Sikupata nafasi ya kuangalia mjadala wa bunge jana kwa muda mrefu. Lakini nilibahatika kufuatilia zile debate za mwisho mwisho. Nilichojifunza ni kwamba vifungu vingi vinapitishwa kwa sababu tu wabunge wa CCM wako wengi na sio kwa uzito wa hoja.
Nilibahatika kuona mjadala kwenye kifungu cha adhabu za makosa ya barabarani na jinsi Mh Tundu Lissu alivyotoa hoja nzito ili kurekebisha kifungu hicho na kuacha kiwango cha 20,000. Majibu yaliyotolewa na Waziri wa Fedha yalinishangaza, nikajiuliza inawezekanaje mtu mwenye akili akatoa majibu yale. Alisema kwa kuwa kiwango cha adhabu kimeongezeka basi kiwango cha makosa kitapungua na hivyo kupunguza mapato kutokana na adhabu hizo. Aibu ilioje!!!!!
Ninaona kabisa kuwa CCM wanawapa nchi hii wapinzani na hasa CDM. Wanadhani wapo pale kwa ajili ya kutetea bajeti ipite tu. Wanashindwa kuelewa kwamba baada ya hapo kuna upande wa utekelezaji. Baada ya hapo kuna bajeti tena ya mwaka ujao. Kutetea tu bajeti na kupitisha kutokana na wingi wao bila kujali maslahi ya wananchi wanajipiga kitanzi wenyewe.
Lazima wajue kuwa wananchi sio wasaulifu kiasi hichi. Tutakumbuka tena haya wanayotetea kwenye bajeti ijayo wakati wanawasilisha utekelezaji wa bajeti hii. Nadhani kuanzia hapo watajifunza kuwa huwezi kuwaongopea watu wote kwa wakati wote. Nawapongeza wapinzani wote walioikataa bajeti hiyo kwa sababu za msingi walizozitoa. Kwani baadaye tutapata ushahidi wa nani alikua anasema kweli, mwaka mmoja sio mkubwa sana na 2015 sio mbali hata kidogo.