Jinsi ya kupika makande

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,764
2,581
Nimepiga plan ya kusimplify mambo hapa mjini nikaamua kwamba! kila weekend especially Jumapili ni mwendo wa kande tu..kwanza na minimize cost.

Nitanunua..Maharage nusu
Njugu Nusu
Karanga Nusu
Mahindi Nusu na Nazi mbili na Mchicha fungu 5... Msosi simple but very smart..Hutaki Acha!

========
Makande ni chakula chenye mchanganyiko wa nafaka mbalimbali kama mahindi, maharage,njugu, mtama au ngano isiyokobolewa.

Mahitaji
  • Mahindi yaliyokobolewa(makande)kg1
  • Nazi 1 kubwa
  • Swaumu iliyosagwa & tangawizi vijiko 4
  • Maharage nusu kg
  • Nyanya 3
  • Vitunguu maji 2
  • Hoho 3
  • Karoti 3
  • Ajinamoto nusu kijiko cha chai
  • Chumvi kiasi
  • Celery kuchu 1
  • Mafuta ya kulanprobo kikombe
  • Mboga za majani kuchu 1
Jinsi ya kupika,hatua kwa hatua

  1. Osha mahindi na maharage kisha injika jikoni baada ya nusu saa weka mahindi kisha funika yaendelee kuiva.
  2. Kuna nazi yako weka tui la kwanza zito, kisha saga nyanya ziweke tayari Kwa kupikwa.
  3. Kata vitunguu, karoti na hoho mtindo wa quips.
  4. Baada ya hapo weka anagalia kama makande yameiva
  5. Kisha weka sufuria yako ya kuungia jikoni, weka kitunguu maji baada ya dakika 1 au 2 tia mchanganyiko wako wa swaum na tangawizi endelea kukoroga.
  6. Tia nyanya uliyosaga kisha funika kidogo iive baada ya hapo weka makande.
  7. Endelea kukoroga kisha punguzia moto chakula chako kiive taratibu ukishaona yameiva vizuri tia tui la nazi na koroga ili lisikatike. Epua andaa mezani

Pia unaweza pika ya mtindo huu

Katika mapishi haya tunatumia nazi na karanga. Ni chakula bora chenye ladha bora na kukupa hamu ya kujiramba.

Mahitaji
  • Mahindi yaliyokobolewa – kilo 1½
  • Maharage ½ kilo
  • Vitunguu maji 3
  • Nyanya 2
  • Karanga ¼ kilo
  • Njugu mawe ½ kilo
  • Pilipili hoho 1
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Mafuta ¼ lita
  • Nazi kubwa 2.
Maelekezo
  • Chambua maharage, mahindi, karanga na njugu mawe kisha osha vizuri.
  • Changanya maharage, mahindi na njungumawe pamoja.
  • Bandika sufuria ya maji jikoni. Weka mchanganyiko wa maharage, weka chumvi kisha acha mchanganyiko uchemke vizuri. Kwa kawaida maharage yanachukua muda mrefu kuiva vizuri. Hivyo unaweza kusubiria takribani dakika 25-30 ili kuhakikisha yameiva. Kama maji yakikauka kabla ya maharage kuiva, ongeza maji kiasi ili yaive vizuri.
  • Andaa vitunguu, pilipili hoho na nyanya kwa kuosha kisha kuvikata vipande vidogo vidogo. Weka vizuri na kusubiria kuvichanganya na makande.
  • Andaa tui la nazi kwa kuchuja tui zito ili liwe tayari kuchanganya na chakula.
  • Kama maharage na njugumawe yakikaribia kuiva (takribani dakika 30) weka karanga kwenye mchanganyiko. Koroga ili vichanganyike vizuri. Acha iendelee kuchemka na subiria hadi mchanganyiko uive vizuri. Mchanganyiko ukiiva vizuri toa jikoni na hifadhi pembeni.
  • Bandika sufuria, weka mafuta ya kula kisha acha yachemke.
  • Mafuta yakipata moto vizuri weka vitunguu kisha koroga koroga hadi vibadilike rangi na kuanza kuwa na rangi ya udongo.
  • Weka pilipili hoho, karoti. Koroga kiasi kwa muda wa dakika 2 hadi 3.
  • Weka nyanya, koroga kiasi na kisha funika na mfuniko. Acha nyanya ziive vizuri kwa mvuke ili ziwe laini. Baada ya dakika 6-8 unaweza kuponda ua kusaga nyanya ili kupata mchuzi wenye rojo. Koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.
  • Nyanya zikiiva vizuri weka mchanganyiko wa maharage kwenye sufuria. Koroga vizuri hadi mchangyiko uwe sawia. Onja ili kujua kama kiwango cha chumvi kinatosha. Unaweza kuongeza kama haitoshi.
  • Weka tui la nazi huku ukikoroga ili kuzuia tui kukatika. Koroga hadi ianze kuchemka.
  • Funika sufuria na subiria kwa muda wa dakika 10, kisha ipua chakula jikoni ili upate kujiramba.
1594387756493.png

Michango ya wadau

Mimi huwa nayapenda ya Nazi m
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa

*Kitunguu maji

*mafuta ya kupikia kiasi

*Karoti (ukipenda)

*Hiriki

*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata...

Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja...

Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa...

Mimi huyaweka na sukari pia ...
----
Jee inajuwa jinsi ya kupika makande?

Makande ni chakula cha mchanganyiko wa mahindi na maharage pamoja na vikorombwezo vingine kama vile vitunguu,karoti,hoho muda mwingine hata nyanya unaweza kuweka.
Katika mapishi ya makande unaweza kuunga kwa kutumia mafuta au ukaweka hata nazi.

Hivi ndivyo jinsi ya kupika makande ya nazi,karibuni sana

Mimi huwa nayapenda ya Nazi
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa
*Kitunguu maji
*mafuta ya kupikia kiasi
*Karoti (ukipenda)
*Hiriki
View attachment 477880*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata... Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja... Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa... Mimi huyaweka na sukari pia ... Hebu jaribu kumtagi na mwenzio aje naye ajuwe ni namna gani ya kupika makande.
 
Umenikumbusha jana wife kapika kitu cha mahindi mabichi njugu karanga njegere haragwe nazi na kachumbari pembeni kwa kweli wabena kwa kande kashinda nazo toka jana mpaka leo mimi nimekimbilia bar ila ni bonge la menu protin hapo mechi yake.
 
Hahahahahaha!nimecheka sana lol!mkuu umetisha kwa huo utaratibu ndan ya mwezi mmoja tu msg itakua send and delivared kwa wahusika,hahahaha!chezea kukuta menu ya makande kila wakitia timu!
 
Wadau mambo.

Naomba kujua jinsi ya kupika makande mapishi mbalimbali.

Asante
:yo:
 
Mimi huwa nayapenda ya Nazi m
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa

*Kitunguu maji

*mafuta ya kupikia kiasi

*Karoti (ukipenda)

*Hiriki

*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata...

Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja...

Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa...

Mimi huyaweka na sukari pia ...
 
Mimi huwa nayapenda ya Nazi m
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa

*Kitunguu maji

*mafuta ya kupikia kiasi

*Karoti (ukipenda)

*Hiriki

*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata...

Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja...

Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa...

Mimi huyaweka na sukari pia ...

Safi sana..
 
Jama mi bado sjayajulia makande. hasa kile kipimo cha maharage na mahindi. nsaidieni pls
 
Mimi huwa nayapenda ya Nazi m
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa

*Kitunguu maji

*mafuta ya kupikia kiasi

*Karoti (ukipenda)

*Hiriki

*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata...

Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja...

Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa...

Mimi huyaweka na sukari pia ...

Sante sana, hii imetulia . nsaidie ratio ya mahindi na maharage best
 
sante sana, hii imetulia . nsaidie ratio ya mahindi na maharage best

Inategemea unapendaje, ila me napenda maharage yazidi, so mahindi yakiwa nusu maharage naweka nusu na robo...
 
Zamani nillikua nayachukia makande nikaja kupikiwa na mama yangu makande ya Nazi achaaaaaa nikaanza kuyapenda ila sasa hivi mbele ya kande la wese hunambiii yani unakula na kale ka harufu ka kitunguu unakasikia na vi karoti na hoho kwa mbali ila sjui ni ugonjwa au nini ukitaka makande ya Nazi niyale niyafaidi niwekee kitunguu swaumu lol leo napika hakya mama umentoa mate wewe!!
Mimi huwa nayapenda ya Nazi m
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa

*Kitunguu maji

*mafuta ya kupikia kiasi

*Karoti (ukipenda)

*Hiriki

*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata...

Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja...

Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa...

Mimi huyaweka na sukari pia ...
 
zamani nillikua nayachukia makande nikaja kupikiwa na mama yangu makande ya Nazi achaaaaaa nikaanza kuyapenda ila sasa hivi mbele ya kande la wese hunambiii yani unakula na kale ka harufu ka kitunguu unakasikia na vi karoti na hoho kwa mbali ila sjui ni ugonjwa au nini ukitaka makande ya Nazi niyale niyafaidi niwekee kitunguu swaumu lol leo napika hakya mama umentoa mate wewe!!

Hahaha, hivi ushajaribu maharage ya Nazi Yalotiwa kitunguu saumu na nyanya ? Matamu balaa
 
Hahaha, hivi ushajaribu maharage ya Nazi Yalotiwa kitunguu saumu na nyanya ? Matamu balaa

Acha kabisa kitu kina kaharufu mimi ni very addicted na vitunguu swaumu napenda haruf yake kwa kweli harage la Nazi ulichanganye na tangawizi na swaumu halaf Nazi ikoleee mmmh matamuje
 
Waungwana,

Nina hamu na makande na ninataka kuyapika.

Je niweke vitu gani ili msosi unoge? Pia, maharagwe na mahindi nayaweka pamoja au nasubirisha kuweka maharagwe?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom