Makanisa mawili yashambuliwa Nigeria

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
120311144300_jos_view_304x171_afp.jpg


Mashambulio dhidi ya makanisa mawili nchini Nigeria yameuwa watu kama wanne.

Shambulio kubwa lilifanywa katika mji wa Jos, katikati mwa Nigeria.
Wakuu wanasema watu watatu walikufa na zaidi ya 40 kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitolea mhanga, alipojiripuanje ya kanisa.
Kishindo cha mripuko huo kilibomoa sehemu ya jengo.
Shambulio la pili lilifanywa katika mji wa Biu, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Nigeria-attack-in-Nigeria.jpg

Polisi walisema wanaume kadha waliokuwa na silaha, walifyatua risasi wakati wa ibada ya asubuhi, na kumuuwa mwanamke mmoja.
Hakuna aliyekiri kuhusika na mashambulio hayo.


Katika miezi ya karibuni, wapiganaji wa Kiislamu wa kundila Boko Haram wamefanya mashambulio kadha kwa bunduki na mabomu.

source BBC SWAHILI
 
UAMSHO wasipothibitiwa watakua Boko haram na wataendelea kuchoma makanisa na wakasahau kuwa Wakristo wangekua na uovu huo kusingekuwepo waislam coz Ukristo ulikuwepo karne 6 kabla ya Uislam kuanza.
 
Sisi tunamwachia Mungu pekee atupiganie.... Hatutaki Kumpigania. Roho ya chuki hatuna
 
Kama wanadamu watavumiliana kidini itapendeza sana. Coz hutapata hasara yoyote ikiwa mtu/watu hawatajiunga na DINI unayoipenda. Mbinguni/Peponi kila mtu ataenda binafsi. Hakuna kundi la boko, uamsho, walokole, wanakwaya au viongozi wa dini! ni suala la nafsi ya mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom