Makelele ya CHADEMA yamkalisha JK nchini.

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,230
32,630
Kwenye kipindi chake cha kwanza cha utawala JK alijulikana kwa majina kama Vasco Dagama, Magellan, Columbus n.k kutokana na kusafiri karibu kila mwezi kwenda Ulaya na US kwa madai ya kwenda kutuombea misaada. Kuna wakati alitokomea huko US kwa zaidi ya mwezi.

CHADEMA na wapinzani wengine kama CUF walipiga kelele sana kutokana na ufujaji wa kodi za raia JK aliokuwa akifanya kwenye safari zake hizo zisizo na tija kama za kutembelea ofisi za google na kubembea kule kwa wapiga msuba Jamaica. Kwa sasa tangu achaguliwe sijamsikia JK kaenda US au EU. Je ni makelele ya CHADEMA na kina CUF yamemtuliza JK nchini au nchi imefilisika hadi hana hata hela ya mafuta?
 
Hakuna cha usikivu wowote huko US na Ulaya nako wamemchoka maana wanashangaa resource zinvyotapanywa wakati wao wanatumia kodi za wananchi wao kutupa misaada.
Shame!!
 
kwenye kipindi chake cha kwanza cha utawala jki kwa majina kama vasco dagama, magellan, columbus n.k kutokana na kusafiri karibu kila mwezi kwenda ulaya na us kwa madai ya kwenda kutuombea misaada. Kuna wakati alitokomea huko us kwa zaidi ya mwezi.

Chadema na wapinzani wengine kama cuf walipiga kelele sana kutokana na ufujaji wa kodi za raia jk aliokuwa akifanya kwenye safari zake hizo zisizo na tija kama za kutembelea ofisi za google na kubembea kule kwa wapiga msuba jamaica. Kwa sasa tangu achaguliwe sijamsikia jk kaenda us au eu. Je ni makelele ya chadema na kina cuf yamemtuliza jk nchini au nchi imefilisika hadi hana hata hela ya mafuta?

hivi kipindi kile alikaa sana us alikuwa anakaa white house?
 
Mmmh acheni apumzike alikuwa anahaha kutafuta ankara ili amalizie ujenzi wa ghorofa lake lililoko maeneo ya Upanga kama unakata kona ya kuelekea Muhimbili National Hospital.

Lililopewa jina la SWISS-TOWER, pia ujenzi wa hotel kubwa na ya kifahari iitwayo Malaika iliyopo Mwanza ktk wilaya ya Ilemela kando kando ya ziwa Victoria na Hotel yake JK iliyopo ktk Hifadhi ya Serengeti.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom