Mie sioni tatizo lolote kwa wanachama wa CCM walioenguliwa kimajungu (Kama ilivyomtokea Slaa kipindi kile), kuhamia vyama vya upinzani. Ila wasi wasi wangu, kuna baaadhi yao ni mamluki ambao wametumwa ili kuleta mtafaruku mzito katika kinyang'anyiro hiki. Yawezekana, wakapewa nafasi ya kuwakilisha chama chochote walichohamia katika upinzani halafu wakajitoa katika siku za mwisho, na kuwaletea fadhaa wananchi, wanachama na viongozi wa chama husika.
Due diligence inatakiwa sana kwa vyama hivi kuwafanyia watu hawa.
Tatizo lingine liko kwetu kwa wanajamvi ambao wengi wenu humu mnaweza kabisa kuingia katika Siasa lakini mmebaki mnapiga makelele nje tu, na kuacha nchi yetu inashikwa na wanyang'anyi. Tulitafakari hili, hata katika uchaguzi wa 2015.
Mapato ya vyama vya upinzani ni madogo sana (not quantified) hivyo kuweza kumudu kumsimamisha mtu makini katika kila jimbo ni kazi nzito, na ndio maana kuna sehemu utakuta hamna jinsi zaidi ya kuwakubali waliotemwa Sisiemu.
Mungu Ibariki Tanzania. Tutafika tu.