Makanisa, sadaka na ndoa

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Habarini Wana Jf
Hili imebidi nililete hapa kulichangia kuona kama kuna ukweli wowote! Leo nikiwa lunch sehemu flani nzuri sana nilikuwa nimeketi karibu na group (nafikiri ni watu wanafanya kazi sehemu moja) la watu ambapo kulikuwa na mjadala kuhusu, Ongezeko la makanisa ambayo uhubiri mahusiano ya ndoa na utoaji wa sadaka kwa wingi siku za ibada! Wakati nashushia soda yangu nilishtushwa kwa kile mmoja wapo alichosema kuwa ongezeko hilo si Mpango wa Mungu ndiyo maana pamoja na mafunzo mengi ya ndoa lakini ndoa nyingi huvunjika na yamekuwa yakihamasisha hasa utoaji wa sadaka ili kulimbikiza mihela ambayo huchukuliwa kutoka kwa waumini! Haikuishia hapo mjadala uliendelea na kufikia kusema Mikoa inayoongoza kwa Uchipuaji wa makanisa, hasa ya aina hii ni Arusha na Mbeya

SWALI:
Je kuna ukweli wowote? Maoni kutoka katika mikoa tajwa hapo juu!!!
Je kuna athari zozote ambazo zinatokana na mafundisho hasa ya ndoa ambayo yanapelekea ndoa nyingi kupukutika?

Naomba mawazo yenu! maana huu mjadala wa hawa jamaaa ulinivutia na kutaka kujua zaidi
Thanx
Kimbweka!!!!!
 
nenda kamuulize mchungaji wako,nadhani atakua na data na ukweli kamili kuhusu haya mambo
 
nenda kamuulize mchungaji wako,nadhani atakua na data na ukweli kamili kuhusu haya mambo

Mie sina mchungaji mkuu ndiyo maana nimeuliza na najua JF wachungaji hawakosekani.....
 
Mie sina mchungaji mkuu ndiyo maana nimeuliza na najua JF wachungaji hawakosekani.....

o.k nimekumbuka rev.masanilo atakuambia,........lakn sidhani kama atakubali kuweka hadharani janja yao ya nyani...asipokuambia nakuahidi jpili nitamuuliza mchunga kondoo wangu halafu ntakujuza.
 
Wafalme 3:4Suleiman akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile..mbele tunaona Suleiman akibarikiwa utajiri,hekima, maarifa, maisha marefu nk. kupita wanadamu wengine..kuna uhusiano ktk kutoa na kupokea..Kristo anasema ni heri kutoa kuliko kupokea..budha wanatoa sadaka,moslems wanatoa,pagans wanatoa sadaka sijui wewe dini gani...wasihubiri ndoa unataka wahubiri nini..mbona kuna ndoa za futari..mkeka nk....au...ndo nyani haoni kundule..!?
 
o.k nimekumbuka rev.masanilo atakuambia,........lakn sidhani kama atakubali kuweka hadharani janja yao ya nyani...asipokuambia nakuahidi jpili nitamuuliza mchunga kondoo wangu halafu ntakujuza.
<br />
<br />
au Pdiddy, nae ana asili ya uchungaji.
 
mimi nitamjuza manake mie ni mchungaji mstaafu. ila inabidi utoe sadaka ya kuuliza manake ww mkubwa mno kwa kipaimara. hayo maswali ulitakiwa uulize kwenye tuisheni ya bure ya sunday skuli ama kipaimara!

o.k nimekumbuka rev.masanilo atakuambia,........lakn sidhani kama atakubali kuweka hadharani janja yao ya nyani...asipokuambia nakuahidi jpili nitamuuliza mchunga kondoo wangu halafu ntakujuza.
<br />
<br />
 
Ndio maana tunaambiwa tutoe tulicho nacho, na ukiwa unatoa jiambie moyoni unatoa sadaka ikafanye kazi ya bwana Mungu wako
kwa hiyo hata wakila dhambi inawaangukia wao wakuu wa makanisa, na sio wewe
 
ujasiriamali ni kila mahali sikuhizi

wachungaji wale wapi,wandugu kuweni makini na makanisa haya yanayomilikiwa na Mr,na Mrs.
 
Wafalme 3:4Suleiman akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile..mbele tunaona Suleiman akibarikiwa utajiri,hekima, maarifa, maisha marefu nk. kupita wanadamu wengine..kuna uhusiano ktk kutoa na kupokea..Kristo anasema ni heri kutoa kuliko kupokea..budha wanatoa sadaka,moslems wanatoa,pagans wanatoa sadaka sijui wewe dini gani...wasihubiri ndoa unataka wahubiri nini..mbona kuna ndoa za futari..mkeka nk....au...ndo nyani haoni kundule..!?

Inaelekea wazazi wako ni wazee wa kanisa ama wachungaji...
 
Back
Top Bottom