Makinda ahimize uwajibikaji badala ya kumwaga chozi la mamba......................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
02_11_c13mja.jpg
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiwa na huzuni wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick anamsomea taarifa kuhusu milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo La Mboto. Makinda ametembelea kambi ya waathirika, Mzambarauni jijini humo.(Picha na Fadhili Akida).
 
Sisi hatutaki machozi ya mamba ya Spika ila tunataka Bunge liliwajibishe serikali hii ya JK kwa maafa yasiyo na ukomo....................na kutunga sheria za kuwafidia waathirika wa maafa yanayosababishwa na uzembe..........................

Makinda ni mnafiki anapodai ya kuwa ajali haina kinga....................................that was boloney.....................................................

Hivi kama hiyo ghala ingelikuwa ilihamishiwa mbali na makazi ya watu baada ya maafa ya Mbagala kweli hiyo ajali ingelitokea na bado angeliita ni ajali haina kinga..............................

Sisi hatutaki misaada ya makato ya wabunge ila tunataka sheria za kuwalinda raia na hii serikali ambayo haimjali raia.............................na kuishia kulipa kifuta chozi au rambirambi kwa kuwafukarisha raia wake..........................kwa matukio ambayo yapo ndani ya uwezo wa mwanadamu kuyarekebisha...................
 
<table class="contentpaneopen" border="0"><tbody><tr><td class="contentheading" width="100%">Wabunge wachanga Sh37 milioni kusaidia waathirika wa mabomu </td> <td class="buttonheading" align="right" width="100%"> Send to a friend </td> </tr> </tbody></table> <table class="contentpaneopen"><tbody><tr> <td class="createdate" valign="top"> Tuesday, 22 February 2011 21:09 </td> </tr> <tr> <td valign="top">

Patricia Kimelemeta na Fidelis Butahe
BUNGE limekabidhi hundi yenye thamani ya Sh37.8 milioni kwa ajili ya waathirika wa makombora yaliyotokea Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo ni mchango wa wabunge na watumishi wa ofisi hiyo ambao kwa pamoja wameguswa na tatizo hilo na kuamua kuchangishana fedha ili kusaidia waathirika wa makombora ambao ni zaidi ya 500.

Akikabidhi fedha hizo, Spika wa Bunge, Anna Makinda, alisema baada ya kusikia tatizo hilo, wabunge hao waliguswa na walilazimika kuahirisha kikao cha Bunge ili kupata taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kwamba, wengine wana ndugu, jamaa na familia zao.

"Tulilazimika kuahirisha kikao cha Bunge baada ya kupata taarifa za milipuko, kwa sababu zilikuwa zinachanganya na wabunge walishindwa kubaini tatizo hilo kwa wakati, jambo ambalo lilisababisha kila mmoja kuona umuhimu wa kupata taarifa kamili kuhusu suala hilo," alisema Spika Makinda.

Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge hao kwa pamoja walilamizika kupitisha michango ili waweze kuwasaidia waathirika hao ambao kwa kiasi fulani wanahitaji msaada kutoka kwao.

"Ajali ni ajali tu, hata kama tutazungumza mengi bado imetokea, wajibu wetu ni kuondoa tofauti zetu na kushirikiana kwa pamoja ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu kwa sababu tunatambua umuhimu wao," alibainisha.

Hadi jana mabomu 2,204 yaliripotiwa kuokotwa maeneo mbalimbali Dar es Salaam na Kisarawe, Pwani.

Alisema wamekabidhi hundi hiyo ambayo wanaamini kuwa, inaweza kupunguza mahitaji ya waathirika hao kwa sababu ni wengi na kwamba, hawawezi kumaliza tatizo, hivyo Watanzania wenye mapenzi mema waendelee kujitokeza kusaidia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Ofisi ya Bunge itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha maafa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambao kwa pamoja ndio wasimamizi wakuu wa waathirika hao kuhakikisha tathmini ya malipo inafanywa kwa haki na kuondoa vitendo vya ubabaishaji.

Lukuvi alisema kuna baadhi ya wajanja ambao wamekuwa wakisubiri matatizo kama hayo ili kuingiza majina yao kwenye fidia na kuneemeka, jambo ambalo limesababisha serikali kulipa fidia hewa kwa baadhi ya wananchi.

Alisema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa, tathmini inayofanywa na watalaam inakuwa stahiki kwa waathirika hao.

Wakati huohuo, Chama cha Wananchi (CUF), kimetoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya Sh1.2 milioni kwa waathirika wa makombora.

Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema tatizo hilo halina itikadi, bali wananchi wote walioguswa.

Profesa Lipumba alisema kutokana na hali hiyo, CUF imeamua kukabidhi msaada huo ili kuwaenzi, kuwasaidia wananchi ambao wamekutwa na janga hilo kwa namna moja au nyingine.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, alisema serikali iko makini kuhakikisha majina ya waathirika hao wanapata malipo stahiki kulingana na ukubwa wa tatizo lake.

Sadiq alisema kutokana na hali hiyo, serikali itasimamia kwa umakini ili kuhakikisha wajanja wachache wanashindwa kuingiza majina yao.

"Tumejifunza mengi sana, hasa baadhi ya watu wanaokuja na kudai wameangukiwa na nyumba zao, lakini tunapokwenda kwenye eneo la tukio wanashindwa kuthibitisha, kutokana na hali hiyo tutakuwa makini kuhakikisha wanaolipwa fidia hizo ni wale wanaostahili peke yao," alisema Sadiq.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, alisema wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kwenye eneo la tukio ili kuona wenyewe na kutoa taarifa kwenye kikao cha Bunge kijacho.

"Tumeona tatizo lililopo na kupata taarifa kutoka kwa wahusika, ripoti yetu tutatoa kwenye kikao cha Bunge kijacho, lakini tunawaomba wananchi wawe watulivu na serikali iko kwa ajili yao," alisema Lowassa.

Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Utambuzi cha JWTZ, Meja Generali Paul Meela, alisema sio kwa Tanzania peke yake kutokea kwa makombora hayo, bali nchi nyingi za Ulaya na Afrika yanatokea.
</td></tr></tbody></table>
 
<table class="contentpaneopen" border="0"><tbody><tr><td class="contentheading" width="100%">Wabunge wachanga Sh37 milioni kusaidia waathirika wa mabomu </td> <td class="buttonheading" align="right" width="100%"> Send to a friend </td> </tr> </tbody></table> <table class="contentpaneopen"><tbody><tr> <td class="createdate" valign="top"> Tuesday, 22 February 2011 21:09 </td> </tr> <tr> <td valign="top">

Patricia Kimelemeta na Fidelis Butahe
BUNGE limekabidhi hundi yenye thamani ya Sh37.8 milioni kwa ajili ya waathirika wa makombora yaliyotokea Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo ni mchango wa wabunge na watumishi wa ofisi hiyo ambao kwa pamoja wameguswa na tatizo hilo na kuamua kuchangishana fedha ili kusaidia waathirika wa makombora ambao ni zaidi ya 500.

Akikabidhi fedha hizo, Spika wa Bunge, Anna Makinda, alisema baada ya kusikia tatizo hilo, wabunge hao waliguswa na walilazimika kuahirisha kikao cha Bunge ili kupata taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kwamba, wengine wana ndugu, jamaa na familia zao.

“Tulilazimika kuahirisha kikao cha Bunge baada ya kupata taarifa za milipuko, kwa sababu zilikuwa zinachanganya na wabunge walishindwa kubaini tatizo hilo kwa wakati, jambo ambalo lilisababisha kila mmoja kuona umuhimu wa kupata taarifa kamili kuhusu suala hilo,” alisema Spika Makinda.

Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge hao kwa pamoja walilamizika kupitisha michango ili waweze kuwasaidia waathirika hao ambao kwa kiasi fulani wanahitaji msaada kutoka kwao.

“Ajali ni ajali tu, hata kama tutazungumza mengi bado imetokea, wajibu wetu ni kuondoa tofauti zetu na kushirikiana kwa pamoja ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu kwa sababu tunatambua umuhimu wao,” alibainisha.

Hadi jana mabomu 2,204 yaliripotiwa kuokotwa maeneo mbalimbali Dar es Salaam na Kisarawe, Pwani.

Alisema wamekabidhi hundi hiyo ambayo wanaamini kuwa, inaweza kupunguza mahitaji ya waathirika hao kwa sababu ni wengi na kwamba, hawawezi kumaliza tatizo, hivyo Watanzania wenye mapenzi mema waendelee kujitokeza kusaidia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Ofisi ya Bunge itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha maafa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambao kwa pamoja ndio wasimamizi wakuu wa waathirika hao kuhakikisha tathmini ya malipo inafanywa kwa haki na kuondoa vitendo vya ubabaishaji.

Lukuvi alisema kuna baadhi ya wajanja ambao wamekuwa wakisubiri matatizo kama hayo ili kuingiza majina yao kwenye fidia na kuneemeka, jambo ambalo limesababisha serikali kulipa fidia hewa kwa baadhi ya wananchi.

Alisema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa, tathmini inayofanywa na watalaam inakuwa stahiki kwa waathirika hao.

Wakati huohuo, Chama cha Wananchi (CUF), kimetoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya Sh1.2 milioni kwa waathirika wa makombora.

Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema tatizo hilo halina itikadi, bali wananchi wote walioguswa.

Profesa Lipumba alisema kutokana na hali hiyo, CUF imeamua kukabidhi msaada huo ili kuwaenzi, kuwasaidia wananchi ambao wamekutwa na janga hilo kwa namna moja au nyingine.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, alisema serikali iko makini kuhakikisha majina ya waathirika hao wanapata malipo stahiki kulingana na ukubwa wa tatizo lake.

Sadiq alisema kutokana na hali hiyo, serikali itasimamia kwa umakini ili kuhakikisha wajanja wachache wanashindwa kuingiza majina yao.

“Tumejifunza mengi sana, hasa baadhi ya watu wanaokuja na kudai wameangukiwa na nyumba zao, lakini tunapokwenda kwenye eneo la tukio wanashindwa kuthibitisha, kutokana na hali hiyo tutakuwa makini kuhakikisha wanaolipwa fidia hizo ni wale wanaostahili peke yao,” alisema Sadiq.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, alisema wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kwenye eneo la tukio ili kuona wenyewe na kutoa taarifa kwenye kikao cha Bunge kijacho.

“Tumeona tatizo lililopo na kupata taarifa kutoka kwa wahusika, ripoti yetu tutatoa kwenye kikao cha Bunge kijacho, lakini tunawaomba wananchi wawe watulivu na serikali iko kwa ajili yao,” alisema Lowassa.

Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Utambuzi cha JWTZ, Meja Generali Paul Meela, alisema sio kwa Tanzania peke yake kutokea kwa makombora hayo, bali nchi nyingi za Ulaya na Afrika yanatokea.
</td></tr></tbody></table>
 
du mwanamke gani huwa analia akiwa serious asifute macho kwa kanga au kitambaa. yaani huyu ni mwanamke gani asiye na machozi? vidole viwili tu vinayakausha!!!
 
Kwa kweli acha shangazi yetu amwage chozi, inasikitisha na inatia uchungu sana ukiwaangalia waathirika wa mabomu. Mungu awatia nguvu daima.
 
serikali ya kinafki,utaijua tuu analia nn wakati hata yeye bungeni keshaanza kubadili sheria ili kulinda wachache?
haya yote yana mwisho ka tunayoyaona misri,tunisia....................................:decision:
 
du mwanamke gani huwa analia akiwa serious asifute macho kwa kanga au kitambaa. yaani huyu ni mwanamke gani asiye na machozi? vidole viwili tu vinayakausha!!!

Don't be insensitive!!!!!

Yo forget that even Speakers have feelings and that is her way of showing hers! Give her a break!!
 
