Makanisa, misikiti, Chuo Kikuu kufutwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki ni miongoni mwa asasi za kiraia 200 zinazokusudiwa kufutwa na serikali.
Hatua hiyo imebainika kupitia tangazo la notisi ya siku 30 ya kusudio la kufutwa kwa asasi hizo, kwa mujibu wa sheria ya muunganisho wa wadhamini, sura ya 318, toleo la 2002.
Katika orodha ya asasi hizo yapo mashirika ya kitawa ya Kanisa Katoliki, Kanisa la Pentekoste, taasisi za Kiislamu na zile zinazojishughulisha na maendeleo ya jamii.
Kaimu Msimamizi Mkuu wa Wadhamini katika ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Phillip Saliboko, alisema hatua hiyo inatokana na asasi hizo kushindwa kutekeleza majukumu na wajibu wao.
Utekelezji huo ulipaswa kufanyika kwa kutoa taarifa ya mabadiliko katika asasi hizo na kutofanya marejesho ya wadhamini kwa kipindi kirefu baada ya usajili.
“Kwa hiyo ninatoa taarifa ya kwamba ninakusudia kufuta udhamini wa asasi hizo baada ya kuisha kwa kipindi cha siku 30 baada ya tarehe ya notisi hii,” alisema katika taarifa hiyo.
Saliboko alisema kusudio hilo linaweza kubadilika kama kutakuwa na sababu za msingi na za kisheria zitakazomridhisha asichukue hatua hiyo.
Baadhi ya asasi zinazotajwa katika kusudio hilo ni pamoja na makanisa ya Pentekoste yaliyopo Iduguta, Morogoro na Korogwe, Pallottine Missionary Sister of the Catholic Apostolate na Masista wa Huruma wa Mtakatifu Visenti wa Paolo wa Innsbruck.
Pia lipo kanisa la jimbo la Tanzania Anglikana la Sumbawanga na Local Spiritual Assembly of Bahai’s ya Ubungo, Moshi, Kakunga na Kigoma.
Asasi nyingine za kidini ni Haidariyya Islamic Centre, Masjid Ghalib Islamic Centre, Masjid Nuurul Islamic Women Madrasat, Arya Samaj Arusha na Masjid Quadiria Mbagala Charambe.
Pamoja na asasi hizo, pia zipo nyingine nyingi zinazojihusisha na maendeleo ya kijamii, zikiwa zimeenea nchi nzima.
Hii ni mara ya pili katika siku za hivi karibuni Rita kutoa notisi ya kusudio la kufuta asasi kama hizo, baada ya ile iliyotolewa mwaka jana ikilenga kufutwa kwa orodha ndefu kama ya sasa.
Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa muda wa siku 30 nyingi ya asasi hizo zilikuwa zimewasilisha utetezi wake, hivyo kuingia katika mchakato mpya wa majadiliano na Rita

CHANZO: NIPASHE
 
sababu za msingi za kufuta mashirika hayo ni nini? serikali hii kweli haina priority, ingekua bize na mambo yanayogusa jamii badala ya kujikita kwenye mambo yasiyo na tija
 
Back
Top Bottom