Duh hii ni balaa
Bora hata hawa ni mbao hazina joto sana
Nenda Arusha pale uone watu wanavyoishi kwenye nyumba za bati full kuanzia chini mpaka juu na fikiria lile joto la bati mchana ila utamkuta polisi anapikia humo humo ndani
Sidhani kama watawala wanaweza wakawajali sana hata kufikiria kuwajengea nyumba zenye hadhi ya kuishi binadamu kwa sababu chochote watakachowatuma kufanya wanakifanya bila kinyongo kwa kisingizio kwamba ni amri kutoka juu kwa wakubwa. Inawezekana hata kuishi humo nayo ni amri kutoka juu kwa wakubwa hivyo ni lazima waikubali na kuitii!
ila hao Askari wana hela balaa, wanashindana na wa-tunduma. Trust me i know them.
dah mkuu umetaja four way nikakumbuka hom.....za rombo ni nzuri in comparison na maeneo mengne,they deserve this hadi watakapokubali changes.....Ukiwakuta Four Way Bar opposite na NMB hutaamini wanavyokamata bia na mbuzi na Corolla zao wamepaki nje. Sio siri pamoja na kuishi kwenye hayo mabanda vijana wana pesa ya kutisha wanazopata kwenye dili za kuvusha mahindi na sukari kupeleka Kenya. Wengine wana nyumba zao binafsi na Noah kadhaa za kubeba abiria kwenda Moshi na Tarakea,
Mbona wanayafurahia maisha kama wapo peponi!!!!!!
Hii ni hali ya kawaida sana kwa askari wetu wengi tu na wala hakuna cha ajabu hapo.
Kama mtu ulikuwa hujui kuwa askari wa majeshi yetu ambao ni rank and file wanaishi maisha duni basi wewe huna mguso na hali halisi ilivyo Tanzania.