02_11_c13mja.jpg
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiwa na huzuni wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick anamsomea taarifa kuhusu milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo La Mboto. Makinda ametembelea kambi ya waathirika, Mzambarauni jijini humo.(Picha na Fadhili Akida).
Hata mtot wa mkulima nae alilimwanga mjengoni..mbele ya kadamnasi...!! sijui ni uchungu wa kweli au ndo zao..:A S 13:
 
Anafikiria yeye amevaa earing kubwa ya dhahabu wakati kuna watu wanalala nje baada ya nyumba zao kupigwa na makombora. Baya zaidi anajuta kukataa hoja ya Tundu Lisu ya kutaka bunge lijadili hili tukio la makombora kama issue ya dhararu.
 
Hata mtot wa mkulima nae alilimwanga mjengoni..mbele ya kadamnasi...!! sijui ni uchungu wa kweli au ndo zao..:A S 13:

Hamna cha kilio hapo...usanii tu..tatizo la hawa viongozi wetu wanajiona wamehitimu Chuo Cha Sanaa Bagamoyo...wewe acha tu muda utakapofika watatoa machozi ya kweli...!!!
 
02_11_c13mja.jpg
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiwa na huzuni wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick anamsomea taarifa kuhusu milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo La Mboto. Makinda ametembelea kambi ya waathirika, Mzambarauni jijini humo.(Picha na Fadhili Akida).

Mama uwe na huzuni hivi hivi kwenye mambo yafuatayo:-
1. DOWANS
2. ATC
3. TRL
4. RADA
5. KAGODA
6. BUZWAGI
7. MELEMETA
8. TANGOLD
9. UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA - NA MATOKEO YAKE
10.
 
Anazuga tu mbele ya public aonekane ana uchungu. Mh. Lissu alipomuomba waongelee hilo suala bungeni kama dharura, Makinda alichomoa tena kwa ukaidi akisema hakuna dharura yoyote. Watu wamepoteza maisha na mali zao wewe unadai hakuna dharura. Ripoti ya milipuko ya mabomu kule Mbagala haijatoka hadi leo, UMMA haujui what's going on. Na sasa Gombo la Mboto hata hawajui, wanasubiri uchunguzi kutoka nje ya nchi. Sasa kwa nini kusiwe na udharura ili kuzuia janga lingine???
MAKINDA ACHA KUZUGA.
 
serikali ya kinafki,utaijua tuu analia nn wakati hata yeye bungeni keshaanza kubadili sheria ili kulinda wachache?
haya yote yana mwisho ka tunayoyaona misri,tunisia....................................:decision:

Kila mtu akilia nani atachukua hatua? Pinda alilia na huyu nae Spika analia! Chukua hatua ya kuwawajibisha wahusika, full stop!

Bunge limekuwa Muhimili wa Walizi?
 
Hili Libibi si ndiyo lilikataa kufanya kikao cha dharura cha Bunge, tena kwa kejeli likasema ile milipuko haiwezi kuwa dharura???
Hapo kinachomliza ni nini sasa?

!@#$%^&*(*&^%$#@!~!@#$%^&*

Bofya hapa.
 
02_11_c13mja.jpg
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiwa na huzuni wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick anamsomea taarifa kuhusu milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo La Mboto. Makinda ametembelea kambi ya waathirika, Mzambarauni jijini humo.(Picha na Fadhili Akida).

:A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:
 
Hamna cha kilio hapo...usanii tu..tatizo la hawa viongozi wetu wanajiona wamehitimu Chuo Cha Sanaa Bagamoyo...wewe acha tu muda utakapofika watatoa machozi ya kweli...!!!

Huyu BIBI NI MNAFIKI hamna lolote hapo. Angelia pia siku walipobadili kanuni ili kuweka mapandikizi kwenye kamati nyeti za Bunge. Mbona PM alipodanganya UMMA hakulia??? instead alikuwa mkali kama amekula KIJITI cha Mufindi. Siku ipo nayo yaja atatoa machozi ya ukweliiiiii.
 
Back
Top Bottom