MAKINDA: Nusu ya wabunge wataka kuacha ubunge kutokana na hali ngumu ya maisha

Wanasubiri nini kutekeleza azma hiyo ya kizalendo? Waachie ngazi fasta fasta mama Makinda wasitusumbe vichwa bila sababu
 
Let be carefully, kweli hili sio wabunge wa chama kimoja tu; wako kwenye vyama vyote ambao hawaungi mkono hoja wanajulikana, it is clear....
 
Kama wabunge hoja yao ni tofauti ya malipo baina ya bunge letu na mabunge mengine kama Kenya n.k. Basi kwa kigezo hicho hata walimu na madaktari walipwe kulingana na jinsi nchi nyingine kama Botswana n.k. wanavyolipa walimu na madaktari wao.Usawa usiwe tu kwa wabunge wa kenya na wabunge wa Tanzania tu bali hata kwa sekta na idara nyingine otherwise ni ukaburu wa wanasiasa kujiona wao ndio bora kuliko wengine.
 
Huyu mama anaposema kuwa hawa wabunge wetu wanalipwa kidogo compared na wabunge wa nchi nyingine, je anajua hali ya uchumi wa hizo nchi anazojifananisha nazo? Je anajua kiasi gani cha budget ya Kenya inatoka kwa wafadhili? Sasa mnapoomba muongezewe posho mnajua kuwa maana yake kuomba walipa kodi wa Ulaya waongezewe kodi ili nyinyi ndio wawafadhili na hiyo posho mnayolilia; huoni kama ni aibu kwa nchi tajiri kama hii? Acheni ufisadi ili nchi ipate mafanikio na uchumi ukue na hapo muombe posho zaidi.
 
Huyu mama anadhani watanzania ni walewale wa 1947..Hivi kwanini watawala wetu wanadhani sisi ni wajinga na mapunguani namna hii? Hivi kwanini huyu mama anataka watanzania tuamini hoja za kijinga kama hizi? Kama wanataka kuacha kazi waache kwanza wametuchosha sana....Hivi Dr au Prof angewezaje kuacha kazi ya kufundisha na kufanya research za mabilioni aende kwenye siasa isiyolipa? Hili ni tusi kwa watanzania,anatudharau kuwa hatujui kuwa kinachoendelea,huyu ni wa kumuadhibu kwa namna yoyote ile..tena anasema Bunge letu ndio linalipa posho ndogo kuliko mabunge yote duniani tena kwa ujasiri,shit hivi hii ni nini wakuu..hii nchi inaenda wapi?
 
huyu huyu alisema posho mpya zimeshaanza kulipwa sasa hajaeleza kilichomsibu,hapo atajua bunge si mhimili wala chochote
 
Write a comment...
[h=6]Mimi Mwanakijiji
[/h][h=6]Kama Ubunge ni "umaskini" kwanini matajiri wanafanya kazi kubwa sana kuutafuta? Ingekuwa vizuri tuwape maskini maana hao tayari "umaskini" wameshauzoea![/h]

Kweli kabisa mwanakijiji,ukweli ni kwamba wanaona aibu kwa jinsi Rais alivyowashushua na wana wasiwasi na mapokeo ya umma kuhusiana na huo ulafi wao kudhihirika hadharani.
Lakini hapa kuna Jambo moja kubwa la kujiuliza.Kama wabunge wanakabiliwa na ukata kwa kiasi hicho,ebu wajiulize mwananchi wa kawaida yuko katika hali gani kwa sasa..?
 
Wabunge maslahi waache tu kazi labda tutapata watumishi wa umma wa kweli kwenye chaguzi ndogo zitakazofata.
 
Sikia we maza, usijilinganIshe na majirani zetu, wao suala la rushwa na kubariki ufisadi
hakuna, so wanapaswa kulipwa vizuri kwani wanakaba kila mianya. Sasa wewe kabla hujaanza kulialia
Pambana na rushwa na ufisadi, na sisi tukiona tumeweza kununua angalau baiskeli, hapo ndipo mdai nyongeza.
WE WANT TO SEE THE BETTER LIFE THEN WE WILL SUPPLEMENT YOUR INCOME.
SWALI MMEFANYA NINI HADI TUWAONGEZEE MISHAHARA??? AU NI HUKO KUKAA NA KUANGALIA WATU KAMA TAKATAKA.......
 
amesema nusu ya wabunge.. CCM wana theluthi mbili ya wabunge.. so chukua idadi nzima ya wabunge wote.. toa wabunge wa CDM wote kasoro wawili.. hiyo idadi itakayobakia gawanya kwa nusu.. wanataka kuacha.. ha ha ha.. mtu mzima hatishiwi nyau eeh.



Waache tu, tumeshawajua walienda bungeni kujipa mapesa na si kutumikia wananchi. mbona huku kuna watu wengi tu watakaogombea kwa nia ya dhati ya kuwatumikia wanamchi na si after money.
 
Leo hii kaja na kali nyingine!

Mh. Spika Anna Makinda amesema nusu ya wabunge wetu wanataka kuacha ubunge kutokana na ukata,
Je, hii ni kweli? na kama ni kweli,Je, wabunge wa CDM nao wamo?

Source - ITV taharifa ya habari jioni hii

uzee unamsumbua huyo.wanaacha kwasababu ya kunyimwa nyongeza ya posho?watakuwa wametusaidi kuwajua wenye nia njema ya kutetea wananchi na wachumia tumbo.ubunge ni wito na cyo ajira
 
huyu mama mwongo mpaka yeye mwenyewe anajishangaa!
wabunge wanataka kuacha ubunge karibia nusu nani mbunge amewahi kusema hayo ! tena tutafurahi kweli kweli! Arumeru wanalogana kupata ubunge huku wanataka kuacha! ukiwa ccm ni kama wewe sio mwehu basi ni mwizi!
 
Ebu wakuu mnieleze uchumi wa Tz unazizidi nchi ngapi duniani ili tulinganishe kwa ratio ya mapato na matumizi. Ila vilevile vp vipato na posho za watumishi wengine wa umma.vp luzuku kwa wakulima?
 
atatuambia zile yutong kazitoa wapi kama kweli ubunge ni umaskini....hivi kwanini majitu yenye sura ngumu yanakuaga na roho mbaya kama huyo maza kiroboto na yule mtoto wa mafisadi anajiita mtoto wa washika jembe.watatuambia tu ,kwani zimebaki muda si mwingi sana,wote tutawafilisi na jela mtaenda hilo halipingiki....nyambaff kabisa.
 
Huyu mama anaposema kuwa hawa wabunge wetu wanalipwa kidogo compared na wabunge wa nchi nyingine, je anajua hali ya uchumi wa hizo nchi anazojifananisha nazo? Je anajua kiasi gani cha budget ya Kenya inatoka kwa wafadhili? Sasa mnapoomba muongezewe posho mnajua kuwa maana yake kuomba walipa kodi wa Ulaya waongezewe kodi ili nyinyi ndio wawafadhili na hiyo posho mnayolilia; huoni kama ni aibu kwa nchi tajiri kama hii? Acheni ufisadi ili nchi ipate mafanikio na uchumi ukue na hapo muombe posho zaidi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom