Makinda ampinga Zitto hoja ya Kumuondoa Waziri Mkuu

Kumbe Makamba sio MZALENDO kama tulivyokuwa tunajua hapo awali

Mtoto wa mamba ni mamba, mtoto wa nyoka ni nyoka, mtoto wa kenge ni kenge, ukipanda mbegu ya mahindi utavuna mahindi so GAMBA linazaa GAMBA!!
 
Hivi inamaana Mjanja Zitto wa Kabwe halijui hili au? Kaazi kweli kweli. Tuanakurupuka sana kutaka umaarufu
 
3 (a) inatumaliza watanzania, siku 14 zisipungue!!! ina maana suala hili mpaka baada ya bunge hili au itakuwaje? maana saini J3 siku 14 itakuwa lini tena? bunge si litakuwa limefungwa, mwenye ujuzi zaidi anisaidie
 
Mkuu soma katiba Ibara ya 53A na ibara ya 42. Hapo utapat utaratibu wa kikatiba jinsi ya kupiga kura ya kutokuwa na imani n PM.
 
Kifungu cha 133 (3) a) PM kitampiga chini, hizo 14 days si lazima bunge liwe mkutanoni, na 20% zipo wazi, na hoja ya namna hiyo kutokuwa na imani for 9 months haina uzito, MPs wakiamua hana la kupona, itakuwa ngumu mno la sivyo awawajibishe those sleeping & corrupt ministers....
 
Duu! Kumbe mambo hayako kama tunavyo yaona kirahisi hivyo.
hawa jamaa kabla ya kuanza kuifilisi nchi walisuka system nzima hadi katiba ili iwe vigumu kwa atakayeingilia huo mfumo.

Mi nadhani mfano mzuri ni kama wananchi wa Misri wangeamua kufuata "taratibu" kumuondoa Hosni Mubarak madarakani kwa hakika ingetumia karne nyingine moja! Sasa tuamue, kama kufuata njia ya Misri/Libya ni ngumu basi tujaribu hii ya akina Ole Millya. Kama kweli tuna uchungu na nchi hii kama wale wabunge walivyokuwa wakitokwa na mate

 
Ina maana Mh. Zitto hakulijua hili??

Kama uliangalia bunge jana utakuwa ulimsikiliza vizuri Zitto na kuelewa mchakato anaotaka kuufanya.

Katika kuwasilisha hoja ya kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, mwenye hoja anatakiwa kwanza awe na sahihi sabinni za wabunge, na ndicho alichosisitiza Zitto jana kwamba wabunge wote wenye uchungu na nchi hii kuanzia leo wajitokeze kusaini ili sasa kuanzia hapo hoja hiyo ipate kufikishwa kwa spika kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji.

Nadhani kuna watu wanajaribu kuipotosha hoja hii as if Zitto akishapata saini sabini tu, basi waziri mkuu ana step down. Tujitahidi kujiepusha na upotoshaji unaofanywa hapa, bila shaka kwa malengo maalum.

Hata alichoandika january makamba kwenye twitter yake ni katika kujipapatua tu, iko wazi kabisa kwamba Zitto ni mtu maarufu sana, hawezi kuhitaji public stunt katika hili, bali amewatega waosha vinywa wote wa ccm ili watanzania wajue ni mbunge yupi mzalendo na ni yupi domokaya.
 
kwa wale wataalamu wa mambo ya sheria na kanuni za bunge, naomba kuelimishwa,
Hivi zito anaweza kuwasilisha hoja j3, then baada ya wiki 2 (siku 14) spika akitisha kikao cha bunge kwa ajili ya kupiga kura za siri? inawezekana?

...Elewa, siku zisizopungua kumi na nne
kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni; kwa hiyo siyo lazima kikao hiki, inaweza kuwa jikao kijacho lakini notice itolewe siku kumi na nne kabla ya kikao kijacho. Kikao kijacho kinaanzawiki ya kwanza ya mwezi juni 2012, hivyo wanatakiwa kuwasilisha siku yoyote kuanzia j3 hadi tarehe 14 May 2012. Januari anataka kuwachanganya watu tu.
 
anafurahia kusafiri kwenda norway kujifunza eti namna ya kutumia mafuta na gesi hapo kesho
wao ni mainjinia wa hayo mambo? kwanini hiyo kazi wasipewe watu wa TPDC kwenda kuangalia?
hana uchungu na nchi
kanuni zitarekebishwa tu wabunge watakaa hata kwa dharura
lazima wazirir mkuu angoke
 
Back
Top Bottom