Makinda aanza kazi aliyotumwa

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Kuna tetesi kuwa hoja binafsi ya Katiba iliyowasilishwa na Mh. Mnyika na ile ya Dowans ya Mh. Kafulila hazitajadiliwa katika kikao kijacho cha bunge kwa kisingizio cha kutoundwa kamati ya uongozi ya bunge yenye jukumu la kupitia hoja za serkali na wabunge binafsi na kuzitolea uamuzi..
Dalili hizo zimejitokeza baada pia ya spika mwanamama Makinda kusema ofisi yske haijapokea hoja binafsi ila imepokea taarifa tu za makusudio ya kuripoti hoja.

Binafsi nanusa harufu ya kutimia malengo ya waliomuweka hapo na ucheleweshaji wa makusudi ili maamuzi ya kibabe yapitishwe kwanza

Source: Nipashe Jumanne 18 January 2011
 
Kama Spika atafanya mzaha na hoja hizo mbili utakuwa mwanzo mbaya kwake; hoja ya Kafulila kuhusu Dowans inagusa suala ambalo linatishia kuvunja hadhi ya bunge lenyewe. Ikumbukwe bunge lilikwisha azimia kuwa mkataba uliofanyika baina ya TANESCO na Richmond ulikuwa batili hivyo nchi inapolazimika kulipa mabilioni ya fedha kutokana na uamuzi huo, bunge halina bidi lipewe fursa ya kutathmini, ni wapi lilikosea. Vivyo hivyo, hii hoja kuhusu katiba mpya ina maslahi makubwa ya kitaifa, na hivyo haistahili kupigwa teke
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.
 
zomba.... naona umekurupuka kutoka kwenye mashine ya kukoboa mahindi
 
Kama Spika atafanya mzaha na hoja hizo mbili utakuwa mwanzo mbaya kwake; hoja ya Kafulila kuhusu Dowans inagusa suala ambalo linatishia kuvunja hadhi ya bunge lenyewe. Ikumbukwe bunge lilikwisha azimia kuwa mkataba uliofanyika baina ya TANESCO na Richmond ulikuwa batili hivyo nchi inapolazimika kulipa mabilioni ya fedha kutokana na uamuzi huo, bunge halina bidi lipewe fursa ya kutathmini, ni wapi lilikosea. Vivyo hivyo, hii hoja kuhusu katiba mpya ina maslahi makubwa ya kitaifa, na hivyo haistahili kupigwa teke
Thubutu yake Makinda hawezi kuileta Dowans bungeni kwani atakuwa anaukata mkono wake mwenyewe ,watu walimfugia safari Iringa na kumpa ulaji eti leo hii awe na kifua cha kutaka kuwaumbua hiyo haiwezekani huenda mto Nile uanze kumwaga maji ziwa Victoria
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.

Mkuu hizo sheria wanazijua wao tu?
kuwa speaker doesnt mean u have the whole knowledge ya sheria za bunge
Lazima tuangalie hoja zenye maslahi ya umma hata kama tulizoea kusuasua kwani kujadili hoja ni kulima ndo mpaka utoke jasho?
 
Sheria na kanuni zimeundwa kwa dhumuni la kujenga taifa letu! Na c kunufaisha wachache! Vp hatuwezi kuzitwist kidogo kwa manufaa ya taifa hili 'changa' , hoja zikasikilizwa na kutolewa majibu yanayoeleweka! !
bunge linaongozwa na sheri na kanuni za bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa jf.
 
Every minute counts....pengine hilo huwa tunalisahau. And above all, usione vyaelea, vimeundwa
 
Sheria na kanuni zimeundwa kwa dhumuni la kujenga taifa letu! Na c kunufaisha wachache! Vp hatuwezi kuzitwist kidogo kwa manufaa ya taifa hili 'changa' , hoja zikasikilizwa na kutolewa majibu yanayoeleweka! !

kule mjengoni kuendesha kikao cha hawa waheshimiwa ni gharama sana sasa tunahitaji wafanye kitu cha maana kwa mustakabali wa hali tete ya taifa na sio kwenda kupiga story na kutafuna nyama za kuku chako ni chako na kuhadaa wadogo zetu wa udom
 
Nilimsikia jenerali ulimwengu kwenye mjadala wa katiba kwamba walitwist katiba kwenda kwenye simple majority, kwa hofu ya mrema, kama kwa katiba iliwezekana naamin hamna kinachoshindikana
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.

Wabunge hapo wamekurupukaje?

Ratiba ya shughuli za Bunge huandaliwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge, kwa hiyo ina maana kikao cha Bunge cha mwezi Februari hakitaweza kufanya shughuli yoyote kwa kuwa kamati hazijaundwa?

Ina maana kuunda hizo kamati na kuchagua wenyeviti wa kamati ni kazi ya wiki 2 ambazo Bunge litakaa Dodoma mwezi ujao?

Alichosema Mama Makinda ni excuse ya kutaka kupokea hoja kwanza aziweke kwenye darubini na kuzipeleka serikalini/vikao vya CCM kabla ya kutoa maamuzi kwamba zijadiliwe au la. Mbinu kama hiyo ilitumiwa na Sitta alipobana hoja ya Dr. Slaa kwa kisingizio kwamba anapeleka vielelezo polisi maana anahisi ni vya kughushi.
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.
Kwa vile na wewe umechangia JF, basi UMEKURUPUKA .............. I just using your statement
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.

Wewe ni mmoja wao.Kila siku unakurupuka kama gari bovu la mkaa kwenye down ya Kibamba.
 
Kuna tetesi kuwa hoja binafsi ya Katiba iliyowasilishwa na Mh. Mnyika na ile ya Dowans ya Mh. Kafulila hazitajadiliwa katika kikao kijacho cha bunge kwa kisingizio cha kutoundwa kamati ya uongozi ya bunge yenye jukumu la kupitia hoja za serkali na wabunge binafsi na kuzitolea uamuzi..
Dalili hizo zimejitokeza baada pia ya spika mwanamama Makinda kusema ofisi yske haijapokea hoja binafsi ila imepokea taarifa tu za makusudio ya kuripoti hoja.

Binafsi nanusa harufu ya kutimia malengo ya waliomuweka hapo na ucheleweshaji wa makusudi ili maamuzi ya kibabe yapitishwe kwanza

Source: Nipashe Jumanne 18 January 2011

KWA AMRI ZAKE................. NA UGUMU WA HOJA ALIZOTUMWA KUZIBANIA................... nina wasiwasi kama atamaliza muda wa miaka 5. Lets wait and see...........
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.

Bado kazi ipo.
Nadhani tunapshwa kuwa shauri kama wana kwenda mrama.
Si kuwa katisha tamaa.
Lengo si maslahi binafsi.:frusty:
 
KWA AMRI ZAKE................. NA UGUMU WA HOJA ALIZOTUMWA KUZIBANIA................... nina wasiwasi kama atamaliza muda wa miaka 5. Lets wait and see...........

Mkuu nina hakika yule mama atazua masongombingo kibao kwa imla zake
hana weledi huo wa kusimamia kanuni ipasavyo
 
Bunge linaongozwa na sheri na kanuni za Bunge. Hawa wabunge wapya inapaswa walijuwe hilo na wasikurupuke kama wanavyokurupuka wachangiaji wa JF.
sheria ipi inazuia hizo hoja kuwasilishwa?
 
Back
Top Bottom