MAKINDA: Nusu ya wabunge wataka kuacha ubunge kutokana na hali ngumu ya maisha

Anayeona hawezi kufanya kazi ya Ubunge kwa kuwa ina marupurupu kidogo si aache kwani analazimishwa? Tatizo watu walitegemea kuja kuvuna pesa na maisha bora huku kwenye Ubunge, kufika wamekuta hakunaga basi ni frustration tupu! Sijui tuamue kuufanya Ubunge kazi ya kujitolea?
Hahaha!

Mkuu, unampinga kiranja wako?
 
Hahaha!

Mkuu, unampinga kiranja wako?
Kigwangalla anamaansha anachokisema, jana usiku alikuwa na Zitto Kabwe Mlimani TV na aliliongea hili bila kumung'unya maneno, huyu kijana sasa ameanza kujitambuwa na tuwaunge mkono vijana wa Magamba wenye mtazamo chanya kama huyu na Janualy Makamba.
 
Anayeona hawezi kufanya kazi ya Ubunge kwa kuwa ina marupurupu kidogo si aache kwani analazimishwa? Tatizo watu walitegemea kuja kuvuna pesa na maisha bora huku kwenye Ubunge, kufika wamekuta hakunaga basi ni frustration tupu! Sijui tuamue kuufanya Ubunge kazi ya kujitolea?

Sidhani kama Ubunge ni "hakunaga" kwa kweli; kwani hata ukiondoa faida ya kifedha (financial gains) ambazo wabunge wanazipata na nyingi bado wabunge wanapata clout kubwa katika jamii na inawafungulia milango mingi sana. Mbunge ambaye anashindwa kutumia nafasi yake ya Ubunge kutengeneza network za kufanikisha maisha yake bila kutegemea posho na njia haramu hawezi kufanikiwa hata angekuwa nje! Ndio maana watu kama kina RA ameweza kuachilia Ubunge kwa kebehi kwani hakuwa anautegemea kwa ajili ya maisha yake.

Leo hii wabunge hawawezi kuachilia Ubunge hivi hivi akawa bado timamu! Atalipa vipi madeni mengi aliyojiingiza yeye mwenyewe? Siwezi kushangaa kuwa baadhi ya wabunge wanatumia miaka ya mwanzo ya ubunge kulipa madeni mbalimbali ili hatimaye waweze kujikomboa. Matokeo yake, muhula wa ubunge kuanza kulipa kwa kweli ni ule wa pili na kuendelea! Mbunge wa muhula wa kwanza kwa kweli ni kuservice madeni mbalimbali na kujijengataratibu. Mara nyingi ni ule mwaka wa uchaguzi ndio wabunge kweli wanaanza kujionesha wanatumikia wananchi na kutafuta kusikika sikika kwenye luninga.

Hili hata hivyo haliondoi ukweli mwingine kuwa wapo kweli wabunge ambao walienda Bungeni kutumikia na hata leo wakiambiwa wauachilie watauahilia wka furaha. Kundi hili haliogopi kuuudhi wabunge wengine, haliogopi kuudhi chama chao na kwa hakika limejijenga kuwatumikia wananchi. Tatizo pekee ni kuwa kundi hili laweza lisijaribiwe sana na masuala ya fedha lakijni linajaribiwa sana na madaraka (power). Hivyo, linaweza kusacrifice financial gain kama litaweza kugain more power!

Sasa hata wale wenye kutaka kutumikia wananchi wanaweza kweli kabisa kutovutwa na fedha lakini nguvu ya madaraka ni kubwa zaidi kuliko fedha. Ukitaka kujua ni kwa kiasi gani mtu anavutwa Bungeni tuanzishe kampeni ya kupunguza ujiko wao na clout ambayo Ubunge unajenga. Vitu kama:

a. Mbunge alipwe mshahara at parity na watumishi wengine wa umma - in this case kwa mfano Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya

b. Mbunge asilipwe posho ya mafuta na badala yake alipwe mafuta kwa mwezi; akitumia zaidi ya yale anayotengewa alipe kutoka mfukoni mwake. Kiwango cha mafuta kitapangwa na watu huru baada ya utafiti wa kina. je lita 1500 kwa mwezi ni kidogo au nyingi?

c. Posho za vikao, nguo, n.k zifutwe na wabunge wanunue bima zao wenyewe.

d. POsho ya dereva ifutwe na badala yake madereva wa wabunge wawe watumishi wa umma (aidha waajiriwa wa Halmashauri au Bunge).

n.k

Tukiondoa minofu yote hiyo, tutajikuta tunabakiwa na wabunge wanaotafuta madaraka zaidi na kutumika zaidi; wale wanaotaufa fedha zaidi wataona "ubunge kweli haulipi"!
 
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! jamani jamani inatia hasira, hawa wabunge wanamtishia nani? huyu Ana makinda aka makinda ya ndege anamtishia nani? wabunge wanaotaka kuacha waache, hawa magamba shenzi zao wasitubabaishe kwanza hawana faida hata kidogo kwa nchi yetu, inamaana watanzania wengine hili janga la bidhaa kupanda bei kila kukicha sisi halituumizi au nyie ni akina nani, kwanza magamba mfe wote hamna maana nyie hata kidogo, SHAME ON YOU NA KIKWETE WENU
 
Nadhani kuna kitu nyuma ya pazia...kauli za huyu mama kwa wiki hii ni za kutatanisha....mara hatagombea ubunge 2015...mara anataka kuchukua mkopo benki ajenge...leo tena katoka kivingine!..Yangu macho na masikio...ngoja nisubiri.

Mkopo wa ngapi huo Katika Wabunge masikini Makinda si miongoni mwao nit tamaa aliyozaliwa nayo.Hapa MSASANI Jirani na MWALIMU NYERERE nyuma ya Heiniken anamiliki Maghorofa Manne yenye thamani inayokadiliwa kufikia milioni mia tano.amnbayo ameyapangisha kwa kulipwa Dola za kimarekani kwa mwezi,pale kijito nyama anamiliki Ghorofa lililosababisha kufungwa mtaa wakati wa ujenzi wake,anamiliki Ghorofa Bora njombe nzima,Dodoma anamiliki ghorofa lililokuwa la BOT BADO HUYU NI MASIKINI WA KUHITAJI POSHO ya laki mbili kweli kama sio uroho nini?
 
Hizi kauli za Makinda kwamba nusu wabunge wanataka kujiuzuru na kwamba wabunge wa Kenya wanatucheka ni saikoloji ya kitoto sana ya Makinda kutaka kumjibu JK kwa kupitia kisingizio cha "fulani anasema". Kwanza nasubiri kwa hamu jibu toka kwa wabunge wa Kenya. Huyu Makinda hapa ametafuta namna ya kumjibu JK baada ya kuona amedhalilishwa na kitendo cha JK kumkana suala posho.
 
anayeona hawezi kufanya kazi ya ubunge kwa kuwa ina marupurupu kidogo si aache kwani analazimishwa? tatizo watu walitegemea kuja kuvuna pesa na maisha bora huku kwenye ubunge, kufika wamekuta hakunaga basi ni frustration tupu! Sijui tuamue kuufanya ubunge kazi ya kujitolea?
kwenye kijani hapo kaka mkubwa,hivi kweli wako serious au wanatishia?mimi nikotayari kufanya kazi ya ubunge kwa mshahara huohuo bila posho,naomba spika asiwakatalie wakitaka kuacha kazi,sisi ndio tunajua maisha magumu huku mtaani,waambi wenzio wasitishie kujamba wakati wanaumwa ugonjwa wa kuhara watafungasha kubwa kwenye boxer,nipo tayari kufanya kazi ya ubunge kwa mshahara huhuu wa sasa bila posho nipeni kazi mimi hiyo......
 
Makinda hajasema ukweli kuhusu posho,anavyosema wabunge wa tz wanlipwa kiwango kidogo kabisa hapa duniani.analinganisha na nchi gani?utafiti huo aliufanya yeye na ndugai?au badala ya kushindwa katika nyongeza ya posho anajaribu kujenga hisia kuwa alichokuwa anakipigania kina mantiki?kwa nini ajilinganishe na wabunge wa kenya na sio mwalimu/medical doctors/nurses/n.k?huyu mama na ndugai hawajawahi kuwa watetezi wa wananchi zaidi ya kikundi kidogo cha watu walio waweka kwenye hizo nafasi,ushauri wa bure mara ya mwishoakiwa dodoma na waandishi waabari alilalamikia waandishi kumuuliza maswali ya mtego,sasa kwa maelezo yake kama haya mbona maswali yako wazi tu?eti wabunge wanataka kuacha kazi ya ubunge kwa sababu haina hela kumbe mjengoni mnaingia kutafuta hela tu baadala ya kuwatumikia wananchi na nchi yenu?hakika anne makinda unaroho mbaya sana wewe mama,ni mlafi ukiwa mkuu wa mkoa songea nilikuwa nakuona kanisani asubuhi kila siku unasali kumbe anaomba kuwaumiza watanzania wenzako,duuuuu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Daah! Mtu mzima unamtishia nyau! Kwani ana hajui kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchuuzi?
Kwanza mnazalisha nini ili tujue mwananchi ataathirika!
kama kweli muandamane tuunge mkono hoja.
 
Kitu ambacho bado kinanichanganya kwenye hii taharifa ya huyu mama ni Je, wabunge wa Chadema nao wamo
kwenye hilo sakata la kung'atuka kutokana na maslahi madogo au ni wabunge wa CCM tu?

Kwenye msafara wa Mamba na kenge wamo, Naamini hata huko CDM wapo, huko nako si malaika wenye mawazo hayo wanaweza kuwepo vipi kuhusu Shibuda na 30
 
Mbona wao hawachangii chochote au hawapo humu?noooooo wao kwanza ndo waanzilishi wa hii kitu na kwanza tumewaona,afu kwa nn waache ubunge nawakati huo walikuwa wanajua nn wanakifuata?noooooooo makinda kuwa mkweli una lako jambo au ndo unataka kutimiza ya mwanalisi kuhusu baraza jipya ndo posho?kama kuna njama zingine mseme ila sio posho kwani hilo posho limeanza saizi?wapya wangapi wameingia mjengoni ndo wameona amna masilai?ushauri wa bure naomba wanao ona posho ndogo waende kufundisha nadhani watarizika kuliko ubunge,lakini nalo litakuwa tatizo coz wengine shule haipo kabisa.
 
Back
Top Bottom