Makazi haya ni salama?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
Leo nimemkuta huyu Ndugu akiwa amestarehe chini ya daraja la Mkapa, ambapo anadai ni makazi yake, na nilipoangazaangaza niliona blanketi kwa pembeni.
Alikuwa hana wasiwasi, huku akipata chakula cha mchana, ugali+samaki aliowavua hapohapo kwenye mto Rufiji.

Je wadau, kuna usalama kwa mwenzetu huyu anayelala hapo,ukizingatia mto Rufiji una mamba kibao?
Na je hakuna madhara kwa maisha ya daraja kwa kitendo cha kuzuka kwa makazi na shughuli za binadamu chini yake?

DSC03813.JPG
DSC03825.JPG
DSC03828.JPG
 
PJ, huyo mtu ina maana kuna shughuli za kujiingizia kipato anazofanya hapo hawezi tu kuwa analala na kuamka, je uliuliza ni shughuli gani?
 
maisha bora kwa kila mtanzania na kasi zaidi,nguvu zaidi na kasi mpya!!!!!!!!!!!!!kaaaazi kwelikweli hv hili daraja halina ulinzi???maana kuna kipindi nilisikia watu wanaiba nati na kung'oa vyuma
 
leo nimemkuta huyu ndugu akiwa amestarehe chini ya daraja la mkapa, ambapo anadai ni makazi yake, na nilipoangazaangaza niliona blanketi kwa pembeni.
Alikuwa hana wasiwasi, huku akipata chakula cha mchana, ugali+samaki aliowavua hapohapo kwenye mto rufiji.

Je wadau, kuna usalama kwa mwenzetu huyu anayelala hapo,ukizingatia mto rufiji una mamba kibao?
Na je hakuna madhara kwa maisha ya daraja kwa kitendo cha kuzuka kwa makazi na shughuli za binadamu chini yake?swali la kizushi:ulikuwa unatafuta nini kule chini ya daraja hadi ukamkuta ???/?

View attachment 31960
View attachment 31961
View attachment 31962
swali la kizushi: Ulikuwa unatafuta nini kule chini ya daraja??????????
 
maisha bora kwa kila mtanzania na kasi zaidi,nguvu zaidi na kasi mpya!!!!!!!!!!!!!kaaaazi kwelikweli hv hili daraja halina ulinzi???maana kuna kipindi nilisikia watu wanaiba nati na kung'oa vyuma
Pembeni mwa daraja kuna kibanda cha polisi ambao hawafiki siku hizi.
Ulichoona PJ ni uhalifu na matumizi mabaya ya miundombinu yetu.
Nadhani Magufuli au watu wake wataiona hii.
 
Maisha yakiwa magumu kila sehemu inakuwa salama. Anatia huruma kwa sababu ana uchaguzi mdogo. Wapo wengi zaidi wanaoishi chini ya madaraja kwenye "nchi zilizoendelea", labda kwa sababu madaraja yako mengi pia.
 
Kazi nzuri pj, na wewe ulifuata nini darajani?pale si mahali salama kabisa au huyu jamaa ni mmoja wa watekaji magari pale?
 
Huyo jamaa atakuwa jambazi tu.mzee chini ya daraja ulikuwa unatafuta totoz nini?
 
PJ, huyo mtu ina maana kuna shughuli za kujiingizia kipato anazofanya hapo hawezi tu kuwa analala na kuamka, je uliuliza ni shughuli gani?
Mkuu, kama unavyoona picha,huwa anakamata samaki hapohapo kwenye maji, na anawachoma, sometimes anawauza na kurudi na kilo za unga, then maisha yanaendelea!
 
Kwa hiyo kama anashuguli ndo akae chini ya daraja?! Suppose shughuli yake ni kufungua vyuma vya daraja na kuenda kuviuza kama chuma chakavu?.
PJ, huyo mtu ina maana kuna shughuli za kujiingizia kipato anazofanya hapo hawezi tu kuwa analala na kuamka, je uliuliza ni shughuli gani?
 
Mimi naona kuna nyufa pale kwenye daraja, Picha ya kwanza na ya pili. Ni vizuri kama ni kweli ukamtumia Engineer Magufuli haraka. huyo jamaa achana naye waweza kukuta ana kazi pale maana UWT ni kiboko kwa Mbinu za Medani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom