Makazi Ya Polisi Rombo - Miaka 50 ya Uhuru

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Makazi ya Polisi Rombo Mkuu, Mkoa wa Kilimanjaro eneo linaloitangaza Tanzania kwa walimwengu kutokana na utalii.

Inasikitisha kuona Askari polisi walivyodharaulika na kutopewa umuhimu na serikali kwa kuwaandalia makazi yenye hadhi kiafya. Mbona majeshi miengine kama jeshi la wananchi na la Kujenga taifa wana nyumba nzuri zinazolingana na hadhi yao, iweje serikali iwatelekeze jeshi la polisi ambalo muda mwingi wako busy na majukumu mazito ya kulinda raia wa nchi hii na mali zao licha ya kuwa watetezi wakubwa wa watawala? Hawa ni chombo cha kutumiwa tu bila kuangalia maslahi yao na mazingira wanayoishi.

ben.jpg

Askari polisi Rombo mkuu akitoka kwenye nyumba yake.​

ben2.jpg

Nyumba za askari polisi Rombo Mkuu kwa nyuma.

Picha kwa hisani ya Mjengwa Blg
 
kwanza mbona wanakaa kwenye nyumba nzuri sana...hii si self contained hii....full furnished house..safi sana said mwema..ukisikia maisha bora kwa watanzania ndo haya ..what else do u need jamani
 
kwanza mbona wanakaa kwenye nyumba nzuri sana...hii si self contained hii....full furnished house..safi sana said mwema..ukisikia maisha bora kwa watanzania ndo haya ..what else do u need jamani

Uminivunja mbavu, maana naona aliposimama huyo askri upande wa kushoto plywood zilizofanya ukuta zimeoza na kutoboka na kufanya shimo kubwa sijui askari anajisikiaje kuishi hapo
 
Mkuu acha utani bana.....

Kwani hayo si mabanda ya Kuku na Mbuzi?

Tutumie basi picha za nyumba wanazoishi BINADAMU ili tuzione.

Binadamu hao huwa wakali sana kuitetea CCM, nina imani nyumba zao zitakuwa na hadhi fulani.

Hii ya kuleteana picha za mabanda ya Ng'ombe wa maziwa na Kuku wa mayai tuyaache jamani. Eti humo wanaishi POLISI...

Wachaga kiboko jamani, hadi kwenye mabanda ya Wanyama wameweka Madishi ya TV? Nasikia kuna mifugo inapenda sana TV...... Halafu hiyo milango na kuta, yaani hata kwa kununua tu mbao, wangeliweka safi ila hawajali kwa sababu wanaishi humo ndani ni Wanyama/ndege.

ben.jpg

Kama humo ndani wanaishi POLISI, sasa naelewa hasira zao kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu....
 
Tukiwaona mitaani wanaonekana nadhifu hivyo lakini makazi yao bora nyumba za makuti vijijini kulika haya mabanda ya kufugia kuku.
 
Duh hii ni balaa
Bora hata hawa ni mbao hazina joto sana
Nenda Arusha pale uone watu wanavyoishi kwenye nyumba za bati full kuanzia chini mpaka juu na fikiria lile joto la bati mchana ila utamkuta polisi anapikia humo humo ndani
 
kwa mtaji huu wanachi watapigwa mabomu sana maana hawa jamaa wanao lala humu vyovyote vile hawawezi kuwaza ka binadamu!
 
Hii ni hali ya kawaida sana kwa askari wetu wengi tu na wala hakuna cha ajabu hapo.

Kama mtu ulikuwa hujui kuwa askari wa majeshi yetu ambao ni rank and file wanaishi maisha duni basi wewe huna mguso na hali halisi ilivyo Tanzania.
 
Duh hii ni balaa
Bora hata hawa ni mbao hazina joto sana
Nenda Arusha pale uone watu wanavyoishi kwenye nyumba za bati full kuanzia chini mpaka juu na fikiria lile joto la bati mchana ila utamkuta polisi anapikia humo humo ndani
Umenikubmusha nilishaona mabanda kama hayo Tabora Chuo cha Ardhi kabla hakijengewa majengo mapya.
 
Umenikubmusha nilishaona mabanda kama hayo Tabora Chuo cha Ardhi kabla hakijengewa majengo mapya.

Mkuu police wetu wanaishi maisha ya ajabu sana na duni kupita kiasi
Ila wana nguvu za kutoka hapo na kuvalishwa mabomu kwenda kuwapiga wananchi ambao wanaandamana na wakiwa wamebeba majani
Ni aibu ila ndo hivyo maisha yanasonga
 
we muone tu anatoka kwenye mabanda hayo, wana pesa balaa hao,kwa sababu ya kazi za magendo
 
Hivi huo mlango unastahili hilo komeo na kufuli kubwa namna hiyo??

ben.jpg
 
ila hao Askari wana hela balaa, wanashindana na wa-tunduma. Trust me i know them.
 
Ukiwakuta Four Way Bar opposite na NMB hutaamini wanavyokamata bia na mbuzi na Corolla zao wamepaki nje. Sio siri pamoja na kuishi kwenye hayo mabanda vijana wana pesa ya kutisha wanazopata kwenye dili za kuvusha mahindi na sukari kupeleka Kenya. Wengine wana nyumba zao binafsi na Noah kadhaa za kubeba abiria kwenda Moshi na Tarakea,

Mbona wanayafurahia maisha kama wapo peponi!!!!!!
 
Mbona hizo ni bora kuliko za Magomeni mikumi Dar es Salaam ambazo ni full Bati kuanzia kuta mpaka kwenye paa. Hawa jamaa wamepumbazwa na mfumo na wameridhika na maisha ya aina hii. Tuwaombee mabadiliko ya kifikra hususan waweze kujua haki zao za msingi kama Binadamu.
 
Back
Top Bottom