MAKINDA: Nusu ya wabunge wataka kuacha ubunge kutokana na hali ngumu ya maisha

Kwa nini Makinda anarudiarudia kuwasemea wabunge kuwa ni masikni na kwamba wanataka kuacha kazi KWA SABABU PESA WANAZOPATA HAZIWATOSHI?
Wabunge wanapokea milioni mbili na laki tatu na maruprupu mengine wanateseka! Je, Walimu wanaopokea laki mbili bila marupurupu! na wale wa kima cha chini nao?... Hoja yake kuwatetea wabunge kwa kulinganisha na nchi nyingine haina mshiko kabisa.mazingira ya sasa ya tanzania na watanzania ni tofauti. SPIKA CHAMBUA KABLA HUJASEMA JAMBO HADHARANI
 
Pamoja na kwamba kauli ya Makinda inatupa majibu sisi wananchi kuhusu watu kukimbilia Ubunge, lakini nahisi anchofanya huyu mama ni kutuma salamu kwa Kikwete. Makinda anamwambia (Kikwete) kama hatobadilisha msimamo kuhusu posho basi nusu ya wabunge wa CCM watatomtosa (pengine kwa kukataa kupitisha bajeti mwezi Julai?). Lakini hata kama watafanya hivyo lazima itakula kwao maana hii movie inaangaliwa na wananchi. Mliyataka wenyewe wabunge kaeni muyanywe!

kama upo kichwani mwangu vile na huyu mama akumbuke pia amekalia kiti cha basi la abiria.. wakati wowote watamuundia zengwe na watamtoa c'se kuna sababu nyingi sana za kumtoa kwenye hicho kiti kuliko za kumwacha pale. Na kama ccm kitataka kushinda 2015 ni lazima wamtoe mama kabla ya 2014

hawa mabingwa wa kuuza viwanja vya wazi unafikiri wanataka kulikoroga.. wao wameridhika na madili wanayoyapiga kwenye ngazi zao za manispaa na halmashauri..

kuna baadhi ya madiwani ni wasafi
 
Spikaa awe mkweli,na asimame atupe mfano wa mbunge anayetaka kuacha! Jamani huyu spika angekuwa mkweli angetuambia tu kwa mifano ili isije ikawa hawatutumikii kwa sababu wanataka kuacha.

Lakini hebu spika atueleze kisa cha Kafulilo kuung'ang'ania ni nn? na Hamad naye kwa aendelee kupigania kitu kisicho masilahi? Ama kweli wenye akili wameshamwelewa Spika ! Ni kiongozi yulele wa mfumo ulele unaotuliza na kutuangamiza kila siku.
 
Mbona wanaununua huo ubunge kwa kuwahonga wapiga kura? Huyu Bi Kiroboto amechanganyikiwa, mpuuzi sana huyu Kiroboto. Anamdanganya nani kama ubunge ni umaskini kwa nini asijiuzulu kuliko kulalamika?
 
Amesema wabunge waliowengi waliutafuta ubunge kwa kuwa walisikia mshahara wa bunge ni Tsh mil 12
Lakini walipoingia mjengoni wamekuta hali ni tofauti kabisa....so wanataka kuachia ngazi

wabunge wengi ni ccm na ndiyo iliyowapitisha kugombea, kwa hiyo anadhihirisha kuwa ccm haipo kwa maslahi ya tanzania bali matumbo yao?
 
MAKINDA anatakiwa kuyajua matatizo ya tanzania kwa sasa ndipo kama spika ayasemee. kama anaona kuwa tatizo la tanzania kwa sasa ni kipato kidogo cha wabunge basi kachemsha!
 
Spikaa awe mkweli,na asimame atupe mfano wa mbunge anayetaka kuacha! Jamani huyu spika angekuwa mkweli angetuambia tu kwa mifano ili isije ikawa hawatutumikii kwa sababu wanataka kuacha.

Lakini hebu spika atueleze kisa cha Kafulilo kuung'ang'ania ni nn? na Hamad naye kwann aendelee kupigania kitu kisicho masilahi? Ama kweli wenye akili wameshamwelewa Spika ! Ni kiongozi yulele wa mfumo ulele unaotuliza na kutuangamiza kila siku.
 
Kwa nini Makinda anarudiarudia kuwasemea wabunge kuwa ni masikni na kwamba wanataka kuacha kazi KWA SABABU PESA WANAZOPATA HAZIWATOSHI?
Wabunge wanapokea milioni mbili na laki tatu na maruprupu mengine wanateseka! Je, Walimu wanaopokea laki mbili bila marupurupu! na wale wa kima cha chini nao?... Hoja yake kuwatetea wabunge kwa kulinganisha na nchi nyingine haina mshiko kabisa.mazingira ya sasa ya tanzania na watanzania ni tofauti. SPIKA CHAMBUA KABLA HUJASEMA JAMBO HADHARANI
Huyu mama nahisi wa kupima huyu, sio mzima. Sisi wenzake tukiona kazi haina maslahi huwa tartiiibu tunachukua karatasi na peni tunadraft application letters kutafuta greener pastures. Yeye na wabunge wenzake nini kinachowafanya wang'ang'anie kazi isiyowalipa???Kwani wanalazimishwaga kuwa wabunge??Kama wanaona ubunge ni mzigo si wautue kama mwenzao Rostam alivyofanya???kwani lazima wafie bungeni???Waje huku mtaani zipo kazi za zaidi ya Dola elfu 20 kwa mwezi, waje wa apply wasitupigie kelele. Huyu mama anadhani watanzania ni mazezeta na hatuelewi kwanini tunapinga posho zao haramu. Kama hakutajirika miaka 30 iliyopita, basi hatajiriki tena kwa miaka yake iliyobakia. Tena hata akiweza asisubiri hadi hiyo 2015 ni mbali sana kwa mzigo na mbabaishaji kama yeye kuwa Bungeni.Aachie ngazi now.
 
hatimaye tunashuhudia mambo yanazidi kujidhihirisha nadhani kuna mengi yatajitokeza kwani makamanda wanaendelea kuchachafya mjengoni, waliwabeza na kuwakejeli sana, hatimaye matunda yanaanza kuonekana. MAKAMANDA KAZI KUBWA BADO IPO MBELE YENU HADI KIELEWEKE kwani dalili zimeanza kuonekana. tunawashukuru kwa utulivu na uvumilivu hapo mjengoni maana mnaambiwa mengi ya kuwavunja moyo. Aluta continua!!!!!!!!
 
Amesema wabunge waliowengi waliutafuta ubunge kwa kuwa walisikia mshahara wa bunge ni Tsh mil 12
Lakini walipoingia mjengoni wamekuta hali ni tofauti kabisa....so wanataka kuachia ngazi

Ni kweli kasema aisee?? Siamini!
 
Amesema wabunge waliowengi waliutafuta ubunge kwa kuwa walisikia mshahara wa bunge ni Tsh mil 12
Lakini walipoingia mjengoni wamekuta hali ni tofauti kabisa....so wanataka kuachia ngazi
Hii ina maana anazidi kututhibitishia kuwa walitafuta ubunge kwa ajili ya maslahi yao na sio kutumikia wananchi waliowachagua.
Wakiacha watakuwa wametutendea wema mkubwa.
 
Mwanzo nilikua na huzuni, kisha ikaja hasira na sasa imefika kiwango kwamba nawaonea tu huruma hawa "waheshimiwa".
 
Spikaa .... atupe mfano wa mbunge anayetaka kuacha! Lakini hebu spika atueleze kisa cha Kafulilo kuung'ang'ania ni nn? na Hamad naye kwann aendelee kupigania kitu kisicho masilahi? Ama kweli wenye akili wameshamwelewa Spika ! ....

Ajibu na haya maswali?
1. Kwani waliomba ubunge kwa nia ya kwenda kupata 12M au kuwatumikia watanzania kwa ujumla?
2. Kama walijua kazi inalipa 12M na kumbe siyo, je tuwaite ni mambumbumbu kwa kuomba kazi wasiyojua mshahara wake?
3. Kwa nini CCM inatumia bilioni tatu kupiga sarakasi za kupata jimbo kwenye uchaguzi mdogo il-hali jumla ya pesa zote atakazo lipwa mbunge kwa kipindi chake chote hazifiki hata bilioni moja? Hapa CCM huwa inauza ng'ombe ili ishinde kesi ya kulipa mbuzi?
4. Atwambie na Lyatonga naye anataka kuacha ubunge?
 
Mpuuzi mkubwa huyo bibi. Yani yeye anachokiwaza ni posho tu.. Walimu mbona hawalipwi posho!
 
Back
Top Bottom