kuomba samahani na ikididi kuadhibiwa. Mbona tanajikanyagakanyaga.:msela:

Msitufanye Mambumbumbu (Jangwani square itawaumbua):embarrassed:
 
Spika wa bunge anasema hatalirudisha swala la Lema Bungeni......eti atalimaliza mwenyewe. Nauliza; kama lema angeshindwa kuleta utetezi Anna makinda asingelirudisha hili swala bungeni? huyu mama anataka kutupeleka wapi? Anaendelea kuwafanya wa - TZ ni wajinga. Lema usikubali na sisi wapenda mageuzi hatukubali.
 
PM yuko sahihi kabisa na hakusema uwongo, nyie CHADEMA mliisha pewa agizo la kuacha maandamo, kwa utovu wenu wa nidhamu, kujitafutia umaarufu kwa gharama za maisha ya watu na kujifanya wajuzi kama sio wajuvi, ndiko kuliko sababisha mauaji na vurugu za Arusha.

Yaonekana ulizaliwa kwa kutanguliza makalio. Huenda hata brain ikahamia makalioni.
 
Kwa maneno haya ya spiker Ana makinda anataka
kuwaambia nini watanzania na watu wa Arusha?
Je hii sio mwanzo wa kushindwa kuliendesha bunge?
Je atahimili au yeye ndie atakuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani? Nawasilisha :source magazeti ya Leo.

Pamoja na yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote, Makinda hawezi Bunge. hana qualities hizo ni hayo ya kuwekwa to cater for mafisadi interests. na kweli ameanza. MAKINDA HAWEZI, HAWEZI,
 
Kwanza ieleweke vema, na nadhani wengi hawafahamu, Mh Lema hakumtuhumu Pinda. Baada ya maelezo ya Pinda aliomba mwongozo wa spika kutaka kujua kiongozi anayeongea uongo hi hatua gani anazochukuliwa. Hakumtaja pinda bali kiongozi.
Maoni yangu: Mh Lema hakupaswa kujibu kama alivyoagizwa na Spika Makinda, kwasababu aliomba muongozo na si kumtuhumu mtu.

Makinda: Kwa kutaka kuonyesha kuwa anajua zaidi na pengine kuwafurahisha wale waliomfikisha hapo, akakurupuka kutoka kusikojulina na kumuagiza Mh Lema alete maelezo. Hii ipo kwenye Hansard za bunge. Kibaya zaidi hakusema apeleke ofisini kwake bali apeleke bungeni.

Majibu: Nimesoma majibu ya Mh Lema (Raia mwema), kwakweli ni afadhali Makinda ameepusha aibu kwake binafsi na kwa waziri mkuu. Majibu yale yameandaaliwa na Vichwa vilivyotukuka vya Chadema. Kama Makinda haelewi basi zifanywe jitihada zaidi za kuanzisha tuition baada ya vikao vya bunge.

Mwelekeo: Huyu mama amedhamiria kuwakwamisha Chadema kwa kulinda maslahi binafsi ya kundi fulani. Amekataa hoja binafsi, na jana Mnyika ameomba suala la umeme lijadiliwe, Makinda akalirudisha katika kamati ya January kwani huo ndio ulikuwa mpango wao. Hoja nzito zipelekwe kwenye kamati. Sasa sijui watu watajadili vipi Richmond/Dowans ikiwa mwenyekiti wa kamati ya nishati ni January, na kamati ya Ulinzi na mambo ya nje (inayowahusu wawekezaji ) ni Lowasa.
Chadema jipangangeni maana bunge limezibwa kila mahali na Mafisadi. Hili kundi la mafisadi linayumbisha nchi sio siri. Lina nguvu sana na sasa naelewa kwanini Mh Pinda[/COLOR] aliwahi kusema ni watu hatari sana.

umechambua vizuri ila umeniudhi hiyo sehemu uliyomwita pinda mheshimiwa,.huyu fisadi,mwongo,mwoga kumwita mheshimiwa ni kosa,hana heshima mzee huyu,tokea awe pm kafanya kitu gani outstanding???
 
Hamna kitu kama hicho,yule mama ana umuhimu wake mkubwa tayari kwetu wanawake,ndo kwanza ameanza kazi, si rahisi kuwa spika wa bunge kama la sasa.....
watu wako tu kwenye PC zao wanaandika as if ingekuwa wao wangeweza zaidi,Makinda is more of a man kuliko wanaume wengi wanaosahau kuwa yeye ni binadamu na anakosea pia.....let her be,mng'oeni Ngeleja kwanza na Pinda ndo muende kwa yule mama.....si kujitafutia umaarufu kwa yule mnayemuona dhaifu na pengine kwa kuwa ni mwanamke.....Pinda has to go first and not Makinda.....

MAKINDA alaumiwi kwa sababu ya uanamke wake, tatizo la MAKINDA anaweka maslahi ya chama na kundi fulani ndani ya chama chao mbele kuliko Maslahi ya UMMA. Uwezo wa kuongoza anao lakini KIATU cha mahaba na upendeleo AKIVUE. Amasivyo itaonekana USPIKA ni cheo kizlicho mzidi uwezo. Haiwezekani mama kakaa BUNGENI zaidi ya miaka 30 hajanye mambo ambayo MBUNGE aliye na asiyezidi miezi mitatu MNYIKA ambaini kuwa anachemsha, yeye kaombwa muongozo badala ya kutoa muongozo anatoa karipio na kutaka uthibitisho, Sasa kulielewa hili inataka uwe mwanaume? kwa sasa mimi naamini ni mapenzi kwa CHAMA chake kuliko nchi yake ndiko kunamfanya apotoke, lakini akiendelea ni wazi itajidhihirisha kuwa si mapenzi kwa chama chake bali uwezo na uelewa mdogo alionao ndio tatizo limsumbualo.

Kumbuka PM ni mbunge kama wenzake bahati yake ni kuwa Rais kamteua kuwa PM hivyo kama mbunge anadanganya kwa nini PM nae asiweze kudanganya? je na hili inabidi uwe mwanaume kulitambua?

Kumbuka kazi ya wabunge ni kuwawakilisha wananchi kuidadisi serikali mambo mbalimbali yausuyo maslahi ya wananchi hao na Taifa kwa Ujumla, kinadharia kauli ya MBUNGE ni kauli ya wananchi wa JIMBO lake, lakini kiuhalisia kauli ya PM Bungeni ni kauli ya Serikali. Sasa Bunge anapotekeleza jukumu lake la kuihoji serikali kuhusiana na wananchi wa jimbo lake kuuwawa na serikali halafu PM anatoa jibu lisilo sahihi, MBUNGE kuhoji kama kiongozi mkubwa akipotosha/kudanganya nini kinafanyaika ni kosa?

MAKINDA anasema PM ni kiongozi mkubwa na anayepaswa kuheshimiwa, Hilo ni sahihi kabisa, lakini anayepaswa kuheshimiwa ni lazima na yeye hajiheshimu pia na kuheshimu wenzake, sijui kama kulielewa suala hilo linahitaji uwe mwanaume?

Kama PM kashindwa kujieshimu na kuwatungia uongo wenzake, kuhoji ni hatua gani inapaswa kuchukuliwa juu yake ni kosa la kukemewa?

Tatizo hapa si jinsia ya Mama MAKINDA, watu wanachohoji ni uwezo wake ktk kuliongoza BUNGE, Yupo mama HILLARY CLINTON, MAMA ROSE MIGILLO, Mama SHORTY wa UK aliyetupigania tusiumizwe kuhusu RADA nk MBONA ni wanawake lakini wameonyesha uwezo wa juu?

Tatizo si jinsia tatizo uwezo wa kiutendaji wa mama MAKINDA
 
Kama huyu mama ameamua kushughulikia swala la lema njeya BUNGE kwanini,
ALIMWAGIZA LEMA ALETE USHAHIDI WA MAANDISHI WAKIWA NDANI YA BUNGE NA HAKUSUBIRI AKAONGEA NAYE YEYE BINAFSI KAMA ANAVYOTAKA KUFANYA SASA? ,WABUNGE LEZIMA MUWE MAKINI NA MHAKIKISHE HAMBURUZWI NA HUYO MBEIJINI.
CHADEMA KUWENI MAKINI NA MHAKIKISHE JAMII INAELEZWA. KINACHOENDELEA, KWANI MAKINDA ANATAKA KUFUNIKA ISSUE,PINDA NI MWNGO AADHBIWE KAMA MBUNGE, KWANI PINDA NI MBUNGE NA ANAPASHWA AJIELEZE NDANI YA BUNGE KWANINI ANADANGANYA RAIYA NA HATA KUDHALILISHA MAREHEMU KWA KUSEMA WALIKUWA WAKIPAMBANA NA POLISI KARIBU NA KITUO CHA POLISI, MTU KAMA HUYU NI EVIL:clap2: PINDA MUST GO........................................
 
Itabidi utafute utaratibu Mh Lema na wananchi woote hasa wa Arusha waombwe radhi, haiwezekani Pinda adanganye Bungeni aachwe tu hivihivi huyu bibi Makinda anajitia aibu bure na CCM yake....
Pinda ndiyo ajue enzi za kuongea bungeni kwa mazoea kama roboti zimekwisha, sasa hivi lazima mtu afikiri kwanza kabla ya kutamka kitu chochote bungeni.....
Kaaibika mno na sura yake ile..ilikaa lo.!
 
Anne Makinda...... The worst bunge speaker ever!!!!!!!..... AAAGH!! I feel like bursting!!!!!
 
Kwa mtazamo wangu Bunge taratibu limeanza kupoteza heshima yake kwa jamii. Mafisadi wamefanikiwa kulidhibiti kupitia kwa huyu mama. Nyota mbaya huanza kuonekana asubuhi.
Utabiri: Tutegemee mengi ya ajabu katika bunge hili
Naomba hapo kwenye red ungeweka "kwa kasi ya ajabu" kwa sababu toka day 1 walianza kuchakachua kanuni za bunge na wanendelea kufanya madudu
 
Na wewe dada nilikuwa nakuheshimu sana. penye ukweli ni vizuri ukausimamia sio kushabikia makinda kwa vile ni mwanamke mwenzio. Hivyo unaonyesha udhaifu sana dada yangu. Muungwana husema yale yaliyo na ukweli na kuyasimamia. Ukweli Makinda Hili bunge litamshinda we subiri.
Na linamshinda kwa sababu ya uelewa wake mdogo na SIO JINSIA YAKE Michelle
 
Na Romana Mallya



17th February 2011

















Lema%283%29.jpg

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema)



Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema uamuzi kuhusu suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema), hautarudishwa bungeni na badala yake anakusudia kulimaliza mwenyewe.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu uamuzi wake baada ya Lema kuwasilisha vielelezo vyake vya kutetea hoja yake kama alivyotakiwa na Spika..
CHANZO: NIPASHE

No Haikubaliki na hitakubalika..! Kama anaweza kulimaliza mwenyewe...asigelianzisha mbele ya bunge ..angeacha bunge limalizike akailianze mweneye akiwa na lema mwenyee.... Tunataka limalizikie lilipoanzia.... !!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom