Makanisa yataka katiba mpya

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
•Yasema wakati wa NEC kuvunjwa umefika
•Yataja dosari zilizojitokeza Uchaguzi Mkuu
•Yaonya wanasiasa kuchanganya ahadi na haki
•Yakosoa CCM kuingiza Kadhi kwenye Ilani

Na John Daniel
JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT) imeitaka Serikali kuhakikisha inakamilisha haraka utaratibu wa kuandikwa Katiba mpya ili kukidhi mazingira yaliyopo ndani ya nchi.Akisoma tamko la Jumuiya hiyo Dar es Salaam jana, kuhusu kasoro zilizojitokeza
wakati wa Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula, alisema wamejiridhisha kuwa kulikuwa upungufu mkubwa unaohitaji marekebisha ya haraka kwa maslahi ya Taifa.
“Ni nia yetu ya dhati kuona tunakuwa na Katiba mpya haraka iwezekanavyo itakayotungwa baada ya tafiti za kina kufanywa kwa umakini....” Kwa kusikiliza na kuzingatia sauti na utashi wa watu na uzingativu wa kutosha wa dalili za nyakati na mazingira ya nchi pamoja na kuheshimu maono na falsafa za waasisi wa Taifa letu,”alisema Askofu Kitula.
Alitaja kasoro hizo kuwa ni pamoja na udini, matusi, kejeli, vitisho na rushwa kwamba ni mambo ya hatari yalijitokeza katika mchakato huo.
“Jumuiya ya Kikristo ilipeleka waangalizi wa uchaguzi 28 kutoka ndani na nje ya nchi, tunachukua fursa hii kusema tumesikitishwa na mambo yalijitokeza kama vile rushwa ya uchaguzi iliyokithiri hata baada ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kupitishwa.
Matamshi na malalamiko yaliyotolewa na wanasiasa kuhusu udini bila kuthibitisha au kuwachukulia hatua za kisheria waliotumia udini kuvuruga amani ya nchi au kuingilia kwa makusudi ya kuchafua mchakato wa uchaguzi ama kutumia udini kama farasi au njia ya kuwaingiza madarakani ama dini kutumika kisiasa kwa nia ya kuwalaumu, kuwachafua na kuwadhalilisha wanadini walio safi,”alisema Askofu Kitula.
Alisema matumizi mabaya ya lugha za kejeli baina ya wanasiasa, vyama, viongozi na dini baina ya wafuasi, matusi ya wazi na maneno ya udhalilishaji pamoja na vitisho kwa baadhi ya maeneo kuwa dosari zinazopaswa kufanyia kazi haraka.
Alisema mchakato wa uchaguzi wa demokrasia ni njia sahihi ya kutoa fursa kwa Taifa kupata viongozi bora na waadilifu bila vurugu, uvunjifu wa amani wala kudhalilishana.
Alisema licha ya mapungufu hayo, CCT inawapongeza Watanzania kwa kuonesha m w a m k o n a m a b a d i l i k o , kutambua haki zao na kutokubali kuyumbishwa na wanasiasa.
“ Tu n a w a p o n g e z a s a n a watanzania kwa mwamko wao kisiasa, kuzijua haki zao, kujitambua haki zao na kuonesha kwa vitendo dalili za wazi kutopenda kuyumbishwa na misukumo ya kisiasa isiyo endelevu,”alisema Askofu huyo.
Alisema CCT inawapongeza Watanzania kwa utulivu na uungwana wa hali ya juu katika mazingira ambayo yangevuruga nchi.
“Tunaamini kuwa wakati umefika wa kuwa na Tume huru na mpya ya uchaguzi itayokuwa imeundwa kwa kuvishirikisha vyama vyote vya siasa, wasomi, watafiti na wadau mbalimbali. Tunaamini elimu ya kutosha kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla pamoja na taratibu huru na wazi zitakazowakilisha ari za vyama, makundi yote ya kijamii zitakazolenga kuboresha mahusiano mema ni njia pekee ya kuondokana na kero na machungu ambayo tumeyaona katika uchaguzi mwaka 2010,”alisisitiza Askofu Kitula.
Aliendelea; “vinginevyo tumeanza kuhofia kuwa chaguzi zinazopaswa kuwa huru, haki na amani sasa zinatishiwa kuwa za vurugu,uvunjifu wa amani, vitisho na mabezano, matusi na kejeli zisizotujenga kama nchi.
“Vyama viache, viepuke na vikwepe ushawishi wowote wa kutumia njia iwayo yote ya kampeni zenye ahadi za uwongo na zisizotekelezeka”alisema na kuongeza vyama vijifunze kutofautisha ahadi na haki, mfano upatikanaji wa maji, elimu, afya, na utabibu,miundo mbinu na haja nyingine ya msingi ni haki na havihitaji kuwa sehemu za ahadi kwa wanaoomba kura,”alisema.
Alisema CCT inataka vyama vya siasa kutambua kuwa uboreshaji wa njia za uchumi kwa wananchi ni wajibu wa kiongozi yeyote na siyo hisani. Alisema Jumuiya hiyo inavitaka vyama vya siasa kuwaonesha wananchi njia za kupatikana kwa mahitaji ya haki na ya msingi na kwamba watahukumiwa kwa uwajibikaji wao na siyo takrima au rushwa zinazotolewa wakati wa kampeni.
Udini
Alisema tatizo hilo lilianza mwaka 1986 na hakuna kiongozi w a S e r i k a l i a l i y e j i t o k e z a kulikemea badala yake Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilizidi kufanya makosa kwa kuingiza suala hilo katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ni kosa kuhusisha dini katika siasa na kwamba waasisi wa Taifa letu waliona hilo na kuweka bayana mahusiano kati ya dini na Katiba.
“Kazi ya kutangaza dini,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi,”alisema Askofu Kitula akinukuu Sheria ya mabadiliko ya kumi na nne katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namba moja ya mwaka 2005.
“Kuanzia miaka 1986 kulianza kujitokeza mihadhara ya kidini na kidhehebu katika jamii lakini jambo hili halikukemewa wala kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 ilitamka bayana kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, ikumbukwe kuwa mahakama ya kadhi ni jambo la kidini na kiibada katika dini ya kisilamu, jambo hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa hakuna aliyeona hatari yake na kwamba litakuwa chanzo cha udini ndani ya siasa za Tanzania, “alisema.
“Tafsiri yetu ni kwamba chama chochote cha siasa hakitakubaliwa usajili wa muda endapo kwa kufuatana na Katiba yake au sera ya chama hicho kinalenga kutetea au kuendeleza maslahi ya imani au kikundi chochote cha kidini.
pamoja na kwamba CCM iliondoa kifungu hiki katika Ilani ya 2010 bado mbegu ya udini haikuondoka kwani baadhi ya viongozi wa kisiasa na dini bado wanaendelea kulizungumzia,”alisema.
Kejeli na matusi
Lugha za kejeli na matusi vilitumika bila aibu na kwa makusudi kabisa, mbaya zaidi ni pale ambapo mgombea wa ubunge wa CHADEMA alipomtukana mgombea urais wa CCM, jambo hili lilishtua na kusikitisha Taifa zima,”alisema Askofu Kitule.
Alisema CCT inalaani vitisho vilivyotolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na kwamba vilichangia wapiga kura wengi kushindwa kujitokeza kwa hofu ya kushughulikiwa na chombo hicho kikubwa zaidi cha dola.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watanzania watatu waliuawa kikatili wakati wa kampeni huko Musoma, Maswa na Kibakwe, jambo la kusikitisha hadi leo hakuna kiongozi wa chama chochote anayesema wala kemeo,”alisema.
Alisema licha ya uchaguzi na kazi ya kuhesabu kura kufanyika kwa amani, dosari kubwa ilijitokeza baada ya vyombo vya dola kuingilia mchakato huo wakati wa kusafirisha masanduku ta kura huku baadhi ya mawakala wakifichwa.
“Tunaona kuwa ni ishara ya kujenga mazingira yanayoweza kuendeleza uvunjaji wa amani, hali hii ikiachwa itakuwa donda ndugu katika nchi nzima,”alionya.
Alisema CCT inatoa wito kwa vyombo vya usalama kubaki na wajibu wa kulinda wananchi na mali zao, vyama vyote bila upendeleo wala vitisho.
“Vyombo vya ulinzi na usalama vione kuwa ulimwengu tunaoishi ni wa mabadiliko, ni wajibu wa vyombo hivyo kwenda na kulinda michakato ya mabadiliko bila kuathiri uhuru na haki ya watu kuchagua viongozi wao kidemokrasia,”alisisitiza.
Wakijibu maswali ya waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa CCT Askofu Dkt. Valentino Mokiwa, alisema hakuna sababu ya Taifa kwenda kama kipofu kwa kupapasa. Alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kufuata Katiba na maelekezo ya kisheria na kuachana na udini ili kunusuru amani na utulivu wa nchi.
“Suala la Mahakama ya Kadhi inapaswa kuzikwa kabisa na wala lisiwepo tena midomoni mwa wanasiasa, nisingependa kodi yangu itumike kujadili mahakama ya kadhi, hakuna kitu kitakachojadiliwa Bungeni bila kodi ya mwananchi kutumika."Ningepende kodi itumike kupeleka dawa hospitali, suala hili life kabisa, libaki la kidini kama Mokiwa anavyoweza kuwa na idara yake ya maendeleo ndani ya Kanisa bila kutegemea kodi ya wananchi,”alisema.
Viongozi hawa pia waliipongeza Serikali hatua ya kuundwa kwa Serikali ya umoja kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF) na kuwataka wanaopinga suala hilo kufunga midomo.
Hata hivyo viongozi hao walikosoa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa kuwataja mawaziri na viongozi kadhaa wa Serikali ya Kenya kuhusika na mauaji ya watu baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na kuhoji kwanini wahusika wa mauaji ya Iraki wasitajwe wala kushitakiwa? .
 
Back
Top Bottom